Mrejesho wa demo: Kilimo cha pilipili

Entreprenuare

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
1,616
1,714
Wakuu!

Mimi napenda sana sekta ya kilimo na ufugaji, sasa nilifanya Demo ya kilimo cha pilipili, kwa miche 3 tu. Leo nimevuna .

Naona pili pili zimetoka vizuri sana, nimeona kumbe naweza kufanya kilimo cha pili pili.

Location, ni DSM

Sasa, ni wakati wa kuingia shambani, kufanya seriously horticulture

IMG_1325.jpg

Hiyo ndio product niliyo pata, baada ya demonstration.
 
Hongera sana mkuu. Binafsi nina ndoto kubwa ya kulima pilipili kwa ufanisi wa hali ya juu, nilishawahi kujaribu kupanda demo bahati mbaya zilidumaa lakini nilivuna. Asante sana kwa kunitia moyo, nami nakutakia kila la heri katika kilimo cha pilipili.
 
Wewe upo wapi? Kama upo seriously, tunaweza kuunganisha nguvu.

Mm nipo dsm, nampango wa kwenda kulima kwenye mashamba ya mto ruvu.
 
Ukiweza kulima pilipili alafi ukatengeneza zile chachandu fresh kwenye makopo ukauzaa its much better. Sema hata kuuza moja hamsini sio mbayaa
 
Wow! zinapendeza hongera, vipi zinachukua muda gani hadi kuvuna?, kwenye hiyo demo umekutana na changamoto gani hasa?, zinazaliana ipasavyo? Ukivuna mara moja ndiyo basi ama unaendelea kuvuna kama zile nyanya chungu?

Naziomba hizo
 
Haha kwanza leo nimetumia kidogo, aisee zinanukia vizuri sana .
 
Wow! zinapendeza hongera, vipi zinachukua muda gani hadi kuvuna?, kwenye hiyo demo umekutana na changamoto gani hasa?, zinazaliana ipasavyo? Ukivuna mara moja ndiyo basi ama unaendelea kuvuna kama zile nyanya chungu?

Naziomba hizo

Zimechukua miezi 3 na zaidi kidogo

Hizi una chuma tu, mfululizo.

Changamoto sijaona kusema kweli. Ila ngoja niingie kwenye kilimo kikubwa tuone,
 
Kazi nzuri karibu shambani, mie ni mkulima wa pilipili huu ni mwaka wa tatu Sasa Niko mkoa bt ukiwa na tatizo kuhusu pilipili usisite kunitafuta , nakutakia mafanikuo mema.

Asante sana mkuu, my contact 0654171555,
 
Zimechukua miezi 3 na zaidi kidogo

Hizi una chuma tu, mfululizo.

Changamoto sijaona kusema kweli. Ila ngoja niingie kwenye kilimo kikubwa tuone,
Unapo sema mfululizo una manisha nini? . Mimi nalima matikiti kigamboni huko, naweza kujaribu na hiyo kitu.

Zinakua tayari kuchumwa baada ya muda gani?
 
Kitu kizuri ni kua umefanya demo kwanza, maana mambo ya kilimo ukiingia kichwa kichwa inakula kwako mazimaaa.

Kimsingi nimetokea kuamini katika kilimo hasa hiki cha mazao ya kumwagilia na ya muda mfupi.
 
Hongera sana.
Ila ningekushauri pia shambani anza na robo heka. Ukivuna msimu wa kwanza then panda nyingine wakati unaguna mchumo wa pili robo au nusu heka

Hapo ni sawa umepata uzoefu wa kufuga kuku wa kienyeji wawili ( toka vifaranga mpaka wametaga na kutotoa vifaranga) ukasema sasa unataka kwenda shamba kufuga kuku wa kienyeji mia moja kwa mkupuo

Utapata matokeo ya kura za maoni, kigamboni.
 
Kitu kizuri ni kua umefanya demo kwanza, maana mambo ya kilimo ukiingia kichwa kichwa inakula kwako mazimaaa.

Kimsingi nimetokea kuamini katika kilimo hasa hiki cha mazao ya kumwagilia na ya muda mfupi.

Itabid tuanze na mazao yenye low risk, pia na mpango wa kufanya demo ya nyanya chungu
 
Back
Top Bottom