Mrejesho;nimerudi kazini sijamkuta mke wangu kuuliza majirani naambiwa ameondoka kwenda kwao

Dezoizo52

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
524
1,052
Wanajamii forum nilikuja kwenu kuomba ushauri kwa kweli nawashukuru sana.Mlio wengi mlinipa ushauri kadri mlivyolichukulia kutokana na uzito wake. Tuliweza kufatilia mawasiliano ya mke wangu ya simu na tulikuta ni wifi yake alikuwa anamshawishi aondoke arudi kwao. Kimsingi mke wangu ni yatima amelelewa na kaka yake ambaye mkewe ndiyo alimshawishi aondoke. Baada ya kupata mawasiliano utaratibu wa kipolisi ulifanyika ilibidi akamatwe wifi yake hivyo akamwambia mke wangu aripoti polisi na polisi walipiga simu lindi kuwa mke wangu kaonekana. Kaka wa mke wangu amenipigia simu na kunieleza kuwa yeye hajui kinachoendelea.Kwa haya machache niliyoyapata kuhusiana na mke wangu kwa moyo mkunjufu na bila kinyongo nmeamua kumuacha aende.
-Ameripoti polisi leo baada ya kuona anatafutwa lakini ameongea kuwa tuligombana na huwa ninampiga mara kwa mara akaamua aende kwao.
-Ameona kwao ndiyo sehemu salama lakini hakunifahamisha wapi alipo.
Kutokana na haya machache nmejiridhisha kuwa hii ndoa ni beyond repair kwa sababu ya maneno ya uzushi na uongo. Sikatai nasema yapo madhaifu kwangu ila ndoa inachangamoto na kabla ya hapo kuna washenga na ndugu kama walikuwa wanahitaji kurekebisha ingeweza kufanyika hivyo.
 
Pole sana ila hakikisha unasimama juu ya msimamo wako mana Siku yaja atarudi,hivyo jipange.
 
Back
Top Bottom