Mrejesho 2: Nimempa mimba mwanafunzi mwenzangu

KAFA.cOm

JF-Expert Member
Jun 22, 2013
1,301
739
Habari humu MMU,

Miezi michache iliyopita nilileta thread nikiomba ushauri nifanyeje ili kuliepuka tatizo, namshukuru MUNGU nililimaliza salama binti alikuja kwa mama yangu ambako ndo anapotunzwa.

Na pia nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 na kwa sasa nasubiria mtoto kwani binti anategemea kujifungua mwezi wa 6.

Nashukuruni MMU kwa ushauri wenu yakinifu.Kwa kweli nilichanganyikiwa kiasi cha kutaka kunywa sumu saa nyingine nikawaza kukimbia shule mpaka kuna wakati nilidumbukia kwenye utumiaji wa canabis sativa ili kupunguza stress.

Ila kibaya zaidi ni kwamba mtaani nimedhalilika asana na ile sifa yangu ya upole imepotea kabisa, nilichojifunza kwenye hili suala ni kwamba marafiki zangu wote walinikimbia kabisa.Mrejesho: Nimempa ujauzito mwanafunzi mwenzangu, naomba ushauri
 
nikikumbusha tu hii inatakiwa kuandikwa kwa mcharazo " canabis sativa".
 
Pole sana mkuu, kuna wakatimukiishi kama mtakatifu sana ni shida kwenye jamii. Hongera kwa hatua
 
Pole na hongera mdogo wangu,siku nyingine utajifunza kwamba anaeleta aibu ni mwanaume,unatakiwa kutumia ubongo sio moyo,jifunze kuchanga karata zako
 
Hongera mkuu. Naona umeamua kuanza majukumu mapema. Lakini kwa msaada wa familia zenu naamini mtavuka salama.

Ushauri: Hakikisha unaubeba ubaba ipasavyo. Lakini pia utafanya kosa kubwa sana na utakuja kulilipia huko mbeleni kama utajaribu kumtelekeza huyo dada wa watu. Amekusaidia sana. Hakuwa mbinafsi. All the best
 
we jamaa ushamaliza pepa la f6. daa we mwanaume kubaliana na hali hongera hukumuua hiko kiumbe maana najua akili zetu zilivo. natamani ujipe namba yako pm tupige story. me nko first year chuo kimoja karibu sana kk. natuma mdada anaendelea poa coz wazaz wametoa sapot na ushirikiano.
 
Kweli kaka huyu binti alinibeba kupita maelezo nampenda kwa kweli
 
we jamaa ushamaliza pepa la f6. daa we mwanaume kubaliana na hali hongera hukumuua hiko kiumbe maana najua akili zetu zilivo. natamani ujipe namba yako pm tupige story. me nko first year chuo kimoja karibu sana kk. natuma mdada anaendelea poa coz wazaz wametoa sapot na ushirikiano.
Usijali mkuu pamoja sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom