Mratibu huyu anakiuka agizo la rais

motonkafu

JF-Expert Member
Dec 2, 2015
1,019
705
Ikumbukwe waraka wa elimu bure ulikuja na agizo la rais akikataza michango yote ya elimu, na kweli January 2016 michango ikafutwa na waliochangishwa baada ya hapo wakatumbuliwa immediately.

Sasa leo huyu mratibu anatembea na fomu maofisini akiwataka walimu wachangie madawati. Kwa mujibu wake anasema wameamua kuiita harambee ya madawati.

Hivi kuchangisha walimu pesa ya madawati sio kukiuka agizo la Mh. Rais la kukataza michango yote ya elimu???
 
serikali hii si yawatumishi ni ya wananchi kwani sioni lolote linalomwona Mwalimu kama kiungo muhimu katika Elimu Bure..aaaagh ni nishachoka..
 
walimu wenyewe mishahara yao kidogo, hawana nyumba za kuishi, mazingira magumu ya kazi, tena michango duu hapo ni kuwaonea, kwanini wazazi wa hao watoto wasichangie? Hii ndiyo tabu ya kuchanganya siasa na elimu. Dunia ya leo hakuna "free lunch" mzazi unawajibika kumhudumia mwanao kwa mahitaji yake, haiwezekini kuzaa uzae wewe, dawati achangie mwingine, huku ni kudanganyana.
 
"NO FREE LUNCH" Katika dunia ya leo na kutaka kuamini hilo chunguza watoto wa wakubwa wote wanasoma uko kwa buree bin bwerere jibu husinipe mimi.... we must share cost
 
Walimu mmezidi uoga ifikie atau watu wajitambue huo mchango Mara mia ukanywa hata kahawa mshahara wenyewe kiduchu na mchango tena
 
walimu saa zingine nataman hata kuwatukana... unashindwa kumpa makavu huyo mratibu... mwambieni akakusanye hiyo michango kwa yule aliyesimamisha michango ya madawati kwa wanafunzi achange yeye... si aliona mtelemko achange sasa asilete upuuzi....!
 
bora nyie mnaombwa, halmashauri fulan kanda ya ziwa walikuwa wanarazimishwa kabisa
 
Back
Top Bottom