Mzee Sabodo alifanya makosa ya kuitangaza will yake magazetini huku akimrithisha huyo niece wake mamilioni. Hata kabla hajafa, niece anajiuliza jee ni mpaka uncle afe ndipo aanze kuishi kimilionea?. Kijana kaamua huna haja kusubiri bali kaanza kutumbua na kutanua huku bili zikienda kwa uncle ikiwa ni sehemu halali ya urithi wake!.
P
BILIONEA SABODO AFARIKI DUNIA..
Bilionea na Mchumi maarufu nchini, Mustafa Jaffer Sabodo amefariki Dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwakwe, Masaki jijini Dar es Salaam.
"Mzee amefariki leo alfajiri akiwa nyumbani. Taratibu za mazishi zinaendelea na atazikwa katika makaburi yaliyoko mtaa wa Bibi Titi Mohamedi karibu na CBE," amesema Danstan.
Marehemu Sabado alizaliwa mkoani Lindi na alikuwa akifanya biashara katika nchi za Ufaransa, India, Kenya, Sudan, Nigeria, Zimbabwe na Tanzania.
Atakumbukwa kwa mchango wake ulioanzisha Mwalimu Nyerere Foundation National Lottery alipotoa msaada wa Sh milioni 800. Alihusika katika utoaji wa misaada kadhaa iliyohusisha kilimo, ujenzi wa visima na kusaidia wenye uhitaji.
Sabodo atazikwa leo saa 4:30 usiku.
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un.
“We surely belong to Allah and to Him we shall return”
"Sisi sote ni wa Mola, na kwake tutarejea".
Paskali pia anakuaga!.
RIP Jaffar Sabodo.
P