Mpenzi wangu ameathirika, je nimeambukizwa?

Mpenzi wangu ameathirika, je nimeambukizwa?

MFALME WETU

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2021
Posts
4,735
Reaction score
11,344
Huyu Mwanamke alikua ni Ex wangu wa muda tu, ndo mpenzi wangu wa kwanza kipindi naanza chuo 2019, tupo mwaka mmoja wote.

Sikupata tabu sana kumpata maana alianza kuonesha dalili za kunipenda mwenyewe nikaona isiwe tabu japo tayari alikua na mchumba huko alikotoka na walishatambulishana kwa wazazi na pete ya uchumba pia alishavalishwa ila alikua anaitunza kwenye pochi, niliona sio tabu maana yupo mbali so hatokuwa na effect kwenye mapenzi yetu afu ukilinganisha ni pisi ya kwenda na alikua na vishawishi na mitego ambayo mwanaume yoyote kama angeweza kuiruka basi angeonekana kama sio rijali kwenye jamii.

Zaidi zaidi nilimkuta na bikra, kumbe Huyo Mchumba wake alimwambia wasishiriki tendo la ndoa mpaka watapofunga ndoa rasmi kanisani.

Huyo mchumba wake alikua ni Manager wa Hotel fulan kubwa pale Dar hivyo pesa kwetu haikuwa tatizo maana tulikua tukiishiwa hela anapiga tu simu moja muamala unathibitishwa on the spot.

Tuliachana kwa sababu alitaka kushika Mimba yangu namimi sikuwa tayari by the time so nikaona isiwe tabu nikaamua kumpiga chini though tulikua tunapendana sana maana tulikua tunaspend 24hrs tukiwa pamoja
(tulikua tunakaa room moja mpaka first year ilivoisha, ila tulivoanza second year nilitafuta room paspo kumwambia na nikawa sirespond calls wala texts zake)

Juzi tulivoanza mitihani ya chuo ya kumaliza second semester Mwaka wa Pili akaanza kunisumbua kuwa mara amenimiss, mara anataka tusome wote amemiss nimfundishe kama nilivokua namfundisha zamani, mara kamiss show, basi nikasema isiwe tabu nikamwambia njoo kwangu [maana mpenzi wangu wa sasa anasoma chuo kingine so sikuona kama kuna shida,]

Ila kuhusu kurudiana asahau kabisa na aondoe akilini maana sahv nina mtu mwingine ila akakataa akasema yupo tayari kudate na mm hata kama nina mtu mwingine, nikamwambia poa ila iwe siri na asijethubutu kufanya interference yoyote.

So nilimkubalia japo kishingo upande sababu ni mwanamke ambae tulikua tunapendana sana way back, Naweza sema ndo ilikua couple bora ambayo watu walikuwa wana admire in the entire class.

Sasa basi,
Alikuja akastay kwangu kama Kawaida mpaka tulivomaliza mitihani na still akaendelea kukaa for almost two weeks kabla ya kwenda likizo, huku tukibinjuka usiku kucha.

Matatizo yanaanza.

Siku ya kwanza tu kaja tupo katkat ya game akaanza kunambia yupo kwenye siku zake sikumwongelesha zaidi tu tulipomaliza game nkamwambia kesho ameze P2 maana ninazo ndani akasema Hawezi, nikamwambia sawa hamna tatizo ila incase akishika Mimba tuitoe akakubali.

Sasa Juzi usiku akanipigia simu akanambia kuwa anajiskia vibaya as if yupo pregnant, nikamwambia akanunue kipimo tuhakikishe. Jana akanunua kipimo akanitumia majibu ya kipimo nkakuta kweli ana Mimba ila sikumjibu chochote mpaka sahv

Cha kusikitisha zaidi ni hiki nlichokikuta kwenye kabati leo ndo kmenisukuma kuandika huu uzi, it seems alisahau. Sijui ndo ntakua nmeukwaa au la...!!

My Take:
TRUST NO BODY



moja1.png
 
Dah! Inaonyesha huyo ni mhudhuriaji mzuri wa kliniki.

Pole sana kaka.

Ila huwezi kusema ni tayari na wewe umewaka mpaka ukapime.

Inawezekana ukawa umechomoka vile vile.

Fanya ukapime mkuu.
Asante kwa kunitia moyo kaka
Ngoja nisubiri muda ufike nikapime kujiridhisha
 
Maskiniiii pole sana. Na ukimwi ulivyokaa kimya utadhani haupo.

Kama nakuona hiyo hofu uliyonayo sasa?
Usiji'stress, nenda kapime. Ukimwi sio mafua kwamba ukikaa na mwenye mafua tu kuna possibility ya kuyapata.
 
Maskiniiii pole sana. Na ukimwi ulivyokaa kimya utadhani haupo.

Kama nakuona hiyo hofu uliyonayo sasa?
Usiji'stress, nenda kapime. Ukimwi sio mafua kwamba ukikaa na mwenye mafua tu kuna possibility ya kuyapata.
Asante kwa ushauri dada
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom