Mpenzi wangu ana harufu mbaya mdomoni, nitumie njia gani kumwambia?

saidjamali

Member
Dec 3, 2016
66
22
Habari mkuu poleni na majukumu
Nipo katika mahusiano karibu miaka 2 na mrembo flan hivi kwa kipindi chote hicho nimekuwa nikiteseka na harufu ya mdomo pindi tu mnapokuwa katika mambo yetu.. Na nimejaribu kuonesha ishara zote pengine aelewe tatizo lake imeshindwa.

Nikiangalia binti ni mzuri sana tena sana ila tu najikaza kutokana na yeye alivyojiweka kwangu. Ni pole sana and sikumbuki lini alinikosea ila tu nitaanzaje kumwambia kuhusu tatizo lake?
 
Nadhani utumie njia ya mazungumzo tu...ukae nae chini umuelezee kwa upole tu na jinsi ya kumsaidia....Unavyoongea nae usimkatishe tamaa au kauli ya kumtenga/kumdharau usiwe nayo...Ongea nae vizuri tu na ikibidi uende ukamtafutie tiba au muende wote
 
Hata wewe ni tatizo na kikwazo
Umeona hali inakukera tafuta ufumbuzi wa tatizo nunua dawa mpe uone kama hata badilika
 
mwambie wazi sio kufichana natumai itakuwa aibu kwake lakin atakuelewa na mtafute suluhisho sizan kma na yy ataendelea kupenda hiko kitu

@nihayo tu
 
Kwa miaka 2 yote unavumilia tuu kwann hukumwambia mapema!? Inaweza kukugharimu kwasababu anaweza kufikiri umemchoka unamtafutia sababu ndio maana leo unamwambia ananuka mdomo kumbe ww ulikuwa unavumilia na leo uvumilivu huo umekushinda na huna namna tena,.but anyway; mwambie kwa upole,unyenyekevu na upendo wa hali ya juu ili asifikiri vibaya.

Pole.
 
Mi naona ucmwambie.. Angalia chanzo ni nn.. Kama hapigi mswaki jaribu kumhimiza.. Pia mfanye ajali usafi wa kinywa tumia njia za kistaarabu ila ucmwambie kua unakereka coz hawa viumbe anaweza kukujia juu ukaleta uzi kua mmeachana kisa harufu ya mdomo... Ikishndkana hapo zungumza nae kistaarabu kama ulvokua ukimtongoza.. Na muoneshe u care about her...

Ni mawazo yangu tu
 
Kwa miaka 2 yote unavumilia tuu kwann hukumwambia mapema!? Inaweza kukugharimu kwasababu anaweza kufikiri umemchoka unamtafutia sababu ndio maana leo unamwambia ananuka mdomo kumbe ww ulikuwa unavumilia na leo uvumilivu huo umekushinda na huna namna tena,.but anyway; mwambie kwa upole,unyenyekevu na upendo wa hali ya juu ili asifikiri vibaya.

Pole.
Kwa miaka hiyo yote nimekuwa mvivu sana hasa swala la romance so nikawa nafanya kama mambo ya wazungu kuiga sipendi lakini najua tatizo ni nini sema tu itakuwa aibu kwake na mimi pia anaeza sema nimemchoka kwa kumwambia kuwa yuko hivyo
 
Back
Top Bottom