Mpenzi wangu Hataki NIOGE nk nk!!...!

Mpenzi wangu Hataki NIOGE nk nk!!...!

Rapherl

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Posts
3,504
Reaction score
2,256
Wakuu salaam,

Naomba ushauri wenu hapa kwenye hili jambo linalonitatiza sana kwa sasa.

Niko kwenye uhusiano na huyu Malkia wangu kwa muda wa miaka sita sasa anaujauzito,lakini toka amekuwa katika hali hiyo Nyumba imekuwa chungu kwangu...
1.Hataki nioge yaani nikirudi kazini suala la kuoga halipo kwahiyo mm huwa inabidi nikienda kazini asubuhi nioge huko huko,anasema kwamba anataka asikie harufu yangu kwahyo huwa analalaga karibu na kwapani ili asikiwe tu ile harufu...
2.Siku nyingine nikirudi Nyumbani nafukuzwa hataki kuniona bila sababu muda mwingine huniambia "nanuka" pafyumu sasa yeye hataki hiyo harufu hata kama sijajipulizia hii huwa inaniuma sana kwasababu huyu huwa ni zaidi ya mpenziu wangu ni RAFIKI yangu mkubwa...
Sasa akinifukuza nikitoka haitapita nusu saa ananipigia simu nirudi Nyumbani kwanini namucha peke yake?!anadai siku hizi simpendi
3.Kuhusu Chakula
Juzi kaniambia anahamu ya Kuku tumetoka kwenda barabarani tumenunua kuku tumefika Nyumbani nampikia Kuku anasema Yeye anataka Miguu tu!na Kuku mwenyewe hajala kala kamguu kamoja na hakukamaliza...hicho ni kisa kimoja tu vipo vingi!
Wakuu,

Yapo mengi yananiumiza sana hasa muda mwingi nashindwa kuwa nae kutokana na Ugomvi mara kwa mara japo nimejitahidi kuvumilia,kuna wakati natamani hata arudi kwao ila sasa hawezi kukubali kuondoka na mimi siwezi kuvumilia awe mbali nitakosa mtu wa kuongea nae ye ndo Rafiki yangu mkubwa(mimi sina Marafiki sana hili ni tatizo ambalo nalitafutia ufumbuzi)

Naomba mnisaidie ushauri hapa nifanye nini sasa ili niweze kuishi nae kwa Amani?ndo itakuwa hivi hivi mpaka miezi tisa itimie au itafika kipindi ataacha?

Samahani kwa maneno mengi ni Pressure tu inanisumbua.Asante

Sent from BlackBerry
 
Pole mkuu, ndo ujauzito huo mzee, hormonal changes zinafanya kazi yake.
But all is just temporary, na atarudi kawaida akijifungua.
Kila la kheri.
 
Usipandwe na pressure ndugu yangu...ndio kukua huko.Mkulima akipanda mazao shambani anategemea nyasi za aina zote kuota na kuzipalilia ikiwepo sangari...Nakuombea kwa Mungu akupe uvumilivu,zaidi ya hapo sina ushauri mwenzako. Wapo wenzako ambao wake zao wakiwa kwenye khali hiyo wanamtamani babamkwe. Si jui wewe ungesenaje baba yako akitamaniwa na mkeo kila saa anamtaja na kutaka kuongea nae kwenye simu kama vile boyfriend wake.😛ray2:
 
Mkuu,
Huwa akinitimua home au tukigombana anampigia simu Rafiki yetu sote tukifahamiana toka naanza nae uhusiano huyo ndio huwa anamuelewa na kumtuliza watapiga story na kutaniana mpaka hasira ziishe ndo kidogo maelewano yanapatikana...jamaa asipokuwepo napata shida sana
Bob Lee Swagger

Unataka kuniambia atakuwa hivyo mpaka anajifungua?!si nitaisha?!
 
Last edited by a moderator:
Ndio raha ya kulea tumbo changa hiyo.... nenda kacheze pool table hatakama hujui kajifunze funze inavuta muda kdg... anyway ndio ukubwa huo
 
Mkuu,
Huwa akinitimua home au tukigombana anampigia simu Rafiki yetu sote tukifahamiana toka naanza nae uhusiano huyo ndio huwa anamuelewa na kumtuliza watapiga story na kutaniana mpaka hasira ziishe ndo kidogo maelewano yanapatikana...jamaa asipokuwepo napata shida sana
Bob Lee Swagger

Unataka kuniambia atakuwa hivyo mpaka anajifungua?!si nitaisha?!
Usikate tamaa yote hayo yana mwisho wake. Na akija kupata mimba nyingine kutakuwa na mabadiliko,waweza shangaa akataka hata usiende kazini ukae nae tuuu ukilishika shika tumbo na wengine wanataka uendelee kufanya nae tendo hadi siku ya kwenda kujifungua.
 
Pole mkuu!kila jambo na swaga zake.
usijali, ndani ya miezi tisa tatizo litaisha.
Staili hii ya kula miguu ya kuku nayo kiboko!!!!!!!!!!!!!
 
Hongera kwa kuwa baba mtarajiwa...habari njema huyu wa kwako hana matatizo ungepewa wa kwangu kipindi kama hiki wiki ingekushinda kumaliza.....Ni hali ya kawaida kabisa kwa wajawazito na tena usidharau hata hatua moja kwani kwa kufanya hivyo utamfanya mwanao akose mapenzi ya baba tangu tumboni....Wewe umeachiwa kuku unalalama..kula kaka wengine hata mguu hatupewi tehe tehe teheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Vumilia, akijifungua yataisha. Huwa yanawatokea baadhi ya wadada/wamama wakiwa wajawazito.

Pole
 
Vumilia, akijifungua yataisha. Huwa yanawatokea baadhi ya wadada/wamama wakiwa wajawazito.

Pole
huyo wa kwake anajifanyisha tu hamnaga kitu kama hicho!!kasikia tu kijiweni na saloon basi anaaply hebu mkaripie uone asipofyata mkia wake atakuchoma na kisu useme ni miiiimba hiyoooo.hata tembo anabeba yake 2years na hana mbwembwe
 
sasa utasimulia nini baadaye????
It is worthy it, so enjoy the rare and special moment. jifunze kuona positive things ndani ya mabaya!

Kweli Mkuu,
Na hii ndio sababu nyingine inayonifanya niendelee kuvumilia namuona ni yeye ila katika sura tofauti kabisa huwa na cheka sasa nikicheka na yeye kakasirika ni ugomvi pia...anasema namdharau!

Mkuu navumilia ila ni Kaazii!
 
huyo wa kwake anajifanyisha tu hamnaga kitu kama hicho!!kasikia tu kijiweni na saloon basi anaaply hebu mkaripie uone asipofyata mkia wake atakuchoma na kisu useme ni miiiimba hiyoooo.hata tembo anabeba yake 2years na hana mbwembwe

Nivea ,

Nimecheka sana,ngoja nijaribu kumtishia leo niona kesho nitakupa jibu.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom