Mpira wa Tanzania na Uingereza Unafanana

Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
715
1,000
Jamani jamani kati ya vitu tulivyorithi kutoka kwa wakoloni wetu hawa wa mwisho ni majigambo!
Mpira wetu na wao unafanana kwa kuchezwa na mdomo. Tena bora hata wao wanajitahidi timu yao ya taifa hata inafuzu kwenye michuano ya bara lao na ya dunia. Sisi sasa, hata kufuzu ya Afrika tu imekuwa ni ndoto. Yaani mpira ungekuwa maneno aiseee tungeongoza Afrika. Yaani tungekuwa tunafukuzana na Brazil kwa mataji ya World cup! Lol
Tulikaribia kufuzu CAF ila sasa tulivyojisifu utafikiri tumeshinda kombe la dunia. Utasikia mara ooo kikosi chetu ni bora, nilimsikia mchambuzi mmoja akidiriki kusema kwa mwaka 2018 kikosi chetu ni kati ya vikosi bora Africa, wakati hata East Africa tu tupo mkiani. Ingetokea muujiza tu taifa stars wakafika robo finali CAF aiseee nchi nyingine za bara hili wangetafuta bara lao. Manake siyo kwa hayo majidai.
Ukija kwenye club ndo majanga! Hasa hasa Simba na Yanga. Tena bora hata Yanga, Simba sasa ukimchanganyia msemaji wao Haji Manara na endorsements mbali mbali za maceleb utajua bonge moja la klabu yaani kama vile Real Madrid. Utasikia wakisema mfalme wa nyika hua nachekaga mwenyewe. Mpira ungekuwa maneno aiseee Tp Mazembe wasingeona ndani kwa wekundu wa msimbazi. Lakini bora hata Simba leo imeshinda waendelee kuwakilisha taifa japo ni kwa tabu sana.
Kwa majigambo na maneno tupo vizuri aisee. Wangeanzisha tu kombe la dunia la kujitamba tusingeshindwa kamwe labda ushindani wetu ungekuwa Uingereza tu. 😂😂 Yaani huwa nikiwaza mwenywe nacheka na kufurahi kuzaliwa Mtanzania, na shuhudia mubashara kabisa maajabu ya ulimwengu huu.
Na hii sio mpirani tu hata sekta nyingine za nchi Watanzania jamani tunaongea! Ni bora tungechukua hatua zaidi katika kuboresha mpira na michezo mingine kuliko kuzungumza sana. Bora tujigambe tukiwa na cha kujigambia.
 
Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,313
2,000
Nyie mademu huwa mambo ya mpira hamyajui vizuri ungeachana nayo ufanye issues nyingine. Maana umeandika uchafu tu.
 
magnifico

JF-Expert Member
Jan 14, 2013
6,177
2,000
Hao Waingereza unaowaita Wapiga Domo.

1. Wamebeba kombe la dunia.

2. Wanashika nafasi ya pili kubeba UEFA Cl mara nyingi.

3.Europa League mara kibao.

Wewe tafuta nchi nyingine ya kufananisha na domo tunalopiga ila hapo umechemka!
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
3,698
2,000
Hao Waingereza unaowaita Wapiga Domo.

1. Wamebeba kombe la dunia.

2. Wamebeba Euro

3. Wanashika nafasi ya pili kubeba UEFA Cl mara nyingi.

4.Europa League mara kibao.

Wewe tafuta nchi nyingine ya kufananisha na domo tunalopiga ila hapo umechemka!

Waingereza hawajawhipo kubeba Euro rekebisha maneno yako.
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
3,698
2,000
Ila hayo mafanikio mengine nyie mmeyapata

Sent using Jamii Forums mobile app

Waingereza ni taifa kubwa sana ulimwenguni, Wana kila sifa, pesa, miundo mbinu vya kuwafanya wawe na mafanikio. Lakini wanakosa vipaji. Hata ufahamu wao wa Football ni mbovu sana. Bado mafanikio yao ni madogo kutokana na status ya taifa leo.

Vilabu vya kiengereza vinauwezo wa fedha za kutosha kuliko vilabu vya nchi nyingi Ulaya lakini bado wanasuasua kwenye ushindani.
 
ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
12,475

Ushindani gani
Kwa taarifa yako waingereza hawana muda kabisa na michuano ya nje ya nchi yao na ikitokea wakafanikiwa huko ni bahati tu na si mipango......wao wapo bize na michuano ya ndani tu ndio maana uwekezaji wao umelenga palepale bora wako uefa kuliko kukosa epl hayo maumivu yake sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
3,698
2,000
Ushindani gani
Kwa taarifa yako waingereza hawana muda kabisa na michuano ya nje ya nchi yao na ikitokea wakafanikiwa huko ni bahati tu na si mipango......wao wapo bize na michuano ya ndani tu ndio maana uwekezaji wao umelenga palepale bora wako uefa kuliko kukosa epl hayo maumivu yake sasa

Sent using Jamii Forums mobile app

Endelea kujidanganya.
 
Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,452
2,000
Jamani jamani kati ya vitu tulivyorithi kutoka kwa wakoloni wetu hawa wa mwisho ni majigambo!
Mpira wetu na wao unafanana kwa kuchezwa na mdomo. Tena bora hata wao wanajitahidi timu yao ya taifa hata inafuzu kwenye michuano ya bara lao na ya dunia. Sisi sasa, hata kufuzu ya Afrika tu imekuwa ni ndoto. Yaani mpira ungekuwa maneno aiseee tungeongoza Afrika. Yaani tungekuwa tunafukuzana na Brazil kwa mataji ya World cup! Lol
Tulikaribia kufuzu CAF ila sasa tulivyojisifu utafikiri tumeshinda kombe la dunia. Utasikia mara ooo kikosi chetu ni bora, nilimsikia mchambuzi mmoja akidiriki kusema kwa mwaka 2018 kikosi chetu ni kati ya vikosi bora Africa, wakati hata East Africa tu tupo mkiani. Ingetokea muujiza tu taifa stars wakafika robo finali CAF aiseee nchi nyingine za bara hili wangetafuta bara lao. Manake siyo kwa hayo majidai.
Ukija kwenye club ndo majanga! Hasa hasa Simba na Yanga. Tena bora hata Yanga, Simba sasa ukimchanganyia msemaji wao Haji Manara na endorsements mbali mbali za maceleb utajua bonge moja la klabu yaani kama vile Real Madrid. Utasikia wakisema mfalme wa nyika hua nachekaga mwenyewe. Mpira ungekuwa maneno aiseee Tp Mazembe wasingeona ndani kwa wekundu wa msimbazi. Lakini bora hata Simba leo imeshinda waendelee kuwakilisha taifa japo ni kwa tabu sana.
Kwa majigambo na maneno tupo vizuri aisee. Wangeanzisha tu kombe la dunia la kujitamba tusingeshindwa kamwe labda ushindani wetu ungekuwa Uingereza tu. 😂😂 Yaani huwa nikiwaza mwenywe nacheka na kufurahi kuzaliwa Mtanzania, na shuhudia mubashara kabisa maajabu ya ulimwengu huu.
Na hii sio mpirani tu hata sekta nyingine za nchi Watanzania jamani tunaongea! Ni bora tungechukua hatua zaidi katika kuboresha mpira na michezo mingine kuliko kuzungumza sana. Bora tujigambe tukiwa na cha kujigambia.
Vumilia.Soka siyo mchezo wa karata.Kwamba unaficha kuanzia karata hadi furaha kifuani adui asione.Soka siyo hivyo.Ni lazima umpe mshindani wako changamoto ya majigambo ili anywee ushinde.Halafu majigambo siyo dhambi.Ni sehemu ya kinogesha mchezo tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom