MREMA Kama mimi ni mzee, mbona Slaa ni mzee kuliko Kikwete? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MREMA Kama mimi ni mzee, mbona Slaa ni mzee kuliko Kikwete?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pengo, Oct 5, 2010.

 1. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na Elvan Stambuli-Globalpublishers
  Mgombea ubunge katika Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP, Augustine Lyatonga Mrema, amesema anapanga kujibu mapigo kwa kuhamishia nguvu zake katika majimbo matatu ambako Chadema wana matumaini ya ushindi kutokana na chama hicho kumharibia kwa kuwaambia wapiga kura wake kuwa wasimchague kwa kuwa ni mzee.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa simu akiwa Moshi, Mrema alisema anashangazwa sana na propaganda za Chadema kuwaambia wapiga kura kuwa wasimpe kura kwa sababu ni mzee na kwamba anaweza kufia bungeni.

  “Kama wao wanadai kuwa mimi ni mzee eti niwaachie vijana, sasa mimi niulize kati ya Kikwete na Dk. Slaa, nani mzee?
  Kama ni uzee basi inatakiwa Slaa amwachie Kikwete uongozi, kama Slaa anataka kwenda Ikulu naye atafia huko, waniache nami nifie bungeni, mbona kuna wabunge wanafia humo?

  “Kama Chadema inavyogawa kura zangu Vunjo, vivyo hivyo nami nitahakikisha Mbowe, Mrema na Ndesamburo, hawanusi Bunge …nitafanya kampeni kubwa katika majimbo yao, kuhakikisha TLP inakuwa na wapiga kura wengi, ili kuzuia ushindi wanaotarajia Chadema, nitahakikisha hadi kinaeleweka,” alisema Mrema.

  Amesisitiza kwamba, haendi kwa bahati mbaya katika majimbo hayo, bali nia ni kuwavurugia kama chama hicho kinavyomtibulia mipango yake ya kuingia bungeni, baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31.
  Alisema kutokana na kufanyiwa siasa chafu na Chadema, sasa chama chake kitahakikisha kinaelekeza nguvu Hai anakogombea Freeman Mbowe, Vunjo anakogombea John Mrema na Moshi Mjini anakowania Philemon Ndesamburo.

  Mrema alisema madhumuni ya kuelekeza nguvu katika majimbo hayo ni kutokana na alichokiita upinzani wa kinafiki unaofanywa na Chadema, ambapo alisema kauli ya Chadema kuwa Mrema atakwenda kufia bungeni ni matusi huku akisisitiza kwamba hakuna mtu asiyekufa katika dunia hii na akasisitiza kama ni kufa aachwe akafie huko kwa kuwa ana uchungu wa kutetea watu wa jimbo lake.

  Aliwaonya mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa, Mwenyekiti Mbowe na Ndesamburo kutokanyaga jimbo la Vunjo na kama wataamua kwenda waende kistaarabu.

  “Wakiendelea kunichezea rafu za kisiasa, nitatahakikisha kati yao hakuna anayeshinda katika uchaguzi mkuu, kwani nitafanya kampeni za nguvu kuhakikisha nagawa kura za Hai na Moshi Mjini,” alisema Mrema.

  Aliongeza kuwa, anashangazwa na upinzani uliopo sasa miongoni mwa vyama vya upinzani kwani havijalenga kuchukua madaraka ya nchi hii kama baadhi ya viongozi wanavyowahubiria wananchi bali kushambuliana, jambo linalozidi kudhoofisha kambi ya wapinzani na kuiacha CCM ikitamba.

  Wananchi wa Jimbo la Vunjo wanamfahamu Mrema kama mwanasiasa mkongwe ambaye aliwahi kuwawakilisha vema wapiga kura wake na kutokana na uchapa kazi wake Rais wa awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassani Mwinyi aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi.

  Katika enzi zake za uwaziri, Mrema anakumbukwa na wananchi wengi kwa sera zake za kuwapa watuhumiwa mbalimbali siku saba au kuwaamuru kuripoti ofisini kwake.

  Alikuwa akijiita polisi namba moja na aliwahi kukamata dhahabu yenye thamani ya mamilioni ya shilingi ambayo ilikuwa ikisafirishwa nje ya nchi kwa magendo.

  Aidha, akiwa upinzani, aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi na aliliwakilisha vema jimbo hilo.
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Mrema tumeshasema ni PSYCHIATRIC CASE.Hana jipya zaidi ya kutaka aonewe huruma.Funga mada han impact kwenye duru za siasa
   
 3. E

  ELIHURUMA Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Globalpublishers
  Mgombea ubunge katika Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP, Augustine Lyatonga Mrema, amesema anapanga kujibu mapigo kwa kuhamishia nguvu zake katika majimbo matatu ambako Chadema wana matumaini ya ushindi kutokana na chama hicho kumharibia kwa kuwaambia wapiga kura wake kuwa wasimchague kwa kuwa ni mzee.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa simu akiwa Moshi, Mrema alisema anashangazwa sana na propaganda za Chadema kuwaambia wapiga kura kuwa wasimpe kura kwa sababu ni mzee na kwamba anaweza kufia bungeni.

  "Kama wao wanadai kuwa mimi ni mzee eti niwaachie vijana, sasa mimi niulize kati ya Kikwete na Dk. Slaa, nani mzee?
  Kama ni uzee basi inatakiwa Slaa amwachie Kikwete uongozi, kama Slaa anataka kwenda Ikulu naye atafia huko, waniache nami nifie bungeni, mbona kuna wabunge wanafia humo?

  "Kama Chadema inavyogawa kura zangu Vunjo, vivyo hivyo nami nitahakikisha Mbowe, Mrema na Ndesamburo, hawanusi Bunge …nitafanya kampeni kubwa katika majimbo yao, kuhakikisha TLP inakuwa na wapiga kura wengi, ili kuzuia ushindi wanaotarajia Chadema, nitahakikisha hadi kinaeleweka," alisema Mrema.

  Amesisitiza kwamba, haendi kwa bahati mbaya katika majimbo hayo, bali nia ni kuwavurugia kama chama hicho kinavyomtibulia mipango yake ya kuingia bungeni, baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31.
  Alisema kutokana na kufanyiwa siasa chafu na Chadema, sasa chama chake kitahakikisha kinaelekeza nguvu Hai anakogombea Freeman Mbowe, Vunjo anakogombea John Mrema na Moshi Mjini anakowania Philemon Ndesamburo.

  Mrema alisema madhumuni ya kuelekeza nguvu katika majimbo hayo ni kutokana na alichokiita upinzani wa kinafiki unaofanywa na Chadema, ambapo alisema kauli ya Chadema kuwa Mrema atakwenda kufia bungeni ni matusi huku akisisitiza kwamba hakuna mtu asiyekufa katika dunia hii na akasisitiza kama ni kufa aachwe akafie huko kwa kuwa ana uchungu wa kutetea watu wa jimbo lake.

  Aliwaonya mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa, Mwenyekiti Mbowe na Ndesamburo kutokanyaga jimbo la Vunjo na kama wataamua kwenda waende kistaarabu.

  "Wakiendelea kunichezea rafu za kisiasa, nitatahakikisha kati yao hakuna anayeshinda katika uchaguzi mkuu, kwani nitafanya kampeni za nguvu kuhakikisha nagawa kura za Hai na Moshi Mjini," alisema Mrema.

  Aliongeza kuwa, anashangazwa na upinzani uliopo sasa miongoni mwa vyama vya upinzani kwani havijalenga kuchukua madaraka ya nchi hii kama baadhi ya viongozi wanavyowahubiria wananchi bali kushambuliana, jambo linalozidi kudhoofisha kambi ya wapinzani na kuiacha CCM ikitamba.

  Wananchi wa Jimbo la Vunjo wanamfahamu Mrema kama mwanasiasa mkongwe ambaye aliwahi kuwawakilisha vema wapiga kura wake na kutokana na uchapa kazi wake Rais wa awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassani Mwinyi aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi.

  Katika enzi zake za uwaziri, Mrema anakumbukwa na wananchi wengi kwa sera zake za kuwapa watuhumiwa mbalimbali siku saba au kuwaamuru kuripoti ofisini kwake.

  Alikuwa akijiita polisi namba moja na aliwahi kukamata dhahabu yenye thamani ya mamilioni ya shilingi ambayo ilikuwa ikisafirishwa nje ya nchi kwa magendo.

  Aidha, akiwa upinzani, aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi na aliliwakilisha vema ji.....................................................................,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, MREMA L,ANAUMWA SO 2MWACHEN2 HAJUI ALITENDALO JAMAN BUNGEN AKAFANYE NINI MGONJWA
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  :thinking: huyo Mrema anaitaji:help: anatia hurma
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Hii kauli ya MREMA inathibitisha ya kuwa yeye ni kada wa CCM na safari hii hatudanganyiki. Huku anampigia kampeni JK huku analaumu upinzani kwa kushambuliana. Hivi ni nani anashambulia wenzie kama siyo yeye?
   
 6. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,223
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Mwenzenu yuko kibiashara zaidi. anatafuta kazi ya kumpa kipato kwa miaka mitano ijayo. Hana kazi nyingine zaidi ya siasa. huyo ni Mchaga wa kwanza asiyejua biashara. Tumsameheni. Huyu jamaa nilikuwa namweshimu sana katika dira za siasa lakini naona siasa inamuacha vibaya. Mungu amsaidie
   
 7. g

  grandpa Senior Member

  #7
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 24, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo la Mrema ni kwamba anatafuta pesa akajitibu ule ugonjwa wake wa kubabuka ngozi
   
 8. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mrema usalama wa taifa uliacha kazi lini?
   
 9. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,477
  Likes Received: 1,214
  Trophy Points: 280
  duh bado kuna watu mnasoma uwazi udakuuuuuuuuuuuuu pengo umefulia
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kumbe ni habari toka global publisher!
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mrema hajawaelewa CDM.
  CDM walikuwa wanamaanisha uzee wa akili.
  Kumbe Mrema anamtambua Dr. Slaa kama rais.
   
Loading...