Mponjoli Mwakalinga:- Refa bado hajamaliza mpira

Mponjoli Mwakalinga:- Refa bado hajamaliza mpira

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,678
Reaction score
167,642
Jioni katika matembezi yangu ya kunyoosha miguu kwa maana ya maziezi ; nikafika uwanja wa shule nikaanza kuangalia mpira wa miguu katika uwanja wa huo..
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana mmoja juu ya Matokeo ya mchezo.
Kwa tabasamu, alijibu "Wako mbele yetu 3 - 0 !"
Nikasema, "Kweli!
Mbona huonekani kukata tamaa..?"
"Kukata tamaa??!!"
Yule mvulana aliuliza kwa mshangao....
Kwanini nikate tamaa wakati bado refa hajapuliza kipenga cha mwisho ?
Nina imani na timu yangu na meneja wa timu ; Nina hakika tutashinda ! ! !
Na kweli, mchezo uliisha 5 - 4 timu ya kijana ikiwa mbele na kushinda ule mchezo!
Alinipungia mkono taratibu, na tabasamu zuri akiondoka uwanjani; nilishangaa, mdomo wazi, ujasiri mkuu kiasi hiki; such a high and beautiful faith;
Nilipofika nyumbani usiku ule, swali lake lilizidi kuja kwangu zaidi:
"Kwanini niogope wakati refa hajapuliza kipenga cha mwisho?"
Maisha ni kama mchezo.
Kwanini ukate tamaa wakati mwenyezi Mungu ndiye meneja wako?
Kwanini ukate tamaa wakati kungalipo uhai ndani yako?
Kwanini ukate tamaa wakati kipenga chako cha mwisho bado hakijapigwa?
Ukweli ni kwamba watu wengi hujipulizia wenyewe vipenga vyao vya mwisho.
Lakini maadamu ungalipo uhai, hakuna kisichowezekana muda haujakuacha.
Nusu kipindi si kipindi kizima na ratiba ya Mungu kwa mwanadamu si ratiba ya mwanadamu kwa Mungu.
Usijipulizie kipenga chako cha mwisho we mwenyewe.
JIPE MOYO ; USIKATE TAMAA!
KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA ; KAMWE USIKATE TAMAA.

Yupo Mungu ajuae Mwisho kabla ya Mwanzo. — at Njonjo Avenue.
 
True, hamna haja ya kukata tamaa, muda Bado unaruhusu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom