Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere unatumika kisiasa

rushesheka

New Member
May 13, 2021
4
2
Huu mradi wa umeme ulianza mwaka 2015 ukiwa unategemewa kutoka Kinyerezi Dar es Salaam kuelekea Tanga mpaka Arusha ukijulikana kama North East grid KV400 kufika hapo katikati kati 2016 na 2017 hiyo mipango ikasimama baada ya mabadiliko ya uongozi kutoka Awamu ya Nne kwenda Awamu ya Tano awamu ambayo haikupendezwa na umeme wa gas, ukabadirishwa mtazamo na kuelekeza nguvu kwenye umeme wa maji (Hydroelectric power).

Hapa ndipo yaliibuka mawazo ya kujenga bwawa katika mto Rufiji kwenye bonde la Steglas Gorge na baadae kuitwa mradi wa umeme wa BWAWA LA MWALIMU NYERERE.

Mradi huu ulipokelewa kwa shingo upende na wanamazingira duniani , baadae ukawa miongoni mwa mradi wa kimkakati.

Ila ukisikiliza kwa makini matamko ya viongozi wa kisiasa kuanzia Waziri mkuu,Waziri wa nishati pamoja na Naibu wake wote ahadi wanazozitoa hazina uhalisia na kazi inayoendelea.

Kwanza ni kweli ujenzi wa bwawa unaenda kwa kasi kama ilivyo kwenye ratiba ya kazi japo kuna vikwazo vidogo vidogo kama vile kuingiliwa na maji yanayo sababisha kazi kusimama kwa muda.

Wabunge wa majimbo hasa kibaha na chalinze wameuliza maswali mara kwa mara tangu mwaka 2015 kuhusu fidia ya wananchi lakini wakati wote walipewa majibu ya kutia matumaini lakini matumaini yasiyotekelezeka mpaka leo 2021, Slivester Koka Mbunge wa Kibaha juzi alipo uliza swali bungeni kuhusu fidia iliyocheleweshwa kwa muda wa miaka 6 waliendelea kutoa majibu ya kisiasa kama kawaida.

Hapa na nanukuu 'riba ni swala la kisheria kwa kuwa serikali ya CCM ni sikivu watalizingatia hilo' hapa ndio inaingia siasa. Tulitarajia kusikia jibu la waziri linasema kuwa riba imeunganishwa moja kwa moja na malipo ya fidia. Hapo tungejua kama ipo riba ama la. Miaka sita ni mingi sana toka tathimini ifanyike. Njia ya kusafirisha umeme mpaka eneo la Chalinze kuelekea Dar es salam, Dodoma na Tanga bado hawajalipa fidia kwa wakazi wanaopisha mradi huo.

Zoezi la kusafisha njia za kusafirishia umeme mkubwa wa KV400 mpaka CHAUA kituo cha kupozea umeme hapa hakuna dalili ya kitu kinachoendelea

Ukisikiliza maelezo ya Waziri mkuu wakati alipotembelea BWAWA LA MWALIMU NYERERE alitangaza kuwa kazi itamalizika kama ilivyopangwa. Ukimsikiliza Waziri mwenye dhamana amesema tarehe 15/11/2021 wataanza kuingiza maji kwenye bwawa. Kiuhalisia ilo jambo halitawezekana kwasababu kuingiza maji kwenye bwawa inabidi umeme uanze kuzalishwa kwa majaribio. Waziri ameendelea kuliambia bunge kuwa tarehe 15/6/2022, saa tisa mchana umeme utaingia kwenye gridi ya taifa hili ni siasa tu

Hii ni rahisi kusema ila si uhalisia ata kidogo. Miradi mikubwa kama hii uzinduliwa rasimi na Mkuu wa nchi na ni vizuri uwe umemalizika kwa kwa viwango na ubora wa hali ya juu na kujaribiwa vyema na kujiridhisha kwa kila hatua.

Sehemu yenye kuleta kikwazo kama nilivyosema hapo awali ni kwamba wakazi wanaopisha ujenzi wa njia kutoka Rufiji mpaka Chalinze kutoka chalinze mpaka Dar hawajafidiwa ili kupisha ujenzi wa mradi, Kumbuka tunaelekea mwezi wa sita tuchukulie ata wakianza kulipa mwezi wa sita wahathilika wana haki ya kupewa siku 90 za kisheria ili waweze kuondoka hizo sehemu.

Tuchukulie zoezi la kuhama kupisha ujenzi unachukua miezi mitatu ni mpaka mwezi wa kumi , kumbuka njia ya kusafirisha umeme bado ujenzi kuanza mpaka fidia ilipwe, hapohapo mwezi wa November 2021bwawa linajazwa maji. Hapa inakuwa umebakiza miezi sita kuingiza umeme kwenye grid ya taifa. Mpaka hapa lazima viongozi wawe wakweli

Umeme ambao utakua hauna njia ya kufika kwenye hiyo grid. Kujenga minara (towers)kuna hitajika muda wa kutosha umbali wa kilometa karibia 500 ni umbali mrefu Kifupi tuanze kuwa wakweli. Muda ni msemakweli.

Waziri Mkuu kaa na Waziri wako wa nishati na wataalamu wako wakwambie ukweli kabla. Kitendo cha kuongea na vyombo vya habari mambo yasiyo na ukweli yanafanya wananchi kuondoa imani kwenye serikali yao. Tafadhari tusiingize siasa kwenye mradi huu haya ni maisha ya watu.
 
Mungu akipenda tarehe 15/11/2021 tutaanza kujaza maji rasmi bwawa letu la mwl Nyerere.

Karibu ushudie.
 
Mungu akipenda tarehe 15/11/2021 tutaanza kujaza maji rasmi bwawa letu la mwl Nyerere.

Karibu ushudie.
Bora umetanguliza Mungu akipenda maana wanasiasa wetu hawa... Bado tuna maumivu ya Richmond baada ya maji kwenye mabwawa kupungua sababu ya ukame na mabadiliko ya tabia nchi.
 
Kila mradi serikali ya CCM unaanzisha siyo kwa ajili ya manufaa ya wananchi na kuwasaidia bali ni kwa ajili ya ufisadi wao.

Na ni hodari sana kwa hili kuanzisha mamiradi kama ya mwendo kasi, gesi nhii Stigler.

Mwendo kasi walipewa mkopo na WB 600 Billion dollars wakatumia 250 billion dollars 350 billion wamekula na ni sisi tutawalipia hilo deni yani ni mashetani yaliyokubuhu.
 
Back
Top Bottom