Mrejesho: Kilichonipata Malta ni zaidi ya Ukraine, siku 18 za kufa na kupona

Route ya mwana baada ya kupakizwa kwenye mtumbwi. Inasikitisha sana. Ila sema nini, mwana alipiga kama vitatu vinne hivi, sio mbaya.
Screenshot_20220707-221231_Maps.jpg
 
Kama uzi wangu niliyowahi kuutoa kuhusu kukutana na mrembo wa Malta

Niliondoka tarehe 12 February na Qatar air na kufika tarehe 13 Malta airport na baada ya taratibu zote za uhamiaji

Nilifanikiwa kukutana na mwenyeji wangu,akiwa ameambatana na mabinti wawili na Kijana wa kiume mmoja

Waliponipokea walinipeleka resting point moja karibu na airport na kuagiza vinywaji fulani hivi,sikupata ladha ya kile kinywaji, nikakataa na kuagiza soda

Wakiwa wanaongea kiingereza kidogo wakichanganya kilugha fulani, nilihisi kama kijana wa kiume hakufurahishwa mimi kufika kuonana na binti huyo, wengine wa kike wenyewe walikuwa wanafurahi kuona shemeji yao

Binti Sarah ambaye ndiye mwenyeji wangu alinikaribisha vizuri na niwe na amani na akaniambia wanaishi Saint Julian's hivyo, tukanyenyuka tupanda basi ya kuelekea huko

Baada ya kufika huko licha ya kufika huko na kukaa na binti Sarah hotelini huko Julian's,makubwa yalipata baada ya siku tatu, makubwa mnooo

Nahitaji daktari wa saikolojia anitibu ndo nije kuendelea na simulizi,nikipona nitakuja kuendelea ,kwa sasa sipo vizuri ...........

Wakati tupo na wenyeji wangu tukitokea airport kuelekea Julian's ,tukiwa ndani ya minibus ,kwenye siti yangu nilikaa na Sarah ,mimi nikawa nimekaa upande wa dirisha ,Sarah upande wa kulia kwangu na siti ya nyuma yetu alikaa Angel na Ann ,yule Kijana aitwaye Jack yeye alikaa sit ya upande wa kulia sambamba na sisi

Wakawa wanaongea kilugha na kiingereza kidogo wananielezea nilivyo ,huku mimi nikiwa kimya nawasikilizia ,nilihisi Jack alikuwa kama ananitukana kwa kilugha,maana alivyokuwa ananiongea ,Sarah na Ann walikuwa kama wanamkaripia muda huo jack ananiangalia kwa dharau

Kama dakika chache hivi Jack alishuka baada ya kurushiana maneno ya ukali na Sarah hivyo akakasirika na kushuka kituo ambacho hakikuwa kimekusudiwa

Baada ya dakika chache Sara akiwa na sim yake mkononi SMS iliingia na mimi jicho likaenda moja kwa moja kwa sms inasomeka hivi "Enjoy with your monkey,and I should do something to it"

"Furahia na nyani wako ,nitamfanyia jambo "

Hata hivyo Sarah hakutaka kunionesha ile sms ,ingawa nilikuwa nimeiona

Baada ya kufika George street tukashuka na kutembea kwa mguu kuelekea mitaa nisiyoijua lakini kichwani nawaza kama huku nilipo kuna usalama,kweli nitarudi kwetu Tz salama au nimekuja kufa

Tukiwa tunatembea mdogo mdogo na mawazo kibao Sarah alishika mkono wa kushoto na ghafla Ann akanishika mkono wa kulia ,Angel akawa amebeba kabegi kangu

Sarah na Ann walinisihi sana nisiwe na mawazo na wakaniomba niwe nafuraha na wakaniomba msamaha kwa kuambatana na Jack mwenye chuki na mbaguzi

Hata hivyo wakaniomba tupite mtaa fulani wanitambulishe kwa waafrika wanaofanya biashara mitaa fulani ili niwe na amani na ikiwezekana nifahamiane nao

Nikawakubalia kupita hiyo mitaa,tukafika mtaa mmoja uliochangamka kidogo tukaingia kwenye duka moja ,wakanitambulisha kuwa mimi ni rafiki yao nimetokea Afrika ,yule muuza duka akajitambulisha kwangu kuwa anaitwa Laurent ametokea Liberia anaishi Malta kwa zaidi ya miaka 7 ,akanambia karibu sana Malta

Basi nami nikajitambulisha kwake nikamwambia nimetokea Tz bahati mbaya akasema hajawahi kuisikia ila nikamuuliza kama amewahi kuisikia Kenya akasema amewahi ,nikamwambia ni jirani

Baadae mabinti wakasema muda umeenda maana ilikuwa inaelekea saa 4 usiku ,wakasema tuondoke tutafahamiana kesho zaidi

Baadae wakasema tupite mtaa mwingne uliye na mwafrika,tukapita yeye ni mmliki wa cafe halafu ni mwanamke ,tukapita tukaingia ndani ya cafe ,walikuwa wanafahamiana na mabinti hao "wakaanza kumwambia ndugu yako huyu hapa ametokea Afrika msalimiane na mfahamiane

Hiyo cafe ilikuwa vijana wa kiume wa kiafrika na na huyo mama mwenye umri kama 45 hivi ,huyo mama alinikaribisha vizuri

Muda huo Sarah akawa amemuomba aniletee chakula cha kiafrika ambacho naweza kula ,yule mama akaleta wali nyama,Angel,Ann na Sarah wakaomba chakula chao cha kimalta wakawa wanakula

Yule mama na yeye akaleta kiti akakaa pembeni yetu na kinywaji akaanza kuniuliza

Nitatumia lugha ya kiswahili kwenye Quotes ili kurahisisha mawasiliano ila alitumia kiingereza

Mama akajitambulisha " Naitwa Mary kule Afrika natokea Lagos Nigeria wewe je ? Nikamwambia "Naitwa Cosovo" si jina nililotaja " Natokea Dar es salam Tanzania " akasema "Akasema karibu sana Malta karibu sana ulaya ,karibu sana Julian's ,akaendelea kusema" Hawa mabinti ni marafiki zangu sana wanasoma hapo chuo kipo nyuma hapo ni marafiki na pia ni wateja wangu ,vipi na wewe umekuja kusoma chuo "? Kabla ya kujibu " Ann akasema "Yah ni kweli amekuja huku kusoma ila chuo Rabat "

Baada ya maongezi marefu kidogo Sarah alilipa na bili ya chakula na kuagana na Mary na kwenda mitaa mingine ili tukapumzike

Tulitembea kwa mguu kama dakika 10 hivi kwa mwendo wa kawaida tukaingia hotel moja imeandika Pope Hotel ,Sarah alikuwa amefanya booking online ,tukaingia ndani vyumbani,

Kwanza tuliingia chumba kimoja nikawaza huenda tutalala wote chumba kimoja ,kumbe baada ya kufika chumbani ,Sarah akawambia marafiki zake "Leo ni siku muhimu kwenye maisha yangu,nimepata rafiki wa kiafrika,natamka mbele yenu kwamba huyu ni boyfriend wangu kuanzia sasa na akipenda kunipeleka Tanzania mi nipo tayari kabisa,nimeumizwa na Thomas kutoka ufilipino ambaye tunasoma naye ,sasa staki mambo yake

Naomba kumuuliza baby wangu kama upo tayari tupime HIV test mbele ya marafiki zangu ," Nikasema haina shida " Akatoa vipimo viwili kutoka kwenye pochi yake tukapima tukasubiri majibu tukitazama vile vipimo wote wanne tukitazama majibu

Baada ya muda kidogo,vipimo vikasoma negative ambapo Sarah na wenzake walifuhi hatari ,kisha tukaagana ,Angel na Ann wakaenda kulala chumba kingine

Mtoto wa kizungu ambacho amebarikiwa ni kutokuwa na aibu akaanza kuvua na kubaki na kyu..p akanambia nisimame nivue tukaoge wote ,nikaanza kuvua lakini jicho lake lipo direct proportional to magogoni

Basi nikavua zote na jamaa akawa ameanza kuwika kwa mbali Sarah akanikaribia akaanza kuitomasa....kilichofuata

Baada ya dakika 20 za kurupukushani za tunda la kati ndipo tukaenda kuoga

Tukarudi nikaanza kumuuliza "una umri gani nambie ukweli" Akasema " 21 " Nikamuuliza "Unakumbuka uliniambia awali una umri gani ? Akajibu " Nilikwambia 17 ila nilikudanganya ,ningekuwa na 17 nisingekuruhusu uje nchini " Nikamuuliza nyumbani hasa ni wapi "Akajibu " popoye" Nikamuuliza wazazi Akajibu "wapo popoye ni wafanyabiashara wakubwa "

Baadae nikamsoma nikagundua hataki maswali kwa sasa anataka.....

Kilichofuata kesho yake



Asubuhi yake akaniambia " Naomba ukae humu usije ukatoka humu mpaka mimi nije ,kuna sms jack na Thomas wameniandikia ukae humu humu usije ukatoka ,akachukua sim akampigia mhudumu wa hotel ile akaja akamwambia" Huyu ni boyfriend wangu ,ni mgeni bila mimi usije ukamwambia yeyote kuwa anaishi humu ,naenda chuo ,umuandalie chakula hasa nyama ,samaki ,wali ,chakula cha huku hali, matunda umletee na chai na mkate na mayai

Hivyo vingine hatakula ,kwa hiyo akihitaji mojawapo umletee ,muda huo naenda kuoga tuletee chai "

Akaingia kwa bafu na kuoga ,mhudumu akawa ameleta chai na mayai ,tukanywa akaniaga na huge ya hatari na kuondoka .

Alipoondoka nikamuita waiter akachukua vyombo vyake nikafunga mlango na kwenda bafu kuoga kisha nikafungulia mziki kidogo nikaingia kuuchapa usingizi ,

Kilichonishangaza kuwa Angel na Ann waliondoka kwenda chuo bila kuniaga ile asubuhi..

Nilichogundua ni kwamba Ann ni mwingereza anatokea Wales ila wazazi wake na yeye wanaishi Malta,

Angel ni mmalta na Jack ni mmalta mwenye asili ya Italy ,mzazi wake mmoja ni muitalia

Wote wanasoma chuo cha saint Julian's kinachomilikiwa na kanisa katoliki

Baada ya masaa mawili Sarah akanipigia video call whasap ,kupokea alikuwa na wale marafiki zake wananipa hai nami nikawapa hai

Baada ya masaa kadhaa akarudi mwenyewe hakurudi na rafiki zake,nikamuuliza rafiki zake wako wapi akasema wapo hostel pale chuo wamekusalimia sana na pia wanakumiss .

Kesho iliyofuata Sara hakwenda chuo ,asubuhi sana alimpigia baba ake sim akimuomba hela ya matumizi,akamwambia anaomba Euro 200 ,akamwambia baada ya saa 1 aende ATM achukue hela

Akanambia Ann anakuja tujiandae twende mjini kutembea ,tukaoga na kuanza kunywa chai Ann akawa amefika ,nikatahamaki alikuwa na box la nguo shat brown lenye maua na suruali ya kaki na raba za kaki ,akasema ni zawadi yako nikasema asant

Ilinibidi nivae zawadi niliyoletewa na Ann baada ya Sarah kunitaka nivae hizo ili tutoke out .

Cha kushangaza walinitaka nivae mbele yao,nikapinga wakakataa ,wakanilazimisha,wakasema ni jambo la kawaida ikabidi nivae tu hamna namna .

Na Sarah naye akapiga nguo zake Ann akiwa amekaa nikajisemea kumbe kawaida tu,ila unabaki na boxer au kyupi

Akaita tax tukapanda tuelekea city senta tukashuka,ile tu tumeshuka nikaambiwa upo chini ya ulinzi...................

Walikuwa vijana wawili wa kizungu ,wakatoa vitambulisho kuwa ni polisi,nikaamrishwa nipande ndani ya gari lao , nikatii ,nikapanda,dreva akaanza kuendesha mpaka kituo cha polisi,wakaniamrisha nishuke chini,wakaniingiza chumba fulani,kumbuka Ann na Sarah wenyewe walibaki mjini wanaduwaa

Nilipoingia chumba hicho polisi wa kike akaagizwa aje kunihoji ,wakaniingiza selo ambayo haikuwa na mtu yeyote ,nikawa upande wa ndani askari akawa upande wa nje ila ni ndani humo humo ila tumetenganishwa na ukuta wa nondo pana

Mahojiano yakaanza kama ifuatayo
Askari" Hujambo? Nikajibu" Sijambo" Akauliza " unaitwa nani,? Nikamwambia majina yangu,akauliza tena ," Umri wako "Nikajibu"30" Akauliza" Taifa" Nikajibu" Tanzania"
Akauliza " Hapa nchini unakaa wapi" nikamwambia"Nimefikia Saint Julian " Akauliza" Umeingia humu nchini lini? Nikajibu 12 February 2022 " Akauliza "Una passport? Nikasema ninayo" Akaniomba,Nikajibu nimeiacha hotel,Akauliza ,Hotel gani? Nikamtajia jina

Akamuita askari mmojawapo walioniarrest ,akamwambia" Huyu mtu ni mgeni na tangu aingie hapa nchini ana siku chache sana na pass anasema ameacha hotel"

Askari yule naye akaniuliza" Umekuja hapa nchini kufanya shughuli gani"? Nikajibu " Kumsalimia mchumba wangu " Akauliza tena " Na pass yako inaeleza hivyo? Nikajibu "Ndiyo''

Wakaniambia twende mpaka hoteli niliyofikia ,sasa wakawa askari watatu na yule wa kike ,

Tukafika hotel hiyo wakajitambulisha kisha wakafunguliwa chumba wakaingia na kunambia niwape pass ,nikawapa ,ilikuwa vissa ,wakasoma ,kisha yule askari wa kike akaniuliza kama nina cheti cha covid ,nikachukua nikawapa vyote cha Tanzania na Malta ,kisha wakaniambia tupande gari lao turudi kituoni

Tukapanda gari tukaenda ofisi za uhamiaji ,tukashuka na kuingia ndani ,askari mojawapo akaongea na afisa uhamiaji kisha akampa vitambulisho vyangu ,yule afisa akaviangalia kisha akaingia kwenye compyuta akawambia yupo nchini kisheria,basi yule afisa akachukua bahasha akaviweka ndani vitambulisho vyangu kisha akanikabidhi

Tukatoka nje ,wale askari walionikamata mmoja wao akaniuliza" Vipi tukurudishe mjini tulikokuchukua ukiwa na marafiki zako? Nikajibu "Sawa"

Tukapanda gari baada ya muda mchache tukafika wakaniambia nishuke ,nikashuka ,ila sasa siwaoni akina Sarah wala Ann ,na polisi wameondoka,nikawa nawaangalia usoni watu kama naweza nikawaona maana sura za wazungu kama zinafanana

Nikasimama pale nusu saa, nikukumbushe kuwa wakati nakamatwa na wale polisi sim yangu alibaki nayo Sarah ,na sikukumbuka kumuomba ,alibaki nayo,nikawa najilaumu sana imekuwaje nikasahau sim yangu?

Basi nimesimama naangaza angaza hapa na pale,ni mjini kati sioni Sara wala Ann na watu ni wengi sana mjini na sina hata senti ya kunipeleka Julian's, na nikajilaumu kutowambia wale askari wanirudishe hotelini kwangu,ili akina Sarah wanikutepo wakihisi kama nimeachiwa

Baada ya kuwatafuta kwa masaa 3 bila mafanikio niliamua kuanza safari kwa mguu kwenda Julian's zaidi ya kilometa 15 ila sijui barabara sahihi ya kuelekeapo

Nikaenda kituo cha mabasi nikauliza mojawapo barabara ya Julian's akanijibu," Panda hilo basi linaenda Julian's, "*Nikajiuliza. Sasa naendaje Julian's huku sina nauli ,nilichokifanya nikusubiri ile basi ionde nianze kuifuata kwa nyuma

Basi ikaanza kuondoka nikaanza kuifuata kwa nyuma na kwa mguu ,hapa basi lilikuwa linaenda taratibu ,ila dakika chache likaanza kuongeza kasi ,likaniacha ,nikaona nikikimbia watu wanaweza kunihisi vibaya ,nikaacha liende ila nikawa nafuatilia mwelekeo ,baadae giza likawa linaanza kuingia,nikawaza sasa hapa sielewi kama nipo njia sahihi ,halafu kiu imenipiga na njaa ya hatari,

Nikawaza " sasa hapa nimuombe mtu simu anisaidie niwatafute," Nikamwendea mzee mmoja wa makamo,nikamuomba hata hakunijibu,nikasogea kwa mzee mwingine hata hakunijibu,nikamsogelea binti hata hakunijibu, nikamsogelea mmama akaniambia nitaje namba,nikasahau kuwa namba za bongo huku hazina mtandao,nilivyotaja tu akasema ,," Wewe hizo namba gani unataja " Dah,! Nikamwambia " I'm sorry ,,"

Ikumbuke kwamba nilipofika Malta Sarah alinipa namba ya sim ya mitandao ya malta na bahati mbaya sikumbuki namba hiyo na ya Sarah

Ikabidi nimuombe anielekeze barabara ya Julian's, akaniambia hiyo hapo ,kumbe nilikuwa kwenye barabara sahihi,nikaanza kuondoka ,nikawaza si nimuombe hela kama anayo nifanye nauli,nikamrudia,"Samahani nisaidie nauli nifike Julian's " Akanambia " Niende kanisani mtaa wa nyuma kuna kanisa watanisaida " Loh! Nikachoka sana,nikaondoka sasa ni usiku

Nimetembea baadae nimechoka,mawazo kibao ,nimefuata nini kwenye nchi hii,watu wanajifanya wako bize hatari na hata hawana muda na mimi. Kila ninaye ongea naye hanijibu ,Dah!! Kwa kweli

Wazo linakuja nitafute kituo cha polisi wanisaidie ,naona hawatanisaidia,sijui niende kanisani ,naona hawatanisaidia

Nikaamua niende nitafute sehemu ya maduka nikaepo mpaka asubuhi ,ukumbuke nina vitambulisho vyangu mkononi,nikaenda nikakaa duka moja kwa nje ,mtu mmoja akaja akaniambia nitokepo haraka ,nikawaza sasa hapa niende wapi mbona maisha yanazidi kuwa magumu

Nikaamua kutembea kwa mguu nikiendelea na safari,ghafla gari likasimama,,nikajiuliza nani tena au ni akina Sarah, loh! Jack akashuka akaniambia "Pole rafiki yangu ,Negro kutoka Nigeria pole sana,najua ulikamatwa polisi lakini ukaachiwa,Sarah aliniambia nikutafute vituo vya polisi,naam umeachiwa,panda kwenye gari nikurudishe Julian's, nikahisi kama mzigo mzito umeshushwa kutoka kichwani,nikahisi tabasamu

Nikaingia ndani ya gari,nikakutamo vijana wengine wawili,gari likaanza kuondoka,na mimi sijui linapoenda ila wameniambia wananipeleka Julian's,

Mimi nilikuwa kimya wakati safari ikiendelea ,huku nimekaa siti ya nyuma na Kijana mmoja,baada ya nusu saa hivi wakaniambia tumefika nishuke, wakati nashuka naangaza angaza nione hotel ,hamna, najiuliza hivi ni kweli ni mahali hapa,sijakaa Sawa Jack na vijana wake wananishika juu juu kama mhalifu,nikarespond maana nipo nchi ya watu

Wakaniingiza kwenye nyumba moja hivi ambamo utahisi watu wanaishimo,wakaniingiza kwenye chumba fulani ghorofa ya tatu kule juu,ila kwa chini nasikia kelele za watoto na akina mama nikajua kwa chini kuna watu wanaishi ila mapigo ya moyo yananipiga mpaka nahisi kuzimia,nikakumbuka wanajf walivyoniambia kuhusu kunyofolewa figo

Kijana mmoja akaniambia " Kaa chini" nikajifanya kama siwaelewi,nikapigwa mtama nikajikuta nimekaa chini,yule kijana akasema" Naitwa Thomas ,mimi ndiye mpenzi wake Sarah,umetoka Nigeria kuja kuchukua mpenzi wangu,nyani wewe ,akanipiga kofi shavuni" Akaendelea kusema" Wewe nyani,sokwe umefuata nini kwenye nchi yetu ? Akanikanyaga miguuni

Jack akasema " Niwaambie tukalale kesho atatuambia afuata nini,sasa Thomas tunza hizo nyaraka zake"

Basi wakaondoka wakazima taa ,wakaniacha kwenye chumba hicho ila hawakunifunga mikono wala miguu

Baada ya masaa kadhaa nikaona kimya ile nyumba,nikanyuka nikashika mlango nikavuta nikagundua umefungwa ,nikaenda dirishani nikafungua likafunguka,nikachungulia nje ila sioni ukingo wowote,sehemu ya kukanyaga sioni

Nikarudi nikakaa,ghafla mlango ukafunguliwa nikaamrishwa nitoke ,wakanishika suruali juu juu mpaka chini ya floor,tukatoka nje wakaniamrisha nipande ndani ya gari ,nikapanda gari likaanza kuondoka, si akina Jack tena ni vijana wawili ,wakanipeleka kwenye nyumba nyingine,mule ndani wakanipiga makonde wananiambia nimefuata nini Malta,muda huo sasa wamenifunga mikono na miguu

Wakanitwanga hadi nikahisi kuchanganyikiwa,nikaanza kumlilia mama angu niliyemuacha Bukoba

Baadae wakaniacha,wakafunga mlango wakaondoka,nililia sana,nikajilaumu sana ,nimefuata nini huku,bora ningekomaa ni Minza wangu pale Katoro kuliko kuja huku kuteseka

Kesho yake ,hakuna mtu aliyekuja mle ndani,njaa imepiga,mate yamekauka ,mwili umechoka na maumivu kila sehemu,usiku ukaingia hakuna mtu

Kesho nyingne sioni mtu,nikapiga yowe inaishia mule ndani ,nikahisi kifo kinanichungulia,sili kitu wala maji na nimefungwa mikono na miguu

Siku ya nne asubuhi sana akaja kijana mmoja ,nimelala chini mwili umechoka sana,nahisi kufa,naona kabisa naelekea kukata kamba, akanipigapiga mgongoni ,nilikuwa nimelala kifudi fudi. Nikamuomba anisaidie maji ninywe,akasema wanataka nife kwa njaa na amekuja kuangalia kama nimekufa

Basi akafunga mlango na kuondoka ,nikajua sasa ninakufa rasmi,baadae akarudi ,akaniambia nikae vizuri,nikamwambia siwezi kukaa ,nguvu sina,akanishika kama gunia akanikalisha,alikuwa na kipande cha mkate akaanza kunilisha ,na kunipa kininywesha kinywaji nisichokijua,nikasema moyoni bora tu njaa ipungue ,ghafla akina Thoma na Jack wanaingia,wanaanza kumgombeza kwa nini ananipa chakula ,na huku wanataka nife kwa njaa

Yuke kijana anawauliza " Hivi nyie hamna huruma na binadamu? Thoma anadakia huyo si binadamu ,huyo ni sokwe,kwanza ungemletea ndizi angeshukuru kuliko kumpa mkate

Wakamwambia kijana jina silikumbuki vizuri. " Acha kumpa chakula ,hebu twende,kabla hawajaondoka,Jack akamwambia Thomas "Sasa huyu sokwe tufanye hizi tumtafutie mwanaume amhudumie ili apate adabu

Nikasema moyoni nimekwisha,,mungu wangu ,wakaondoka na kufunga mlango ,sasa nikawaza wanataka wanifanyie kinyume cha maumbile. Machozi yakatiririka kama kimto kidogo


Siku ya tano ,hakuna mtu aliyekuja,siku iliyofuata ya sita, hakuna aliyekuja,njaa na kiu vimepamba moto hatari,na miguu na mikono imeanza kuvimba kwa sababu imefungwa kwa muda mrefu

Siku ya nane wakaja wakiwa wanaume sita akiwemo Jack na Thomas na kijana aliyenisaida mkate na wengine watatu,mmoja alikuwa mwenye asili ya afrika

Mmoja akawambia kwa hiyo kazi yupo sawa na anaonekana hajala siku nyingi ,ili ashughulikiwe vizuri mfungue na mpe chakula ili afanyiwe kazi sasa

Basi kijana yule akainama na kunifungua minyororo iliyokuwa imekazwa na kufuli,nikahisi kupumua kidogo. Jack akaenda kununua chakula ,akaleta ,sikuangalia kama kinapita au lah! Maana walileta chakula cha kimalta ,nikagonga kisha Jack akaagizwa alete maji ,akaleta nikanywa ,nikaomba mengine ,wakasema kwa vile nilikuwa sijanywa maji kwa muda mrefu waniletee Lita 3 ,Jack akaleta nikanywa hadi yakaisha,nikahisi uhai umeanza kurejea

Baadae wakaongea kimalta wakanifunga miguu na mikono wakaondoka,nikahisi sasa wakija wanakuja kunishughulikia

Siku ya tisa asubuhi,hapa walikuja wanne ,Thomas ,yule mwafrika na kijana mwingine ,yule mwafrika akasema wanifungue ,wakanifungua

Wakaniambia nisimame nikumbatie ukuta ,sikurespond ,yule mwafrika aliyejaza muscles,akanipiga kofi kichwani ,ikabidi nisimame,nikakumbatia ukuta,yule mwafrika akanisogelea akanishusha suruali. Nikasema kwa kiswahili " Mungu wangu anisaidie" Yule mwafrika akasema " Mmmh " akaniuliza kwa kiswahili " wewe ni mkenya" Nikajibu kwa kiswahili " Ndiyo " akaniacha," akanambia kwa kiingereza sasa " Vaa suruali " nikavaa ," Thomas akahamaki ,akauliza vipi kulikoni mbona zoezi halifanyiki " yule mwafrika akajibu " Naomba mtoke muwe pale nje ,huyu mtu namfahamu ,nichukue maelezo yake kisha nitawaita," ,Thomas akakataa ,akasema " Una njama gani na huyu mtu "

Basi mwafrika akaanza kunihoji ,Wewe ni nani na umetokea nchi gani na umefikaje Malta"? Hapo anatumia kiswahili" Nikasema " Naitwa cosovo si jina halisi,nikataka nimwambie nimetokea Kenya ,nikaamua kusema nimetokea Tanzania na nikamsimulia jinsi nilivyofika Malta. Basi akasikitika sana na kunipa pole ,kisha akaniahidi kunisaidia,akasema " Wewe tulia humu ndani ,nitaenda nikusaidie utoke ,maana nikikusaidia sasa hivi hapa kinguvu na tupo nchi za watu tunaweza kuumia ,wewe tulia nikatafute askari waje wakutoe " Ukumbuke hapo pote tunaongea kiswahili

Alipotaka kuondoka nikamuuliza jina lako na hujanambia unatokea nchi gani ya Afrika Mashariki akajibu" ooh ,Naitwa Jose nimetokea Kenya" Nikasema " sawa " wakaondoka

Nikafurahi,nikaanza kupata matumaini ya kuwa huru,nikafurahi kumpata mswahili mwenzangu,nikasema nimepona kufanyiwa unyama huu

Lakini dakika zinayoyoma,masaa yanaenda,Mawazo na masikio yapo mlangoni nikisubiri mlango ugongwe wawe askari wamekuja kuniokoa

Naona giza taa zinawaka ikiashiria usiku umeingia,dah! Moyo unaumia sana,ghafla mlango unafunguliwa ,nikahisi ni Jose na askari lah hasha! Ni akina Thomas na Jack,wanafungua mlango na kunishika juu juu na kunitoa nje na kunibakiza kwenye gari na kuondoka

Nikawaza napelekwa wapi masikini,najutia safari yangu Malta,gari linasimama,nabebwa juu juu narushwa kwenye mtumbwi nikagundua nipo ziwani au baharini

Lilikuwa jahazi ,yale yanayoendeshwa na upepo majini ,wakanirushamo,nikiwa nimefungwa mikono na miguu,wakalisukuma jahazi kuelekea kati kati ya maji na kuliachia

Likaanza kusukumwa na upepo ,nikahesabu sasa nimekufa rasmi ,likaenda ,likaenda na likaenda ,kama alfajiri hivi bado nimelalamo sijui nifanye nini ? Likasimama ,nikaamka kuangalia kumbe limefika pembezoni mwa nchi kavu,kuangalia naona nyumba nyingi zenye taa ,na watu wapo ufukweni,nikapiga kelele watu kadhaa wakaja ,wakanishika wakanitoamo ,wakaniweka nchi kavu,nikawaomba wanifungue minyororo,wakanifungua ,nikaanza kuwaongelesha,hajui kiingereza,basi baada ya kutoelewana lugha wakaniacha wakaendelea na shughuli zao,nikatembea naelekea kwenye mji ,kila ninaye jaribu kumuongelesha kimya,nikafika mjini

Nahisi uchovu,njaa ya hatari,nilipofika mjini kila mtu anaongea kilugha chao,nikawaza acha nitafute kanisa lilipo wanipe msaada ,bahati nzuri nikafika kanisani,nikaenda moja kwa moja kwa father, nikamsmulia mkasa mzima na kumuomba anisaidie nifike Julian's ,Father akaniahidi ,kumbe pale nipo kwenye kisiwa kingine ila ni upande wa Malta

Nikaishi kanisani hapo ,maisha mazuri ,nikaanza kuona uhai umerejea ,amani na furaha

Baada ya siku tatu ,father akanipandisha panton na kunipa Euro 2 kama matumizi,pantoni ikafika, nikawa nimepewa ramani ya kufika Julian's, nikachukua basi nikalipa Euro 1 na kufika Julian's, na Julian's kubwa ,sijui nilipofikia je ni karbu na mtaa ule? Nikaanza kuulizia hotel ya pope,kila mtu sijui, wananiambia angalia code ,

Usiku unaingia bila mafanikio,nawaza niulizie chuo cha akina Sara ,nahisi nitakutana na akina Thomas ,naogopa tena,baadae nikatafuta sehemu chini ya mti ,usiku umeingia nikalala ,kesho yake nikauliza chuo Julian's ,dreva tax akaniambia Euro 1 ,ikabidi nimpe iliyobaki,akanipeleka mpaka chuo,ulizia Sarah na Ann,wanasema hawajui,wananiambia wapigie sim,nachoka mwili mzima,mpaka saa 8 siwaoni,muda huo nahofia kukutana na akina Thomas na Jack

Imefika saa 10 jioni bila mafanikio naamua kuondoka maeneo ya chuo ,nisije nikakutana na wabaya wangu

Nikatembeaa mpaka giza linaingia sijui naenda wapi na natoka wapi,,nikawaza sasa kesho asubuhi niende kituo cha polisi kutoa taarifa na akina Jack wakamatwe wanirudishie nyaraka zangu niondoke Malta nirudi nyumbani

Nikiwa katika dimbwi la mawazo, natafuta sehemu nikae ,nakwapuliwa narushwa kwenye gari tena,kuangalia ni nani tena,ni Jack na Thomas na wengine wawili

Wakanipeleka kwenye nyumba ya mwanzo,sasa hapa ndo wakaanza kunipiga ovyo ovyo,wananiuliza nimemfuata tena Sarah mpaka chuoni,kipigo cha hatari na nimelia kama kichanga na mdomo wangu wameubana kwa kitambaa na wamenifunga mikono na miguu,wanaapa kuwa awamu hii hawaniachi salama ,lazima nife

Baadae wakaniacha,wakafunga mlango na kuondoka, baada ya siku mbili wakarudi wakaendeleza kipigo,sasa nimechoka na siongei,wanapiga kama gunia,baadae wakanikalisha,Jack akachukua kisu akanikata kidole cha kati na kukitoa ,dah nikalia kama chizi. Mpaka wa chini ya ghorofa wakasikia na kuja kugonga mlango,wakagoma kuwafungulia,baada ya dakika chache mlango ukagongwa wakisema ni polisi,ikabidi wafungue,kweli walikuwa polisi,wakawakamata ,na mimi wakanifungua, wakatupandisha kwenye gari la polisi mpaka central,damu zilikuwa zinavuja wakanipeleka hospital nikapewa matibabu na majeraha ya sehemu zingine za mwili,jioni wakanirudisha central, tukahojiwa,nikatoa maaelezo mwanzo mwisho,kisha akina Jack wajatoa maelezo ,

Baadae mimi nikapelekwa chumba kingine ,wakanipa chakula na maji na godoro nikalala,wengine niliwaacha chumba kingine,

Asubuhi ,nafuata na polisi kwenda chumba cha mahojiano,namkuta Sarah na Ann nao wameletwa

Sarah na Ann walivyoniona walishtuka na wakadhani polisi ndo wamenitesa vile maana tangu nilipokamatwa na wale polis wa awali hatukuwahi kuonana tena,basi polis akaanza kuwaeleza vita yetu kisa Sarah,Sarah alisikitika na kububujikwa na machozi

Alilia na kumlaumu Jack na Thomas kwa mateso waliyonipa ,akisema aliachana na Thomas muda mrefu na anataka nini ?

Thomas alitakiwa anipe nyaraka zangu za usafiri,polis wakamchukua na kwenda naye chuo na kurudi na nyaraka zangu na kunikabidhi na kuniruhusu tuondoke,mimi ,,Sarah na Ann

Tuliondoka na kufikia hotel niliyofikia,Sara na Ann ni kunihurumia tu na kububujikwa machozi,tulikaa nao siku mbili na Sarah kunipa Euro 1000,nikakata ticket euro 500 nauli ya kufika Tanzania ,nikabaki na Euro 500 matumizi

Mwisho

Aliye na swali karibu
Sishangai kuwa unatokea Bukoba maana watu wa kanda hii mnapenda sana majuu ila pole sana.
 
Jamaa na ushamba na ukolo mwingi aisee. Yani mpaka hao jamaa wanamdaka ni kwasababu alishindwa kufika mwenyewe hotelini, jiji lilimchanganya.

Hajilindi kwa namna yoyote na yupo ugenini aisee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom