Mrejesho: Nimetembea na wanawake 50, kati yao asilimia 60 wake za watu!

MarchArmy

Senior Member
Aug 19, 2016
160
104
Habari za wakati wakubwa....

Yakiwa yamebakia masaa machache na dakika kabla hatujaingia mwaka 2017, naomba nilete mbele yenu mrejesho kuhusiana na maoni/ushauri mlionipatia kupitia thread yangu hii - Mwaka unaisha, nimetembea na wanawake 50, asilimia 60% wake za watu. niliyoianzisha hapa siku ya jana.



Nashukuru kwa kila mdau aliyetumia muda wake kusema chochote kupitia ule uzi niliouanzisha!

Naomba niseme nimeyaheshimu mawazo ya kila mdau na nimejikana nafsi kutojihusisha tena kimahusiano na wake za watu. Nimeamua kuanzisha mahusiano mapya na asiyekuwa mke wa mtu baada ya kujiridhisha kweli siyo mke wa mtu.


Nimeamua kufanya hivyo ili niweze kujijenga kimaisha kwani hakika nimeshapoteza muda mwingi katika mahusiano ambayo hayangeweza kunipeleka katika mafanikio.


Naomba tuzidi kuombeana kwani bila maombi yenu siwezi japo nipo na nia ya kubadili msimamo wangu wa awali.


Najua nitakutana na changamoto nyingi katika maamuzi niliyoyachukua lakini nina hakika mbeleni kuna NURU.


Nisiseme sana, nawatakieni usiku wa amani tukauanze tena mwaka mpya wa 2017 katika mafanikio makubwa, naamini utakuwa mwaka wangu mkuu wa mafanikio.


Naahidi kutorudi nyuma kamwe!
 
Na yawe maamuzi kweli maana ushalamba sukari sasa kuacha lazma isumbue kidogo
 
Ukikubali kutubu na kukusudia kuacha dhambi na kuweka jitihada za kulitimiza hilo, litakuwa jambo la busara sana!!!!
 
Na umaanishe! ...once a sinner always a sinner...prove huo msemo wrong!

goodluck
 
Back
Top Bottom