Mrejesho baada ya kuagiza Gari toka Japan

BROKE BOYS

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
13,215
39,039
Wakuu salama?

Kwanza kabisa niwashukuru wanajukwaa hili kwa ushirikiano mzuri mlionipa kabla sijaagiza chombo.

Nilikua sina uzoefu wa kuagiza hivyo ilikua mara yangu ya kwanza lakini nilifanikiwa na chuma ilifika imenyooka sana.

Nilitembelea kampuni Nyingi sana za japan kama Beforward, sbt, enhance, trust, autocom na real motors.

Nilitumia kama week mbili kutafuta gari lengo ilikua kwaajili ya wife hivo alikua anataka pearl white. Beforward niliona gari za kawaida na kama ukipata imenyooka bhs na bei imenyooka pia, SBT gari zao ni za kawaida sana na nyingi zmeenda mileage.

Nikatembelea trust na enhance kiukwel hawa wanagari kali sana hata bei zao zmenyooka pia. Mwisho wa siku nikatembelea AUTOCOM JAPAN hawa watu wana gari kali sana afu bei poa.

Baada yakupata gari tunayotaka nika regsta mjapan akanichek whatsapp akajitambulisha japo sikumzingatia nikamtumia ist tuliyoipenda ilikua $2620 C&F tukabargain mpaka $ 2220 so alinipa discount ya $400. Gari ilikua Auction Grade 4

Asbh akanichek anitengenezee invoice nikakubali niliwaza nikiikosa ndo bhs gari nzuri macho huwa mengi. Akanitumia kwa whatsapp japo nilikua simwamini kabisa nikampiga piga maswali nikawashirikisha watu nikaenda mpaka ofisi zao posta pale wakasema iko sawa nilipie tu na mjapan wanamjua ndo sales officer mkuu na walishangaa discount kanipa kubwa sana hata wao huwa hawapewi so ilikua baht tu.

Utaratibu wa kulipia autocom ni unafanya international transfer (TT) yani unaweka cash kwenye A/c yako then wanatransfer kwenye account yao japan ili kuepusha third parties hawataki pesa ishikwe mkononi.

Nililipia 06/04 nakumbuka kesho yake akanichek akasema muamala ameuona so anaanza na inspection na kutafuta space kwenue shipping lines.

Nilisubir kama siku 50 mpaka naipata gari bandarini. Nikipiga hesabu gharama ya gari, kodi na clearing nmetumia kama 12.5 million

Gari kwa kweli nilivyoiona kwa macho laivu ni kali tofauti na inavokua mtandaoni gari imenyooka battery iko safi, engine fresh, imekuja na fog, spare tyre nilichobadilisha ni oil na filter na airfilter bhs. Gari ni inachanganya fasta haili mafuta iko gud sana. Gari imefika ina 66,000 mileage.

4401c86e-7aa5-45dd-9fe0-c8e6e83b4e16.jpg



Siendi tena yard/ showroom gari naagza japan, shida uwe mvumilivu bhs kama unaharaka nenda showroom.

9d39d471-4a59-4828-9951-dae9de92f0ac.jpg
 
Umejikomboa na adha za usafiri wa mjini, sasa kitunze kidumu, jitahidi E yako iwe half tank, service yako iwe kwa mujibu wa manual na sio mafundi wetu aisee, wenye haraka zao road wapishe, jifanye learner kila siku. IST inaelezea kuwa umejikwamua, hivyo ipende aisee, miaka 7 itakuwa nawe.
 
Mkuu yako kali sana dah...Sbt zao mechokachoka sana upo sawa mkuu.

Nimeagiza Sbt toka 9/4/21 gar imefika 13/7/21 af wamekuja kuniambia 20/7/21 af wananiambia nilipie storage sh 25000 per day kuanzia 13/7 mpk nitakapo toa kwa hili ntakwenda petrol ofisin kwao kitakachotoa kitakua mjadala humu.

Profoma mpka kufikisha gar apa ni 12,500,000 af wananiambia et ushuru umepanda niongeze la lak Saba hiv wakati nikiangalia TRA calculator inanionyesha ushuru umeshuka sana pind naagiza ulikua 6.6m leo ushuru ni 6.1m kwa ist ya 2006 af mjomba ananiambia ushuru umepanda sijui aniona mi wa maporini mzee leo sikukuu kesho asubuh sana ntakua ofisin kwao na kidumu changu cha lita 5 kitakachotoa hakitakua Siri kama hakutakua na maridhiano
 
Mkuu yako kali sana dah...Sbt zao mechokachoka sana upo sawa mkuu..

Nimeagiza Sbt toka 9/4/21 gar imefika 13/7/21 af wamekuja kuniambia 20/7/21 af wananiambia nilipie storage sh 25000 per day kuanzia 13/7 mpk nitakapo toa kwa hili ntakwenda petrol ofisin kwao kitakachotoa kitakua mjadala humu...

Hahahaa bila shaka unawasiliana na wabongo, me nilikua nachat na mjapan mpaka gari inafika. Wabongo tuna njaaa sana
 
Wakuu salama?
Kwanza kabisa niwashukuru wanajukwaa hili kwa ushirikiano mzuri mlionipa kabla sijaagiza chombo.

Nilikua sina uzoefu wa kuagiza hivyo ilikua mara yangu ya kwanza lakini nilifanikiwa na chuma ilifika imenyooka sana....
Hongera kwa kupata ndinga ikiwa kwenye ubora wa hali ya juu.

Naomba nipatie namba ya whatsap ya huyo mjapan nahitaji RAV4 killtime.
 
Back
Top Bottom