Mrejesho kutoka TRA baada ya kuninyima kibali cha biashara sababu ya madeni ya gari nililouza

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Mwaka jana nilileta Uzi juu ya TRA kugoma kutoa vibali kwa wafanyabiasha biashara (Tax clearance certificate) mpaka ulipe madeni ya Road Licence. madeni hayo ni yale ambayo watu tuliuza magari bila kufanya transfer/kuuza kama scraper/kuuza kama spea.
Hawajaondoa kodi wala kufuta madeni lakini wanakubali mfanye makubaliano namna ya kuyalipa kwa instalment/awamu na kibali unapewa kabla ya kumaliza deni lote.
Hicho ndio kilio nilichokileta humu wakati ule kuwa madeni hayakupaswa kuwepo na waruhusu biashara mpya zifunguliwe bila mizengwe ya kunyima wafanyabiashara VIBALI Mpaka madeni yalipwe.

Kwa wale wachangiaji wenye mitizamo hasi waelewe kuwa tukileta kero humu zinafanyiwa kazi.wasiwe wanabomoa hoja za watu bila hoja za nguvu.

Baniani Mbaya lakini upatu wake apewe.
 
hao ndio TRA, awali hatukuwa na taarifa hizo tumeuza vigari vyetu baada ya kuwa NGORO kwa muda mrefu sasa TRA wanataka tulipe kodi ya vigari tulivyouza spea 1999! hii haikuji! mtakaa na videni hivyo (bad debs) hadi wenyewe mtafuta. sasa gari miaka 10 haipo barabarani nyie mnataka mlipwe! EBO!
 
mkuu hawana bad debt wala ku write off wanasoma uhasibu wa kuungaunga.mimi gari lina miaka 20 saloon car wanataka kodi.nililikata miaka nane iliyopita.
 
  • Thanks
Reactions: J33
hao ndio TRA, awali hatukuwa na taarifa hizo tumeuza vigari vyetu baada ya kuwa NGORO kwa muda mrefu sasa TRA wanataka tulipe kodi ya vigari tulivyouza spea 1999! hii haikuji! mtakaa na videni hivyo (bad debs) hadi wenyewe mtafuta. sasa gari miaka 10 haipo barabarani nyie mnataka mlipwe! EBO!
Usiwe na fikra fupi,wao wangejuaje kama halipo barabarani?ulivyouza kwanini hukufanya transfer?au lilipokua skrepa kwanini hukuwataarifu?miTanzania ndivyo tulivyo,unataka waote
 
.. inawezekana vipi gari itembee barabarani kwa miaka 10 au 20 bila kulipiwa road license. Na wakati unapewa kadi ya gari TRA huwa hawatoi maelezo yoyote kuwa ukiuza gari au scraper uwape taarifa. Inaonyesha TRA walilala usingizi mzito, hawakuwa na utaratibu mzuri wa kufuatilia malipo, sasa wamekurupuka usingizini wanawabebesha wateja wao mzigo uliotokana na uzembe wao.
 
Mkuu TRA walikuwa sahihi kukunyima tax clearance! Kwasababu Hilo jina lenyewe linamaanisha hudaiwi kodi yoyote!!
Nakushauri ingia nao hayo makubaliano ya kulipa kwa installments ili maisha yaendelee!!
 
.. inawezekana vipi gari itembee barabarani kwa miaka 10 au 20 bila kulipiwa road license. Na wakati unapewa kadi ya gari TRA huwa hawatoi maelezo yoyote kuwa ukiuza gari au scraper uwape taarifa. Inaonyesha TRA walilala usingizi mzito, hawakuwa na utaratibu mzuri wa kufuatilia malipo, sasa wamekurupuka usingizini wanawabebesha wateja wao mzigo uliotokana na uzembe wao.
mkuu hata wao TRA/TRAFFIC POLICE ni victim.wote tulilala usingizi mzito
 
Usiwe na fikra fupi,wao wangejuaje kama halipo barabarani?ulivyouza kwanini hukufanya transfer?au lilipokua skrepa kwanini hukuwataarifu?miTanzania ndivyo tulivyo,unataka waote
Bora hata uwapashe ndg manake wa tz wengi wanaishi kwa mazoea wakati taratibu ziko wazi tu.
 
Ebhana wabongo ni watu wa ajabu sana... sasa unadaiwa mean kwamba ulipaswa kulipa au kufwata taratibu na sheria za kubadilsha umilki.. ambayo inasema ndani ya siku 30 tokea umeuza chombo cha moto uwe umeshabadilisha umilki sasa ulitaka usamehewe? Lipa malimnikizo ya kodi bhana... wote tuchangie taufa na sio ujanjaujanja...
 
Back
Top Bottom