mwayungi
JF-Expert Member
- May 9, 2017
- 1,814
- 3,079
Wadau salamu kwenu,rejea kichwa cha habari hapo juu nilileta mada husika humu jamvini juu ya tabia ya mke wa kaka.Nashukuru kwa wote mliochangia kunishauri,na kunikosoa pia.Ushauri nimeufanyia kazi na nikamuomba kaka anipangie chumba ili nikasimamie biashara zake siwezi kuishi kwake na hilo limewezekana.Shemeji aliniuliza kwanini nimekataa kwenda kuishi nao nikwamueleza kuwa nimeamua kujaribu kujitegemea na alinambia lengo lake lipo pale pale nami nikamuambia kuwa msimamo wangu ni ule ule.Asanteni sana wakuu kwa ushauri mlionipa mubarikiwe