Mpenzi wangu sio rafiki

Mpenzi wangu sio rafiki

Daah hiyo fursa nilikuwa naitafuta siku nyingi embu nipe namba yake kwa maana na mimi nina tabia kama yake, nadhani tutaendana nae au vipi

Mkuu sasa si mtakuwa mnatazamana tu
 
ila kwa upande mwingine hii ni tabia yake (upole) ni ngumu sana kumbadilisha aisee huenda alipitia maisha fulani ndio maana yupo hivyo

Yaaah family yake pia imechangia kuwa hivo kwa upande mmoja au mwingine
 
Mara nyingi watu wa hivyo huwa hawajui mambo mengi yanayoendelea ulimwenguni.

Mshawishi awe anasoma soma vitabu kuanzia vile vya mapenzi mpaka na hivi vya kawaida .

Ukiweza kumfanya ajue mambo mengi akikaa na wewe hatokosa cha kuzungumza.

Pia inaonesha bado hajakuzoea anahisi akiongea kama ataongea pumba vile kwa hiyo anaona suluhisho pekee ni kukaa kimya.

Words, nashukuru kwa ushauri wako mkuu
 
Kuwa na mpenzi wa aina hiyo ni unaboreka kweli kweli. But jitahidi tu,since she is loyal lakini Nina wasiwasi italeta Shida some other days

Mkuu sio inaweza kuleta, ishaleta shida mara kibao yani watoto wamjini wenyewe wanakwambia yashanifika hapaa, na huyu mpenzi mtazamaji wangu.
 
Kutokujua mambo mengi ndiko kunakomfanya kutokuwa mzungumzaji.

Angekuwa anajua vitu asingekuwa mvivu kuchangia.

Kwa hiyo suluhisho pekee kwa huyo msichana ni kumfanya ajue vitu na mambo mengi yanayoendelea hapa ulimwenguni .
Czan kama unachosema ni kweli iyo ni haiba ya mtu tu aijalishi anajua vitu vingi au ajui.
 
Pole sana mkuu...kaa utafakari vizuri na utapata jibu la kupuuza huo msimamo wako..hakuna binaadam asiye na kasoro huu ndo ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app

Lakini sasa mkuu kwa namna hiyo itawezekana kweli kufikia relationship goals, unajua mbaka inafikia kipindi mtu unafurahi kukaa na msichana ambae sio wako kuliko wako ni hatari hii.
 
Umejaribu kumchunguza akiwa na watu wengine na wewe haupo? Bado ni mkimya?

Huyu msichana bwana kutokana na malezi na maisha aliyopitia hakuweza kuchangamana sana na watoto wakiume (wanaume) kwahiyo bora mimi kuliko hao wanaume waliokuwa wakimzunguka kuanzia chuo mbaka kwenye mishughuliko yake ndo hanaga habari nao kabisa, kwa upande wa wasichana wenzake nikiwauliza wanasema wakiwa pamoja ni talkative..,sasa nashindwa kuelewa hapo
 
Back
Top Bottom