Mrejesho: Nimempa ujauzito mwanafunzi mwenzangu, naomba ushauri

KAFA.cOm

JF-Expert Member
Jun 22, 2013
1,301
739
Habari zenu MMU,

Ni wiki sasa imepata tangu nilipoleta hapa jamvini thread ya kuomba ushauri
Nimempa ujauzito mwanafunzi mwenzangu, naomba ushauri asanteni kwa ushauri wenu pia na kejeli pia zilikuwepo.Niliufanyia ushauri wenu kazi na leo nataka niwape feedback.

Mara baada ya kuonana naye yule binti nilimwomba asinitaje kabisa mpaka nitakapomaliza high school nikamwahidi kuwa gharama zote nitakuwa nampa kwa siri niliweza kuzungumza na mama yangu na akanielewa vyema tu ila akaniambia mwambie binti asingizie mtu mwingine ili mimi niweze kumaliza elimu yangu.

Ilipofika Jumamosi mama yake akahisi ana tatizo akampima mkojo na akagundua kuwa ni mjamzito binti akakimbia kwa rafiki ake bahati nzuri mama hakupanic kiasi kikubwa jioni binti akarudi nyumbani mama akamweka chini akamwomba amtajie aliyempa ujauzito binti akamtaja mtu wa mbali huko kabisa kiasi chake mama akaamini.

Mama akaenda kwa rafiki zake huko akaja kumwambia binti kuwa akubali ile mimba itolewe ili aweze kuendelea na shule binti akagoma kabisa akamwambia ka mimi nilivyomwambia kuwa atakuja kusoma huko mbeleni baada ya kujifungua ila kwa sasa hayupo tayari kutoa mimba mama akamuuliza nani atamsomesha wakati baba wa mtoto hamjui? Binti akagoma kunitaja ili kunisitiri nimalizie elimu yangu jana nimeonana naye na yeye ananiambia kuwa kuliko atoe ile mimba bora afe na mtoto.

Wadau nahitaji experience yenu hapa tena kwani mimi pia nimeshindwa kumwambia akubali itolewe.
 
Wewe mwenyewe ni mwanafunzi kula, kulala, na kusoma unategemea kwa wazazi sasa huyo mama na mwanao utawapa nini? Au wazazi wako ndiyo wamekubaliana na wewe kua huyo mkwe wao na watakaomgharamia?
 
Wazazi wa siku hizi....

Enzi zetu unatimuliwa uende kwa alokupa.mimba.....mbona utamtaja tu

Ila huyo binti mjinga

Mleta mada mbinafsi

Khs mama wa kijana i reserve my comment

Mngekuwa na busara mngeenda kumuona mama wa binti mtafute way foward hususan kwa huyo mtoto

Ila sijui huyo binti anajua bomu alitengenezalo
 
fanya mpango uendelee kutanua njia, mana hamna namna nyingine.
 
Tuma mtu ajifanye ametumwa na aliyempa mimb pesa waombe account ya mama yake au yake mwekee minimum 20 million hivi au 15 ukijitahidi 10 na itabidi ujazie tena na tena kumuhudumia hadi mtakapoishi pamoja. ili isaidie mama yake kutulia harafu naye atulie ajue pesa ya kusoma ipo na kulea mtoto wako.

Usimtoe huyo mtoto ni kaisha yako.

Sasa baadae utafanya njia ya kujitambulisha ila peleka pesa kwanza haraka haraka. Ongea na mama yako ili musimuue huyo mtoto kiumbe cha Mungu.

Ole wako uje umkimbie ukikua atakufungulia kesi unalo.
 
Huyo mkweo anaetaka bint yake achoropoe huo ujauzito atakuwa kipindicha michezo radio tanzania waqt uleeee(mbili kasoro robo)wewe mwenyewe utakuja kumtosa huyo bint kwa namna yako bado hujatulia.
 
Wewe unasoma yeye haendelei na masomo..baadae unakuja kumegeuka!
Hukumu ya watu kama nyie ni kunyongwa hamna namna..kwanza mnasababisha uncontrolled demographic,magonjwa,watoto wa mitahani,unyanyasaji wa wanawake,mnarudisha nyuma mchakato wa women empowerment..wewe jamaa honest hufai
 
  • Thanks
Reactions: nao
Wazazi wa siku hizi....

Enzi zetu unatimuliwa uende kwa alokupa.mimba.....mbona utamtaja tu

Ila huyo binti mjinga

Mleta mada mbinafsi

Khs mama wa kijana i reserve my comment

Mngekuwa na busara mngeenda kumuona mama wa binti mtafute way foward hususan kwa huyo mtoto

Ila sijui huyo binti anajua bomu alitengenezalo
Masikini binti hajui chochote, mwisho wa siku huyu kijana aweza kuja kumgeuka huyu binti akitaka kuoa wasomi wenzake tena kipindi hicho kasahau yote na kumwona huyu binti mshamba flani mweeh.
 
Watoto wa siku hizi kujifanya ujuaji mwingi kwamba mnaweza saaaana kubanjuana ninyi kwa ninyi...... Kwa hiyo wewe umalize high school mwenzio amalizie leba? Daaaa sio vizuri hata
 
Wazazi wa siku hizi....

Enzi zetu unatimuliwa uende kwa alokupa.mimba.....mbona utamtaja tu

Ila huyo binti mjinga

Mleta mada mbinafsi

Khs mama wa kijana i reserve my comment

Mngekuwa na busara mngeenda kumuona mama wa binti mtafute way foward hususan kwa huyo mtoto

Ila sijui huyo binti anajua bomu alitengenezalo
Litamlipukia Mwenywe sasa Hivi haezi shituka si penzi limekolea ngoja .....
 
Wewe mwenyewe ni mwanafunzi kula, kulala, na kusoma unategemea kwa wazazi sasa huyo mama na mwanao utawapa nini? Au wazazi wako ndiyo wamekubaliana na wewe kua huyo mkwe wao na watakaomgharamia?
Kwahiyo unaunga mkono mimba itolewe?
 
Back
Top Bottom