Mpo upande gani na wajibu wenu ni nini?

Mpo upande gani na wajibu wenu ni nini?

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,622
Reaction score
3,147
Wafuatao nawaomba wanipe majibu ya swali langu hapo juu baada ya maelezo yafuatayo;

Ndugu zangu, Watanzania, bila shaka kila aliye Mtanzania na anaishi hapa Nchini anajua fika hali ngumu inayowakumba wananchi kwa hivi sasa.

Bei za vitu zinapanda kila inayoitwa leo. Mbolea iliyokuwa ikinunuliwa sh.45,000/50,000 sasa inauzwa zaidi ya sh.100,000/-. Hilo ni ongezeko la bei la zaidi ya 100%. Ikumbukwe kuwa, ongezeko hilo lipo kabla kabisa kufikia msimu wa kutumia mbolea hiyo mashambani.

Hoja yangu ya msingi ni kwamba;

wakati mambo ya ovyo yanayoendelea kutamalaki Nchini, wafuatao wamekaa kimya kana kwamba hawaoni kinachoendelea Nchini.

(1) WABUNGE

Wengi wao wamechaguliwa na Wananchi kama wawakilishi wao kule Bungeni. Lakini haya mauza uza yanaendelea wao wamekaa kimya kabisa kama maji ya mtungi.

(2)WAANDISHI WA HABARI

Tunaamini vyombo vya Habari ni mhimili wa nne wa Dola.
Lakini unakuta mambo mengi ya ovyo yanaendelea Nchini wao wanabaki kimya kana kwamba hayawahusu na wala si wajibu wao kukemea.

(3) WANACHAMA WA CCM

Hawa ndio wenye Chama kinachoongoza Serikali kwa sasa. Hawa walitakiwa kuwa wa kwanza kabisa kukemea mambo ya ovyo yanayoendelea Nchini. Kinyume chake, wapo kimya kana kwamba hawaoni wala hawakii.

(4) VIONGOZI WA DINI
Kazi kubwa ya viongozi hawa si kuhubiri tu bali pia kutoa mwelekeo mzuri kwa Serikali hasa pale mambo yanapokuwa yanakwenda mrama. Hawa nao wapo kimya kana kwamba hawaoni wala na kwamba shida za wananchi si kitu kwao ili mradi tu sadaka zinapatikana.

(5) WANANCHI WOTE

Hawa nao hukaa kimya bila kuwahoji viongozi wao waliowaweka madarakani kwa njia ya kura. Huku ni kukosa kabisa uwajibikaji.
Sina maana kwamba makundi niliyoyataja hapo juu yachukue hatua kali zisizo na maslahi kwa Taifa, hapana, nina maana kwamba, kila kundi liitendee haki Nchi hii kwa kutimiza wajibu wake bila woga.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom