Amekimbia aibu ya kushindwa hana lolote
Hamkani hali si shwari ndani ya Chadema! Kansa Mohamed Mbaruku, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Tabora, amejitoa
kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa, hivyo kumfanya kwa mara nyingine Freeman Mbowe kuwa katika mashindano ya
'farasi' mmoja.
Kwa mujibu wa 'Mwananchi Breaking News', Mbaruku ameamua kujitoa kwa madai kwamba katiba ya chama hicho imekiukwa na
akasema atakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga uchaguzi huo na kuomba ufafanuzi wa kikomo cha uongozi.
Mbaruku amejitoa siku moja tu baada kabla ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake, ambao umepangwa kufanyika kesho Jumapili
Septemba 14.
Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kwamba kujitoa kwa mgombea huyo kunaweza kusababisha mpasuko ndani ya
Chadema kutokana na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi ya uongozi kwamba unaendesha chama kama 'taasisi
binafsi'.
Awali Mbaruku aliwasilisha pingamizi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, ambapo pamoja na mambo mengine, alidai
kwamba Mbowe hana sifa kikatiba ya kugombea tena nafasi hiyo.
Pia duru za siasa ndani ya chama hicho zilieleza kwamba, majina mawili yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na
Usimamizi wa Kanda katika chama hicho, Benson Kigaila, kwamba nao walijitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti, Daniel Ruvanga na
Garambenela Frank, yalikuwa majina hewa yaliyolenga kumsafishia njia Mbowe ya kubakia kuwa mgombea pekee baada ya kuenguliwa
kwa Mbarouk.
Inaelezwa kwamba, Katiba ya Chadema hairuhusu kiongozi wa nafasi hiyo kugombea vipindi zaidi ya viwili vya miaka mitano.
Aache wendawazimu , yeye amekuwa mwenyekiti wa mkoa wa tabora kwa vipindi vitatu mfululizo kwa kutumia katiba hiyohiyo halafu leo anataka itumike kwa mbowe, what a shame.
Taarifa hii ilikuwa nzuri kama taarifa,umeharibu ulipoonesha ushabiki uliposema"duru za kisiasa zinasema kujitoa kwa mbaruku kutaleta mpasuko ndani ya chadema"hapa umeweka chumvi zako labda kwakuumia kuona kapteni Mbowe anapita bila kupingwa kwakuwa anakubalika na kila mtanzania na kuwa uwezekano wa kuiua chadema ndiyo unazikwa rasmi.Unajua kabisa hakuna mpasuko wowote kwani huyo kansa hana influence yoyote katika chama na katika jamii,anachofanya ni kuigiza ili waliomtuma waone kuwa hela zao walizompa zinafanya kazi.
Nakushauri uwe unaongea ukweli acha uongo.
Chadema oyeeeeeeeeeee!!!!!!
Muislamu huyu?