Mradi wa Ndungu hatarini kufa - NANI MWENYE JUKUMU LA KUNUNUA MATREKTA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mradi wa Ndungu hatarini kufa - NANI MWENYE JUKUMU LA KUNUNUA MATREKTA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ustaadh, Dec 15, 2010.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MRADI wa umwagiliaji wa Ndungu katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro unakabiliwa na matatizo mengi na kuathiri utekelezaji wa kilimo kila msimu.

  Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja Mradi kutokuwa na watumishi wa kutosha, vyombo vya usafiri na mitambo, ikiwemo matrekta kwa ajili kuhudumia mradi.Katika taarifa yake aliyoitoa juzi wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Joseph Mkude, Meneja wa Mradi, Alson Kavumo alisema, serikali isipoingilia kati na kurekebisha matatizo hayo, mradi huo hautafikia malengo yaliokusudiwa.

  Kavumio alisema kutokana na mradi kuwa na ukubwa wa hekta 680, imekuwa vigumu kwa wataalamu wa kilimo kuwatembelea wakulima wote kwa wakati mmoja kutokana na mradi huo, kutokuwa na magari na kusababisha wakulima kutopata ushauri kwa wakati.

  "Mradi pia hauna matrekta, hili ni tatizo kubwa mno kutokana na ukweli kwamba inatulazimu inapofikia msimu wa kilimo tukodishe mitambo na matrekta," alisema.

  Kwa upande wake Mkude alisema matatizo hayo, yamekuwa yakiathiri utekelezeji wa malengo ya mradi na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha mradi huo mkubwa kuliko yote katika Wilaya ya Same.

  Mkude alisema mradi huo ni muhimu kwa wakulima wa eneo hilo na taifa kwa ujumla kwa kuwa mapato yake, yatachangia uchumi wa wananchi, lakini pia kuongeza kasi ya uzalishaji wa chakula nchini.

  Mradi huo katika kipindi cha miaka mitatu, 2007-2009,

  Wakulima 1,500 katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2007 hadi 2009, wamenufaika na mavuno ya mpunga ambayo yaliwaingizia fedha Sh 5.44 bilioni.
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Feb 3, 2017
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,001
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hii thread haikupata wachangiaji ila n7 kweli mradi unakufa
   
Loading...