Mavipunda
JF-Expert Member
- Jun 27, 2012
- 7,243
- 8,097
Kwa wale watambuzi wameshaelewa maana ya "miradi ya tembo mweupe" kwa kifupi miradi kama hii huwa haina tija kwa wananchi na mara nyingi huwa haikidhi malengo tarajiwa.
Uwanja umeongezwa njia ya kurukia ili ndege kubwa ziweze kutua na kuruka lakini miundo mbinu mengine kama "Depature na Arrival Lounges" zitabaki kuwa vibanda kwa muda mrefu. Ili baadhi ya miundo mbinu iweze kujengwa ni lazima serikali iwe na fedha nyingi za kulipa fidia kwa wakaazi wa maeneo jirani ambao wapo jirani na uwanja huo kihalali kwani maeneo hayo yalipimwa.
Uamuzi wa kuongeza njia yalifanywa kwa kukurupuka sana bila ya kufanya utafiti.Ni vyema serikali ingetumia fedha zile kulipa fidia ili wananchi waondoke kwanza kwani kwa sasa hata usalama wa maeneo yale ki Aviation upo hatarini.
Au serikali ingeamua tu moja kwa moja kujenga huo uwanja mpya kule Msolwa badala ya kufanya miradi isiyo na tija