Mpenzi wangu ni mjamzito amekutwa ana Ectopic Pregnancy

tawa driller

JF-Expert Member
Dec 11, 2015
296
152
Habari wana jukwaa natumai hapa ni eneo husika kabisa kwa hili tatizo lililomkuta mpenzi wangu.

Mpenzi wangu ana ujauzito wa miezi minne na jana ndio alianza kwenda kliniki. Lakini baada ta vipimo daktari akamwambia kuwa mimba imetunga nje ya mfuko kwa hiyo ni ectopic.

Kwa sababu hiyo akamshauri hiyo mimba itolewe kwa kulinda afya yake au kama anataka kuendelea kukaa nayo basi atatakiwa kutokufanya kazi ngumu ngumu. Kwa maelezo ya daktari ni kuwa kwenye hiyo mimba lolote linaweza kutokea.

Sasa basi kilichonileta kwenye hili jukwaa ni kutaka kujuwa je Ectopic Pregnancy ina uwezo wa kukua hadi kufikia miezi minne (16 weeks)?

Je, Ultra sound inaweza kukosea kutoa majibu au daktari anaweza kukosea kuyasoma majibu ya ultra sound?

Je, nini kifanyike kutokana na situation ya huyo mpenzi wangu?
 
Mi najua ectopic pregnancy inaambatana na maumivu makali sana maana mtoto anakuwa nje ya kizazi, je mmeenda hospital nyingine.?
Hatujaenda hospitali nyingine ila tunampango wa kwenda Sinza Palestina pale juma tatu akafanye tena Ultrasound ili tushabihishe majibu ya hospitali hizo mbili.. maumivu aliyokuwa anayapata ni ya kawaida tu kama mama mjamzito mwingine yeyote anayapata na sio ya kukaa muda mrefu ni maumivu ya siku mbili tatu hadi nne yanakuwa yanapotea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuwa anapata hedhi mkuu... Sema tutajaribu kwenda hospitali nyingine kwa uchunguzi zaidi
Kama mimba imetungwa nje lazima mwanamke alikuwa anapata hedhi kila mwezi kama kawaida je hali hiyo mkeo alikuwa nayo?

Kama hakuwa nayo jaribu kwenda kupima sehemu nyingine muda mwingine ultrasound zinatoa majibu tofauti kulingana na msomaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dalili ambazo yeye alikuwa ananambia ni kuwa kuna kipindi mguu ulikuwa una kaza hadi anashidwa kusimama inambidi akae kwa muda kidogo ndio unaachia ila hiyo hali ikaja ikapotea pia akawa anapata maumivu ya mgongo hadi kiunoni lakini hiyo hali pia nayo ikaja ikapotea akawa anatapika sana ila hiyo hali nayo ikapotea pia kuna kipindi akawa anatoka na vijidamu ukeni sio damu nyingi ila pia hiyo hali nayo ikapotea ndio mpaka kufikia juzi akaenda kliniki ndio akaambiwa hivyo
ana dalili gani ya hatari iliyoambatana na ujauzito huo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dalili ambazo yeye alikuwa ananambia ni kuwa kuna kipindi mguu ulikuwa una kaza hadi anashidwa kusimama inambidi akae kwa muda kidogo ndio unaachia ila hiyo hali ikaja ikapotea pia akawa anapata maumivu ya mgongo hadi kiunoni lakini hiyo hali pia nayo ikaja ikapotea akawa anatapika sana ila hiyo hali nayo ikapotea pia kuna kipindi akawa anatoka na vijidamu ukeni sio damu nyingi ila pia hiyo hali nayo ikapotea ndio mpaka kufikia juzi akaenda kliniki ndio akaambiwa hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
pole,wakati anatokwa na damu ujauzito ulikua na umri gani na pia utokaji huo wa damu uliambatana na maumivu yoyote?
 
Back
Top Bottom