Mrejesho inteview TRA

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,102
Reaction score
828,975
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Moshi Jonathan Kabengwe, amesema majina ya Waombaji wa ajira 1,596 zilizotangazwa na TRA hivi karibuni yatatangazwa rasmi kesho March 22 2025 kupitia tovuti ya TRA (www.tra.go.tz) kwa ajili ya usaili wa kuandika utakaofanyika March 29 na 30 mwaka huu kwenye Vituo 9 tofauti vya Tanzania bara na Visiwani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo tarehe 21.03.2025, Kabengwe amesema kati ya Waombaji 135,027 waliotuma maombi ya nafasi hizo za ajira, Waombaji 112,952 wamekidhi vigezo na kuitwa kwenye usaili wa kuandika ambapo sasa kila Muombaji atatumiwa katika barua pepe yake taarifa ya kuitwa kwenye usaili ambapo pia Waombaji wenye mahitaji maalum watawekewa utaratibu maalum ambao utawasaidia kufanya usaili bila usumbufu.

Kabengwe amesisitiza kuwa Waombaji wote watatendewa haki na kwamba usaili huo utafanyika kwenye Mikoa 8 ya Tanzania Bara na kwa Visiwani Zanzibar usaili utafanyika Unguja na Pemba kama inavyoonekana kwenye orodha ifuatayo.

1. Dar es salaam ambayo itahusisha Waombaji kutoka Dar es salaam na Pwani.

2. Zanzibar ambayo itahusisha Waombaji kutoka Unguja na Pemba

3. Arusha ambayo itahusisha Waombaji kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.

4. Dodoma ambayo itahusisha Waombaji kutoka Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa na Tabora

5. Mtwara ambayo itahusisha Waombaji kutoka Mtwara, Lindi na Ruvuma

6. Mbeya ambayo itahusisha Waombaji kutoka Mbeya, Songwe na Rukwa

7. Mwanza ambayo itahusisha Waombaji kutoka Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu.

8. Kagera ambayo itahusisha Waombaji kutoka Kagera na Geita.

9. Kigoma ambayo itahusisha Waombaji kutoka Kigoma na Katavi.
 
Siku isiyo na jina maandamano ya wasomi yatakapolipuka hakuna wa kuzima huo moto. Kwasasa wamesoma hawajaelimika, kitaa kinawaelimisha wasomi baada ya hiyo elimu nobody can stop them. Mungu wabariki hawa watu aisee.
 
Nmependa hy kugawanyisha mikoa.

Naamini hawatolialia kama waalimu 😎
Mikoa imegawanywa Kwa ajili ya interview tu mkuu,kufanya urahisi watu wasitoke mbali sana kufuata interview..nafasi hazigawanywi mkuu kama wanahitajika tax officer sita bas waombaji wote wa hiyo position nchi nzima mtagombea nafs sita tu.
 
Taadhari UGONJWA wa akili wakati wa Nyerere ilikuwa ukimaliza shule unapangiwa kituo cha kaziπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Samia wapate udahili VETA


View attachment 3279590
UGONJWA wa akili wakati wa Nyerere ilikuwa ukimaliza shule unapangiwa kituo cha kaziπŸ₯ΊπŸ₯ΊπŸ₯ΊπŸ€”πŸ˜‚πŸ˜­
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…