mkuu pole sana,hiyo situation ni ngumu sana aisee,huyo dada ni mkatili aisee(ingawa si sahihi sana kumhukumu sababu ana haki ya kuwa na mtu anaempend), ninachoona wakati mnaanza uhusiano wenu alikua hajamsahau mtu wake , pengine wewe alikutumia kujipumzisha baada ya kuacha na huyo mtu wake wa awali na siku zote alikua anasubiria kurudia kwa penzi hilo, hili ndili ambalo naweza kusema, ni mara chache sana wapenzi waliachana katika mazingira ya huyo dada wakurudiana na kudumu,achana nae kabisa hadi may 2016, watakua wameshaachana na huyo mtu wake anaemuita wa "future" akija usimpe nafasi muache akafunzwe na walimwengu.
Mweleze wazi kwamba haupo tayari kua mchepuko, mtakie heri huko aendako na uwe na moyo wa uvumilivu huku ukijitahidi kuchukulia changamoto hiyo kama daraja lako la kumpata mzuri zaidi ya huyo. Usisahau kumtanguliza Mungu katika hilo
Wakati nasoma uzi huu nlikumbuka Pastor HIZZA wa CCT udsm huwa anapenda kusema hivi
"Binti/kijana ukikataaa akakwambia sikupend, tuachane. Unachotakiwa kufanya ni kupangusa mikono na kumshukuru Mungu kwani hujui kakuepusha na nini! Siku ya ibada ikifika nenda toa sadaka, sema asante mungu"
Then endelea na maisha, hakuna sababu ya kulaumu wala kusononeka.
Mweleze wazi kwamba haupo tayari kua mchepuko, mtakie heri huko aendako na uwe na moyo wa uvumilivu huku ukijitahidi kuchukulia changamoto hiyo kama daraja lako la kumpata mzuri zaidi ya huyo. Usisahau kumtanguliza Mungu katika hilo
Duuuhh, pole sana. Hakuna maumivu makali kama ya mapenzi.
Watu ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya au pombe wanapoamua kuacha hushauriwa kuacha taratibu. Kubali kuwa mchepuko wake huku ukiiandaa akili yako kuachana kabisa.
Pole Mkuu Najua maumivu yake yalivyo!! Bila Shaka huyo hajafikisha hata 24 yrs... Ni mtoto, mtu mzima hawezi kufanyaa upuuzi Kama huyo... Sasa cha kufanya wewe mpotezee mazima... Usimtafute wala nini, ikiwezekana mblock kila mahali halafu futa namba zake, let her go... Ila nakuhakikishia lazima tu wataachana muda si mrefu, na atakutafuta... Hana msimamo huyo mtoto... Wanawake wako wengi sana ndg yangu hawaiishi. Jitahidi uepuke distance relationship kadiri iwezekanavyo. Huyo mdada amekudanganya, ukweli ni kwamba huyo mwanaume Alitoka nAe hapo hapo chuo wakaja Huku dar. Probably ni mwanafunzi mwenzie.
Merry chrissmass