Mrejesho wa hospital ya kujifungua

Big Dy

JF-Expert Member
Dec 23, 2015
399
500
Hospitali gani ya private ni nzuri kwa kujifungulia na gharama zake zikoje - JamiiForums
Habari za mihangaiko wadau, leo nimeamua kuleta mrejesho wa kile nilikua nimeuliza wapi pazuri kwa mama mjamzito kujifungua.
As I said nilikua nafanya klinik Muhimbili hospital na nikaamua kumalizia ng'we huko huku kama nilivyoshauriwa na wengi na haya niliyoyakuta.
1. Public hospital ni nzuri sana ila baadhi ya watendaji wake (wauuguzi) wake wanafanya hizi hospital zidharaulike sana, kuna staff yaan wanafanya kazi zao ili mradi tu mda uende na sio kuwa ni wajibu wao kufanya kazi katika taasisi hii. Kuanzia daktar ambaye alikua ananihudumia tangu kipindi cha klinik yeye akishajua tu umekua admitted hapo anajua kabisa ni lazima apate mpunga wake na wala si kukusaidia kukamilisha safar yako. Daktar anakuja kuchungulia tu na kazi zote zina fanywa na wakunga.
2. It is who are you and who do you know: Hakika huduma zake ni zina base zaidi kwa ni nani unamjua ndo unapata urahisi wa kupata huduma. Hii ni kuanzia kwa walinzi mpka waauguz wenyewe ukiwa ni mtu wa chini na hauna mtu unapigishwa mark time pale nenda rudi mpka ukate tamaa.
3. Ukatili. Hapa ni pa Pana sana ebwana kule labor pamoja ya kuwa wako strictly sana ila bwana wale wanawake wa mule ndani ni wa katili sana sijui ni binadam wa wapi. Kuingia na kutoka salama kwako kule ni kudra za Mungu tu, mtu ukibanwa na uchungu au shida yoyote itokanayo na uchungu msaada wao ni hafifu sana. Unaweza ukajichafua hapo na wao wanakutazama tu. Kuna roho nyingi sana zinapotea humu ndani kwa uzembe wa wakunga wetu hawa. Mungu awasamehe kwa kweli

Itaendelea.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,242
2,000
Huku Jamii Forums hasa MMUni kwa kuwa makini sana. Imagine ID na Avatar ya mtoa mada!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom