“Sitaki uhangaike mume wangu, umehangaika vyakutosha” mke wangu

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,212
4,517
Nawasalimu waungwana!

Leo mke wangu kwa kweli amenikosha sana. Nilikuwa kwenye kikao mahali, mbali kidogo na nyumbani, ile namaliza kikao naona mke wangu ananipigia.

Kama kawaida simu zake napokea kwa mikwara ya utani. Akaniuliza ntakula nini kati ya wali na ugali maana amepika wali na anafahamu mimi napenda ugali. Nikachagua ugali. Akataka kujua nitafika nyumbani baada ya muda gani maana alitaka kutoka na watoto. Kwa kuwa nilikuwa mbali kidogo, nikamwambia itachukua kama saa moja hivi mpaka kufika home hivyo nikamwambia yeye aende tu nitasonga ugali nikifika nyumbani.

Mke wangu akakataa na kunifahamisha kwamba atanisubiri nikifika anisongee ugali ndo aondoke.

Basi kapuku mimi nikapanda zangu train, nikaunganisha basi la kuelekea nyumbani niliposhuka kwenye train maana kwa wazungu huku usafiri wa umma uko vizuri.

Ndani ya kama saa moja hivi nikawa nimefika, kuingia ndani nasikia anakivuruga huko jikona. Dakika chache, ugali kwa nyama hiyo mezani.

Sasa baada ya yeye kuniwekea chakula akawa najiandaa kuondoka na watoto, nikamwambia angeenda tu mapema mimi ningesonga ugali maana mboga alishapika.

Akaniambia “sitaki uhangaike mume wangu, umehangaika vyakutosha”. Basi moyoni nimefirahi hatari hapa nawaza nimfanyie nini mke wangu maana kwa kweli sina cha kulalamika. Mke wangu anasimamia show zote kwa uweledi mkubwa sana na sina shida kabisa, watoto wangu naamini wapo kwenye mikono salama siku zote. Ananiheshimu na kunistiri madhaifu yangu, naye namsitiri.

Haimaanishi hatuna matatizo kwenye nyumba yetu, lah hasha! Sema tumeamua kama watu wazima kubebana na kutafuta amani kwa majadiliano na maridhiano katika familia yetu.

Kesho ni birthday yake hapa nafikiria kumtoa out hiyo kesho ajichetue hasa.


Majinga mnayoendeleza upuuzi wa eti kataa ndoa endeleeni tu huko. Mkifika uzeeni mtakula jeuri yenu.

Mwanaume ni majukumu maboya wasiotaka kufanya kazi na kuwa na majukumu ya kifamilia ndo wanajaza saver za JF na upuuzi wao eti “Kataa Ndoa!


Sisi wenye kusimamia majukumu yetu kwa kutambua kwamb hakuna jamii bila familia tunaendelea na majukumu yetu kama kawa.
 
Akaniambia “sitaki uhangaike mume wangu, umehangaika vyakutosha”. Basi moyoni nimefirahi hatari hapa nawaza nimfanyie nini mke wangu maana kwa kweli sina cha kulalamika. Mke wangu anasimamia show zote kwa uweledi mkubwa sana na sina shida kabisa, watoto wangu naamini wapo kwenye mikono salama siku zote. Ananiheshimu na kunistiri madhaifu yangu, naye namsitiri.
Ilibidi uipige kwanza kabla hajatoka na watoto, na kesho unaipiga Tena mkitoka out😀
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom