Msandawe Halisi
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 647
- 351
Duh. Pole. Inaelekea kuna tendo au mambo fulani maalum ulikuwa unapata ndiyo maana hugeuzi. Na hata kama ni mtundu na 'unawajua' wanawake lakini kuna kitu flani maalum ulipewa au ulikula sasa wataka vunja sahani kwa uroho. Binafsi sikulaumu sababu sijui ulichopewa ukazimika. Nachoweza kukushauri jipe muda. Utasahau.
Wajamani nitakufa. Siku ya alhamisi nimemfumania mpenzi wangu kwa mara ya tatu. Mara mbili nilizo mfumania nilimsamehe. Mara ya tatu nikaona isiwe tabu, mkunguru shetani afugiki. Kwa bahati nzuri siku ya ijumaa nikawa nimesoma hapa MMU kuwa kazi ya moyo ni kusukuma damu siyo kupenda, nikamuacha mpenzi na kashifa juu. Kufika usiku siku ya ijumaa usingizi sikupata, jumamosi moyo uliniuma nahisi damu ilikuwa imepunguza mwendo. Jumapili yote jana nikawa bedrest moyo, akili vimepoteza mwelekeo. Leo kazini kazi sikufanya. Jamani mtoto wa kirangi ananifanya chizi. Nimemtumia sms ya kurudisha majeshi leo, nimekoga matusi.

Nihamia whatsaap huku siko.
Mkuu asante but kupenda kubaya sana. Agrrii!!Pole sana mkuu..
Mimi naamini kuwa kila kitu ni process, lazima kipitie hatua kidogo kidogo mpaka kuja kuwa kitu fulani.
Unapoamua kuachana na mpenzi wako papo kwa papo lazima utadhurika tuu ukweli nakwambia!
Jambo la msingi ambalo ungefanya ni kujaribu kukata kamba mdogo mdogo sio ghafla kiasi hicho.. ungepunguza maumivu!
By the way, nikupe pole... Jaribu kutafuta mazingira ya kuwa wewe pekee, maeneo yenye hewa nyingi..
Piga kelele kwa sauti kubwa sana, sauti ambayo itaondoa maumivu... rudia kadiri unavyoweza...
Rudia zoezi angalau mara 2 ama 3, kunywa maji.. hapo mzunguko wa damu utarudi kwenye kiwango chake..
vipo vya kushea, lakini sio mapenzi!