Mrejesho: Kuagiza rice combine harvester toka China

ipyax

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
4,147
6,521
Mnamo mwezi wa kwanza mwaka huu nilianzisha mada hapa jukwaani nikiomba ushauri wa kuagiza mashine toka China. Ishu ilikua niende China au niagize kwa mtandao kupitia Alibaba.

Nilipata ushauri wa kutosha tu huku wengine wakiniasa kwamba Alibaba nita tapeliwa hela bora tu niende China. Bahati mbaya budget yangu ilikua ndogo kwahiyo nisingeweza weza kwenda China basi nikaamua kuagiza kupitia Alibaba.

Namshukuru mungu mashine yangu ilifika salama kama wiki 2 zilizo pita na sasa nipo shamba napiga kazi. Napenda kutoa ushauri tu kwamba Alibaba wapo vizuri sana katika buyer's protection kwa hiyo risk ya kutapeliwa ni ndogo sana na kama una maswali usisite kuuliza.

1462808898681.jpg


1462808914366.jpg


1462808926342.jpg
 
Mkuu nataka niagize kubwa kabisa kwa ajili ya kuikodisha..
Return yake ikoje?
Usiagize kubwa itakutesa Kwa sababu huku mbeya ardhi ni tope sana Kwa hiyo mashine ikiwa nzito utakua una kwama mashambani kila siku na pia isiwe ya matairi. Ukiagiza yenye tank nayo haina mshiko sana Kwa sababu inapoteza muda kwenda kumwaga mpunga tank likijaa wakati hizi za vipeto hazisimami.

Kuhusu return mpaka msimu wa mavuno uishe ndiyo nitakua na jibu la uhakika kwa sasa naweza sema uongo. Ila karibu kulima mpunga aisee kama una mtaji kwasababu ni zao ambalo linalipa sana bila stress nyingi. Sijawahi kulima mpunga ila kwa hali ninayo iona huku naona kama nimechelewa sana japo nimekua inspired pia.
 
Hongera sana mkuu!
Kweli ukithubutu unaweza!!
Ko nikija na 5million naweza kukodi na kulima shamba kiasi gani hela yangu ini accomodate mpaka mavuno?
Kweli kilimo cha mpunga hakika stress sana hasa huko kwenye facilitilies za umwagiliaji. Na uzuri zao lenyewe linahifadhika.
 
Back
Top Bottom