Mpenzi wangu anatongozwa sana!

Habari wakuu, bila kuchelewa niende kwenye tatizo ninalopata.

Nina mpenzi wangu, tuna mwaka na nusu kwenye uhusiano wetu. Tumekutana katika chuo kikubwa jiji la mtoto wa kolomije, wote tukiongeza elimu ya juu.
Ananipenda sana,ukizingatia Mimi ndio niliyembikili (ni nadra sana kukutana na binti bikra chuoni). Mtoto ni mchanganyiko wa kinyarwanda na kisukuma, kwa ufupi amekamilika kila idara.

Tatizo nalikutana nalo anatongozwa sana yaani mpaka kero, kila wiki lazima aje anieleze, mara flani ananisumbua mara kunajamaa kanisani ananisumbua,wengine nawajua wengine siwajui. Mara nyingi namshauri awajibu vibaya lakini naona wanaendelea tuu.

Naomba ushauri wakuu,nataka kupata mbinu za kijasusi kuwaadabisha wote wanaosumbua kipenzi changu.
Angalizo nimepanga kumuoa mwaka 2019 kama mungu akipenda.

Nawasilisha wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una uhakika wewe hukumtongoza ndipo ukampata?
 
Muongo huyooo usikute hata kutongozwa hatongozwi anaowakubalia na wanaomkula mbona hakwambiii na we unaona unapendwaa kumbe anakujaza
 
Hebu tupia picha yake na namba tuzidi kuwashauri vizuri, binafsi ntaiwekea mkono na kuifanyia maombi akatae wote wanaokusumbueni kwenye huba lenu.

Wako Askofu Gwamajimaji
 
Habari wakuu, bila kuchelewa niende kwenye tatizo ninalopata.

Nina mpenzi wangu, tuna mwaka na nusu kwenye uhusiano wetu. Tumekutana katika chuo kikubwa jiji la mtoto wa kolomije, wote tukiongeza elimu ya juu.
Ananipenda sana,ukizingatia Mimi ndio niliyembikili (ni nadra sana kukutana na binti bikra chuoni). Mtoto ni mchanganyiko wa kinyarwanda na kisukuma, kwa ufupi amekamilika kila idara.

Tatizo nalikutana nalo anatongozwa sana yaani mpaka kero, kila wiki lazima aje anieleze, mara flani ananisumbua mara kunajamaa kanisani ananisumbua,wengine nawajua wengine siwajui. Mara nyingi namshauri awajibu vibaya lakini naona wanaendelea tuu.

Naomba ushauri wakuu,nataka kupata mbinu za kijasusi kuwaadabisha wote wanaosumbua kipenzi changu.
Angalizo nimepanga kumuoa mwaka 2019 kama mungu akipenda.

Nawasilisha wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
ni vyema umwambie aseme na roho yake hapo mtadumu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mkao wake ndo unamfanya atongozwe hovyo! Huenda anavaa mavazi ya kimitego (ya uchi uchi) !
 
Back
Top Bottom