pakapori
JF-Expert Member
- Sep 13, 2015
- 536
- 622
Habari ya muda huu wakuu
Katika miezi kadhaa iliopita nilitokea kuumizwa na msichana niliempenda sana, alinicheat katika mazingira ambayo kila nikiyafikiria huwa yananiumiza sana maana sikuwahi kumkosea na hata nikimkosea tulikua tunaelezana na kusameheana na maisha kuendelea.
Sio siri kupenda ni uchizi asee maana alinicheat mara ya kwanza ilitokea nikafaham nikasamehe yakaisha but kibaya zaidi akaja kurudia kwa mara nyingine, tuligombana sana ila mwisho wa siku nilimsamehe tena.
Simtetei ila kwa sasa kiukweli amebadilika na kuwa mwenye mapenzi ya dhati.
Kinachoniumiza ni ile situation ya kunicheat mara 2 na wanaume wawili tofauti ndio imebaki katika kumbukumbu kichwani mwangu, kila nikikumbuka alivyokua akiniaga kwa kunidanganya kumbe anaenda kwa mwanaume mwingine huwa nachukia sana maana ukiangalia kwa upande wangu toka nimekuwa nae sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine.
Kumpenda nampenda ila nikikumbuka alichonifanyia huwa nachukia sana na kukosa raha. Natamani ningeweza kusahau lakini nashindwa kwakuwa nilimwamini sana sana..,