Mradi wa DMDP, Kata ya Mbagala unavyo suasua kulikoni?

Rusende

Senior Member
Jul 27, 2016
120
90
Wakazi wa kata ya Mbagala Manispaa ta Temeke tuliupokea kwa shangwe kubwa mradi huo wa uboreshaji wa miundo mbinu ya ujenzi wa barabara za kiwango cha lami, mifereji na taa za barabara ni unaofanywa na kampuni ya ujenzi ya Jasco.

Mradi umekua ukisuasua kwa Madai kwamba wanashindwa kufanya Nazi ipasavyo kwa madai kuwa baadhi ya wamiliki wa majumba hawajalipwa fidia na serikali Hadi leo.pamoja na mvua za vuli kuwa kikwazo cha kuendelea na ujenzi,takriban wiki ya Pili sasa wamesimama,tunaomba manispaa ya Temeke watupe ufafanuzi ma kutatua tatizo hili.na hili naamini serikali italishughulikia ipasavyo.
 
Naam mkuu Rusende, nakuunga mkono, hakuna kinachoendelea wakazi wa maeneo hayo wamekuwa taabuni kwa muda mrefu sana ila awamu hii tukawa na matumaini makubwa ya hiyo miundo mbinu kujengwa lakini dah! barabara ilijazwa kifusi tu na ikachimbwa mitaro kiusanii lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea, huo mfereji nao ndio maumivu matupu kwani maji yanayotirirka kutoka maeneo ya charambe na maeneo ya rangi tatu yoote yanakuja maeneo ya kiburugwa na hakuna miundo mbinu yotote kwa ajili ya kupokea maji hayo.
Naiomba serikali iangalie kulikoni hii miradi? mbona inasuasua.
 
Back
Top Bottom