Mrema asema hajutii kumnadi Rais Magufuli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
MWENYEKITI wa Taifa wa chama cha siasa cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema amesema hakufanya makosa na wala hajutii kumnadi Rais John Magufuli kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa sababu alitambua Watanzania wamelamba dume la maendeleo.

Akizungumza na gazeti hili jana mjini Moshi, Mrema alisema Watanzania wamepata mtu wa kuendeleza kazi aliyokuwa akiifanya kipindi yeye wakati akiwa Naibu Waziri Mkuu katika miaka ya 1990, ya kupambana na wahujumu uchumi, wala rushwa na wafanyakazi wazembe.

Mrema alisema Dk Magufuli ndiye mwenye uwezo pekee wa kuyaleta mabadiliko ya kweli yanayohitajika, japo wengi waliamini hayawezi kupatikana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndio maana alichukua jukumu la kumpigia kampeni.

Mrema aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo mwaka 2010 hadi mwaka 2015, alisema anamfahamu vizuri Dk Magufuli tangu akiwa Waziri wa Ujenzi, kutokana na uchapakazi wake, ambapo walisaidiana kujenga barabara za Vunjo, hali iliyosaidia jimbo hilo kuwa na mtandao mkubwa wa barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami.

?Watu walishangaa sana kwa nini nilimpigia kampeni Dk Magufuli, na kumwacha mgombea wangu?nilijua mtu pekee wa kuyaleta mabadiliko makubwa na kweli ni yeye? Kwanza nampongeza sana na nafurahi sana kwa taifa hili linahitaji kiongozi mchapakazi, mwadilifu kama yeye,? alisema Mrema.

Katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu, akiwa jimboni Vunjo, Dk Magufuli alikutana na Mrema wakati huo naye akiomba kura za ubunge, na alimshika mkono na kumtambulisha akiwa katika moja ya mikutano yake, na Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alimpigia debe mgombea huyo wa urais wa CCM.

Mrema alifanya hivyo huku chama chake, TLP kikiwa kimemsimamisha MacMillian Lyimo kuwania urais wa Tanzania, hali iliyoibua mijadala wakati huo wa kampeni, huku mwanasiasa huyo machachari nchini akitetea msimamo wake huo wa kumnadi Dk Magufuli badala ya Lyimo.

Mrema alisema Uchaguzi Mkuu umeibua rais mwema, mwadilifu na mwenye uchungu na Watanzania wote. Aliwataka Watanzania kuacha ushabiki wa vyama vyao vya kisiasa na kuangalia mtu anayefanya kazi ya kulikomboa Taifa hili, kama Dk Magufuli kwa kumuunga mkono na kumuombea.

Alisema tangu Taifa lipate Uhuru, kwa sasa Tanzania imeandika historia ya kuwa na viongozi mahiri watatu wa kupambana na umaskini, ambapo aliwataja viongozi hao ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Sokoine (sasa hayati) na Dk Magufuli.

IMG-20151008-WA0011.jpg

CHANZO: Habarileo
 
Huwezi kuamini kama Mrema wa miaka ya 1990's angeweza kuwa kama huyu wa sasa ambaye kwa sasa anategemea hisani ya Rais Magufuli kikatiba kuwa Mbunge wa JMT.

Mrema wakati akiwa serikalini alikuwa anatoa dozi ya siku saba kwa wafanyakazi kutekeleza jambo analotaka lifanyike.

Ama kweli, a week is a long time in politics!

10-9-2008+3-29-49+PM_0137.jpg

Mrema enzi zake akiwa na Mwl. Nyerere.
 
Haya Magazeti Mengine Yaone Hata Aibu Kufanya Mahojiano Na Mrema.Si Ni Huyu Huyu Hata Mwaka 2010 Alimnadi Kikwete Wakati Chama Chake Kikiwa Kimemsimamisha Mtamwega Mgahiwa? Je,alishajuta Kutuletea Kimeo Kama JK? Na Huu Wa Leo Ni Usanii Kama Usanii Mwingine Ili Apoze Tumbo Lake Tu.
 
Mrema kwa sasa anahitaji huruma ya Magufuli ktkt vile viti kumi.
 
hata zzk ndiko anakoelekea cjui hasomi nyakati au ajifunze kutoka kwa Mrema na Cheyo..
 
MWENYEKITI wa Taifa wa chama cha siasa cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema amesema hakufanya makosa na wala hajutii kumnadi Rais John Magufuli kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa sababu alitambua Watanzania wamelamba dume la maendeleo.

Akizungumza na gazeti hili jana mjini Moshi, Mrema alisema Watanzania wamepata mtu wa kuendeleza kazi aliyokuwa akiifanya kipindi yeye wakati akiwa Naibu Waziri Mkuu katika miaka ya 1990, ya kupambana na wahujumu uchumi, wala rushwa na wafanyakazi wazembe.

Mrema alisema Dk Magufuli ndiye mwenye uwezo pekee wa kuyaleta mabadiliko ya kweli yanayohitajika, japo wengi waliamini hayawezi kupatikana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndio maana alichukua jukumu la kumpigia kampeni.

Mrema aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo mwaka 2010 hadi mwaka 2015, alisema anamfahamu vizuri Dk Magufuli tangu akiwa Waziri wa Ujenzi, kutokana na uchapakazi wake, ambapo walisaidiana kujenga barabara za Vunjo, hali iliyosaidia jimbo hilo kuwa na mtandao mkubwa wa barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami.

"Watu walishangaa sana kwa nini nilimpigia kampeni Dk Magufuli, na kumwacha mgombea wangu?nilijua mtu pekee wa kuyaleta mabadiliko makubwa na kweli ni yeye" Kwanza nampongeza sana na nafurahi sana kwa taifa hili linahitaji kiongozi mchapakazi, mwadilifu kama yeye," alisema Mrema.

Katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu, akiwa jimboni Vunjo, Dk Magufuli alikutana na Mrema wakati huo naye akiomba kura za ubunge, na alimshika mkono na kumtambulisha akiwa katika moja ya mikutano yake, na Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alimpigia debe mgombea huyo wa urais wa CCM.

Mrema alifanya hivyo huku chama chake, TLP kikiwa kimemsimamisha MacMillian Lyimo kuwania urais wa Tanzania, hali iliyoibua mijadala wakati huo wa kampeni, huku mwanasiasa huyo machachari nchini akitetea msimamo wake huo wa kumnadi Dk Magufuli badala ya Lyimo.

Mrema aliseAma Uchaguzi Mkuu umeibua rais mwema, mwadilifu na mwenye uchungu na Watanzania wote. Aliwataka Watanzania kuacha ushabiki wa vyama vyao vya kisiasa na kuangalia mtu anayefanya kazi ya kulikomboa Taifa hili, kama Dk Magufuli kwa kumuunga mkono na kumuombea.

Alisema tangu Taifa lipate Uhuru, kwa sasa Tanzania imeandika historia ya kuwa na viongozi mahiri watatu wa kupambana na umaskini, ambapo aliwataja viongozi hao ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Sokoine (sasa hayati) na Dk Magufuli.

CHANZO:Habari Leo
 
Angalau lakini amajitambua hakujiweka kwenye list ya viongozi waadilifu na wazalendo maana amewataja Jk Nyerere, Sokoine na JPM
 
Mrema anatafuta relevance. Anataka asikike na aonekane ili JPM amkumbuke. Namshauri atafute shughuli nyingine afanye maana JPM hawezi kumpa kitu. JPM si JK!
 
Haya Magazeti Mengine Yaone Hata Aibu Kufanya Mahojiano Na Mrema.Si Ni Huyu Huyu Hata Mwaka 2010 Alimnadi Kikwete Wakati Chama Chake Kikiwa Kimemsimamisha Mtamwega Mgahiwa? Je,alishajuta Kutuletea Kimeo Kama JK? Na Huu Wa Leo Ni Usanii Kama Usanii Mwingine Ili Apoze Tumbo Lake Tu.

ulitaka AMNADI MGONJWA wenu nini?
 
Kwa uhaba wa watu waadilifu iliyonayo CCM Mrema asitarajie huruma kwani hata Magufuli mwenyewe anatamani hivyo viti vya ubunge vya kuteuliwa na Rais viongezwe apate watu waadilifu nje ya mfumo wa CCM ili wawe mawaziri katika baraza lake.
 
huyu naye ameshaanza kuja na lugha za mzee wa kubadilishia Gear Angani? unaufahamu mfumo wewe? Magufuli ni CCM ...Refer hotuba na mahojiano mbali mbali ya Viongozi wa CCM..... kuwa CCM ina watu wengi sana! Kuna wasafi na wasiokuwa na MAKANDO KANDO..... na kuna wenye MAKANDO KANDO..... Ni sisi wenyewe kuamua.... je nyinyi CHADOMO ....mna options gani..... kila utakayemgusa.... kama sio KAPI lenye makando kando basi ni Mstaafu wa uozo fulani...
 
putin v acheni ujuha wenu, Magufuli ni Rais wa Tanzania au ni Rais wa chama chenu cha Mapinduzi? Hamjui nchi inaendeshwa kwa kodi za wananchi na wala si kwa ada za kadi za chama chenu!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Allen Kilewella! Kumbe mlishakubali kuwa MAGUFULI NI RAIS halali wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Changamoto kubwa ni kuwa hatuwaelewi mnataka nini? Mara mnasema Raisi wenu ni JIWE...au yule Jamaa aliyetengeneza MAFURIKO halafu yakambeba mwenyewe....!
 
Back
Top Bottom