Mpenzi wangu amebadilika ghafla

Mpenzi wangu amebadilika ghafla

Amekuta kwako ndivosivo

Au

Huna uwezo na tendo.

He anataka akujibu live?

Bora alibp kimya tusije kukupoteza bure
Maana umekutana na MTU ambae amekuzidi kete kwa mengi.
 
Moja kwa moja kwenye mada!!

Mimi na mpenzi wangu tuna miezi mitano sasa!!
Mimi na yeye tunaishi mikoa tofauti!!

Tulikutana Dar, nikiwa nafuatilia mishemishe flani hivi, na yeye huko ndio kwao, ila kwa sasa yupo mkoa mwingine!!

Kwa kweli baada ya kuonana, nilimuelewa sana, hata yeye alinipenda mno. Mpaka tukafikia stage ya kutambulishana kwa watu wetu wa karibu. Binafsi niliamini hapo mke nishapata!!

Nikaanza kumshirikisha mipango ya jinsi ya kufanikisha kuishi pamoja, yaani kurasimishwa kama mke na mume!!

Nilimuambia, ngoja nijipange vizuri, ili mwezi wa kumi nambili katikati, nikajitambulishe kwao!! Alifurahi sana!!

Sasa, katikati hapo, alinitembelea huku nilipo, na alifurahi sana kwa jinsi nilivompokea, na nilimkarimu kwelikweli, kama wife to be!!

Mara baada ya kurudi kwao, kwa kweli amebadilika sana!! Ana hasira, na gubu balaa!!

Yaani anaweza asinitafute hata wiki nzima, na nikimtafuta anajibu kwa ukali, na kwa kifupi sana!! Naweza tuma text whatsapp, na asijibu au akajibu kwa kuchelewa sana, tena shortcut!!
Na sasa ana mtindo, nikimpigia, tukiongea kidogo tu ananikatia simu!! Kwa kweli kitendo hicho kinanikera sana, na ninahisi ananidharau mno!!

Kwa kweli sielewi ni kipi kinachoendelea upande wake!!

Nilijaribu kumpigia tuzungumze, lakini alikuwa mkali balaa, na eti hataki kuzungumzia mambo hayo!! Akakata simu!!

Jamani hebu naombeni mnishauri, au mwenzangu atakuwa huko ashapata mwingine!!

Sio kwamba siwezi, lakini sikutaka kabisa kuachana naye kwa kuwa, sikutaka tena kutafuta mwanamke mwingine wa kuona, kwa sababu kwangu hiyo ni kazi kubwa sana!!

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu!!
Nakuuliza ulifanya nae mapenzi?
 
Mkuu pole sana! Kwa hakika huyo si wako tena!,
Inaonekana kabla hajaja kwako tayari alikuwa na mwingine ambaye alishamfanyia interview, kwa hiyo huenda alikuja kwako ili kuwapima kimo! Sasa imeonekana alichokuta kwako sicho alichokuwa anakitemea!
Hivyo umeshafeli katika vigezo vyake, hivyo funguo kampa mshindani wako!
Hapo shika time zako, chuna kimtindo anza upya kivingine nina hakika utampata tu wa ndoto zako, vinginevyo utaendelea kujitesa na kujiumiza bure!
 
Ahahahah.pole sana kijana

Ila, Hiv mawazo ya kuoana mnayatoaga wapi ndugu mapema namna hiy wakat hamna hata atleast 2 years pamoja?!

Mimi mawazo ya kumuoa angalau yalikuja kwa mbaaaaaali baada ya SENDOFF yake ndio nikashtuka aallahhhh!!!kumbe huyu ndio mke mtarajiwa!! ?? Basi ndio hapo mawazo ya kuoa nilipoyapata.
But before, walaah!!yan mpaka tumeanza vikao vya harus ila mm hata hayo mawazo ya kuoana sina.😁
 
Mkuu pole sana! Kwa hakika huyo si wako tena!,
Inaonekana kabla hajaja kwako tayari alikuwa na mwingine ambaye alishamfanyia interview, kwa hiyo huenda alikuja kwako ili kuwapima kimo! Sasa imeonekana alichokuta kwako sicho alichokuwa anakitemea!
Hivyo umeshafeli katika vigezo vyake, hivyo funguo kampa mshindani wako!
Hapo shika time zako, chuna kimtindo anza upya kivingine nina hakika utampata tu wa ndoto zako, vinginevyo utaendelea kujitesa na kujiumiza bure!
Asante sana ndugu yangu, nakushukuru kwa ushauri wako!!
 
Ahahahah.pole sana kijana

Ila, Hiv mawazo ya kuoana mnayatoaga wapi ndugu mapema namna hiy wakat hamna hata atleast 2 years pamoja?!

Mimi mawazo ya kumuoa angalau yalikuja kwa mbaaaaaali baada ya SENDOFF yake ndio nikashtuka aallahhhh!!!kumbe huyu ndio mke mtarajiwa!! ?? Basi ndio hapo mawazo ya kuoa nilipoyapata.
But before, walaah!!yan mpaka tumeanza vikao vya harus ila mm hata hayo mawazo ya kuoana sina.
Khaaa!!! We noma sana kakaa!! Hahaa!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom