Mrahaba wa uchimbaji madini Tanzania umekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrahaba wa uchimbaji madini Tanzania umekaaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MANGI1979, Mar 26, 2012.

 1. M

  MANGI1979 Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi za wenzetu hawavutii wawekezaji kuchimba madini yao hata kama hawana teknolojia ya kutosha.Kwanza ndio wanaringa maana yanajiuza yenyewe ukiwashwa kuwekeza masharti yao ni magumu na wanataka pasu kwa pasu na muda wowote unaweza kuchomoka wakiamua nguvu ya umma.hapa kwetu mikataba miaka mingapi wakuu?

  Asilimia ngapi inapata serikali wakuu?ni kwa nini wananchi wenyewe wakichimba rasilimali zao kama madini unanyea ndoo mkuu?kuna haja gani baraza kutunga mtihani shule za msingi kuwauliza wanafunzi shule ya msingi kutafsiri maana ya rangi za bendera ya taifa hasa njano wakuu?

  Serikali imeshafanya geological survey kujua kiasi cha madini tuilichobakiza ili hali wanafunzi wanakosa mikopo hasa wale watoto wa mhogo mchungu na senga wakati wa vigogo wanapeta?tuna haja gani ya kusema tumethubutu, tumeweza, tunasonga mbele huku unabembeleza madaktari, watoto wanasomea ardhini kukosa madawati huku mkurugenzi wa halmashauri akitembelea v8 200m?

  Zigawanye uone ni madawati mangapi mkuu.yanatosha kabisa shule zote na mengine yatatumika kwenye mikutano ya kijiji.kwa nini tusilete wachina waka"bid" tender ya kuongoza nchi na kufunga watu? Ndio maana waajiriwa wa sasa serikalini hawana machungu na uzaledo tena kama zamani,ukimpa chance tu kwenye uongozi penye chakula, ni afadhali ya rooney au drogba yaani hakosei.

  Halafu serikali inakataza ufisadi huku wakikata tawi la mti waliokalia.inakuwaje mzazi anamfundisha mtoto asile bila kunawa huku yeye akifakamia mitonge maji baada ya kushiba?

  Wakuu tutafakari tuchukue hatua hata kama ni dormant.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Inauma sana--Mizamba
   
 3. C

  Cape city Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unaongea mambo mazito sana ndugu yangu. Nchi yetu inasikitisha sana na ukijifanya mjuaji wanaweza hata kukuua hao wenye Nchi...
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Muulize Zitto Kabwe ndio aliteuliwa na Kikwete kufatilia hayo unayoyauliza, anayajuwa nje ndani na Barrick wakamsaidia! yes, wakamsaidiaa jimboni kwake, mimi nasema walimpa rushwa.
   
 5. broken ages

  broken ages Senior Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Katika hili swala la madini tukubaliane tu ya kwamba kuna baadhi ya viongozi na kama siyo wote ktk wizara husika wananufaika binafsi wakishirikiana naa hao tunaowaita wawekezaji maana sioni maana yeyote ya kuwa na hiyo tunayita mirahaba na badala yake ilitakiwa kutengenezwe utaratibu wa kutathimini madini yayovunwa na Hawa watu halafu yake tuweke kiwango halisi cha kodi ama serkali iwe na sehemu yaaake ya hisa katika mavuno aidha asilimia hata thelathini ama arobaini iwe ya serekali kwa manufaa ya nchi.na kama hilo haliwezekani basi ni bora hao wataalamu wachimbaji waajiriwe na serekali walipwe kama ni ujira na serekali inunue hizo equipments za kuchimba na ifanyye hiyo kazi yenyewe hili nalo haliwezekani?kwani wataalamu wetu wa uchumi kazi yao nini?
   
Loading...