Nje huko tukawa tunatafuta sehemu nzuri ya kupata chakula na angalau kuvuta muda ili angalau mpaka saa 4 usiku turudi hotelini kwetu kulala. Tukabahatisha mgahawa mmoja. Tukaingia na kuomba huduma ya chakula. Tukaanza kupata chakula huku tunazungumzia safari yetu kwa maana ya tathimini mpaka hapa tulipofikia na yaliojiri ndani ya safari.
Mara ghafla Milgo huyu hapa! Milgo mbele, Fatma nyuma.
Waione wote wakiwemo:
chiko18 NYANYADO Aristidi selestin Milugwi Heaven Sent icca peterchoka Gobe loveissweet miss nuru Ngosha ze Dong Lee Cho in whitedoug3 pius manasse vesta bertha micheal HARUFU HALELUYA MOSHI Pritty wa joseph
Sehemu ya Tatu:
Nje huko tukawa tunatafuta sehemu nzuri ya kupata chakula na angalau kuvuta muda ili angalau mpaka saa 4 usiku turudi hotelini kwetu kulala. Tukabahatisha mgahawa mmoja. Tukaingia na kuomba huduma ya chakula. Tukaanza kupata chakula huku tunazungumzia safari yetu kwa maana ya tathimini mpaka hapa tulipofikia na yaliojiri ndani ya safari.
Mara ghafla Milgo huyu hapa! Milgo mbele, Fatma nyuma. Namna ambavyo mimi na John tulikaa katika ile meza, ni ule mtindo wa kutizamana, wakati Milgo na Fatma wakiingia, mimi ndio niliokuwa nikiwatazama, John alikuwa amewapa mgongo.
John hakuonyesha kushtushwa na kitendo changu cha kuhamisha macho, kuhamishia uelekeo wa mlangoni, walikokuwa wanaingilia wateja, wakati mimi nikishuhudia kitu ambacho kama siamini, John alikuwa amenikazia macho mimi.
Kichwani nilikuwa nawaza vitu vingi sana kuhusiana na mabinti hawa. Kubwa zaidi ni kuwa kulikoni na haka kagiza, mabinti bado hawajapata pa kulala, ama? Kingine niliwaza, labda ni ndoto ya alinacha, huenda natafutwa kwa minajili, Milgo ameshabadili uamuzi wake na yuko tayari kulala na mimi usiku huu wa kwanza, pengine labda baada ya kujadiliana na nduguye na hatimaye wakafikia consensus, au labda kimenuka, wanakuja kuniuzia kesi!
Yote kwa yote, sikuishiwa mawazo kichwani mwangu kwa tukio lile mpaka pale John aliponishtua. Na wakati nashtuliwa na John, tayari Milgo na Fatma walikuwa hawa hapa!
Wote wawili walionyesha furaha yao baada ya kutuona sisi pale, tukipata chakula kwa umoja wetu. Wakatusalimia na kutufahamisha kuwa wamefanikiwa kukutana na wenyeji wao, ambao ni wasomali wenzao, wakazi wa Tunduma, na kwamba hata hapo Hotelini wameongozana nao, ila wamebaki nje. Milgo akanifahamisha kuwa wapo katika kutafuta vitafunwa ili wakapate chai huko watakapoenda kulala.
Kama mwanaume, tena mwenye tamaa na vitu vizuri, pale pale nikakosa amani, nikajawa na inda, maumivu ya moyo yakaibuka, nikaumia sana ndani, kichwa kikawa kizito. Kisa ni WIVU. Wivu wa mapenzi.
Sikufurahia taarifa ile ya Milgo hata kidogo. Nafsi ikashindwa kuhimili mikikimikiki ya wivu, sura ikakubali kupokea kile kinapita moyoni mwangu. Uso ukajawa na huzuni. Nikashindwa kuficha hisia zangu, maumivu. Macho yakabadilika rangi.
Mawazo.
Nikaanza kuwaza kuwa kuna mtu atajilia vyake kiulaini, tena anajilia kiulaini mzigo bint ambae nimekuwa nae kutwa nzima ya leo, sio tu kuwa nae, bali pia ukweli kwamba nimejimilikisha bint baada ya yeye mwenyewe kuonyesha nia ya kumilikiwa na MSAFIRI QAFIRI!
Nikawaza ule uzuri wa Milgo. Nikawaza alivokuwa ananikumbatia. Kwa kifupi picha zote za akilini kati yangu mimi na Milgo, za kutwa nzima zikaanza kunijia akilini, mithili ya mtu ninaeota vile, ikaja na ile picha ya pale kitandani wakati Milgo alipojipa cheo kuwa AFISA UKAGUZI, akakikagua chumba ambacho kumbe hatakilala! Milgo akakikagua na kitanda mbele ya macho yangu, na bado haikutosha, akakisifia kitanda kuashiria kwamba yuko tayari kwa tukio kabla hajaniruka mita 1000!
Niliumia zaidi baada ya kujipa hisia kuwa haya ndio malipo ninayolipwa na bint huyu, kwamba hii ni adhabu, na kwamba adhabu hii inakujaje wakati kama huu? Kwamba mapema sana kwa safari yetu, tayari yanajitokeza haya! Nilishindwa kushangaa!
Lakini kingine hiki. Je kesho kutakapokucha, nitawezaje kumuona tena? Nitampata wapi? Safari yetu kwa kesho, ya kuvuka boda, ni jioni, je huyu mrembo nitampata wapi kwa kutwa ya kesho angalau nifanye ile watoto wa kijiweni wanasema force king!
Picha zilikatika ghafla baada ya John kunitaka niitikie salamu ya good night niliopewa na Milgo na Fatma kwa pamoja. Sikumbuki kama niliitikia na hata kama niliitikia, sikumbuki niliitikiaje!
Kilicho dhahiri ni kwamba Milgo na Fatma waliondoka wakijua kuwa, taarifa yao walioileta kwetu, mimi na John, usiku ule, pale mgahawani, haikuwa njema. Ilikuwa ni taarifa mbaya, tena kwa nyakati mbaya. Kwa mara nyingine tena nikaingia katika majuto, majuto ya kujitakia. John hakuonyesha hata dalili moja ya kujutia, wala kunionea huruma. Nadhani na yeye alikuwa na msimamo kuwa
haya yanayonikuta, nimejitakia mwenyewe, sipaswi kuonewa huruma!
Tukarudi hotelini. Tukazungumza kidogo na John. John akanipa tathimini yake ya safari, na mimi nikampa yangu. Ni kama vile John alisahau yote yalomkwaza wakati wote wa safari, John aliongea kwa utulivu wa kipekee, na kwa upole sana. Ikanifanya nimsikilize kwa umakini wa ziada.
John alinielezea namna alivojiandaa na safari hii kwao Kampala, Uganda, safari ya Johannesburg, kwamba ukiacha maandalizi ya kifedha na mambo mengine, alishajiandaa kisaikolojia kuwa, safari itakuwa ngumu, yenye changamoto nyingi, lakini katika kile ambacho anasema, anamshukuru Mungu, ni kwamba mpaka sasa anakaribia kuiacha ardhi ya Tanzania, mambo yako sawia.
Anasema ameifurahia safari. Safari imekuwa ya amani na ya kuvutia kwa upande wake. Anasema haya yote anayaona kuwa yana mchango wa moja kwa moja wa mimi, rafiki yake ambae, anasema nina roho ya kipekee! Anasema nimehusika kuifanya safari hii iwe nzuri kwake. Anasema anamshukuru Mungu kwa hili, na anaomba sana, rafiki yake nisibadilike!
Binafsi nilimuelewa, nikamshukuru kwa kutambua nafasi nilionayo mimi rafiki yake katika safari yetu, lakini pia nikamhakikishia kuwa, mimi na yeye ni kama ndugu, si marafiki tena, nitakuwa nae pamoja mpaka mwisho wa safari yetu.
Tuliendelea kujadili vitu vingi sana, ni kama sio sisi ambao muda mchache uliopita, ndani ya chumba hiki hiki tulikuwa tunabishana nani awe wa kwanza kuoga! Sasa hivi tunaongea na kucheka pamoja kama ndugu mapacha wanaopendana, sikumbuki nani alikuwa wa kwanza kupata usingizi, ila tu nilikuwa wa kwanza kushtuka kukiwa kumepambazuka!
Nilitumia lisaa limoja pale juu ya kitanda cha nyumba ile ya wageni, ili kuwaza na kuwazua, nikipanga na kupangua wazo moja baada ya jingine. Niliwaza kama niko sahihi kimaamuzi, niliwaza kama ndoto zangu kuhusu safari hii zitatimia! Nilitumia muda ule kuwakumbuka ndugu na jamaa zangu niliowaacha, wengi wakiwa Tabora, wengine Morogoro, na kadhaa wa Dodoma na Dsm.
Nikamkumbuka girlfriend wangu wa tangu A level. Nikamkumbuka namna alivokuwa ananibishia kuwa nisifanye safari hii. Alinisihi sana kuendelea kupambana hapa hapa bongo, alinipa hoja kuwa kwa elimu yangu ya chuo, nisingesota sana mtaani kabla ya kutoboa! Alisema anaamini sana juu ya uwezo wangu wa kuchakarika! Alidai kuwa, namna anavonijua kuwa mimi ni mpambanaji, basi hata ndani ya bongo, maisha ningeyapatia!
Maskini Lilly wa watu, hakuna nilichomkubalia, alisononeka, alinyongonyea, alilia sana juu ya uamuzi wangu! Mwisho nakumbaka aliniombea sana kwa Mungu, nifanikiwe katika safari yangu na kule niendako, kwa ahadi kuwa atakuwa na mimi kwa kila hatua!
Kwa lilly, South Africa ni nchi wanayokimbilia vijana wasio na kazi, vijana walioshindwa maisha bongo, vibaka na wavuta bangi flani hivi wa mtaani! Lilly hakuwahi kudhani wala kujua kuwa mtu mwenye elimu ya chuo, kama mimi, ningeweza kujiwa na mawazo kama haya yaliopelekea mimi kuanzisha safari hii!
Huyu Lilly. Uhuhsiano wetu ulianzia katika harakati za kielemu high school. Sikusoma nae shule moja, ilikuwa ni katika tuition zinazohusisha wanafunzi wa kutoka mashule mbali mbali, ya jijini Dsm. Nakumbuka nilivompata Lilly. Ilikuwa ni katika ule utaratibu wa walimu wa tuition kuwafanyisha pepa wanafunzi wao kila Jumamosi, ilitokea pepa moja ambayo nilipasua kwa kupiga banda, na hakukuwa na banda lingine katika ile test pepa na bahati mbaya siku ya kurudishiwa hizo pepa, sikuwepo!
Yule mwalimu huwa hataki kubaki na pepa za wanafunzi, akalazimisha mtu anipokelee, hakupatikana mtu, lakini mwishoni mwa kipindi, Lilly alijitolea kwenda kuichukua ile pepa kwa ahadi kuwa atanifikishia mimi mhusika. Tangu Lilly anikabidhi pepa ile, nikamganda, na hatimaye tukafungua ukurasa mpya wa mapenzi!
Kwa hofu ya kumuumiza na kupata upinzani, safari ya DSM kwenda Cape town nilimficha. Na huu ulikuwa ni ujinga ambao nilikiri kwake baadae, mpaka nagonga visa ya South Africa, ya siku 90, Lilly wangu hakuwa anajua kitu, hakuwa anajua kuwa mimi ni MSAFIRI.
Sikumbuki vizuri, kama nilipatwa na akili gani, lakini tangu nigonge visa, sikuwahi kutembea bila ya passport. Kila nilipokwenda, nilikuwa nayo katika mkoba. Ikatokea siku moja nina ahadi ya kukutana na Lilly kwa maana ya kwenda kuiridhisha miili yetu, pia nilikuwa nayo.
Kama kawaida, tulikutana sehemu yetu ile ile tulioizoea, Lilly akiwa mtoto wa Tabata, na mimi nikiwa mtoto wa Temeke, nilibahatika kulijua chimbo moja hivi maeneo ya Buguruni, nyuma ya soko maarufu la Mnyamani, jirani na hospitali ya Buguruni, mkono wa kulia kama Unaeelekea Vingunguti, kulikuwa na lodge imejichanganya katikati ya makazi ya uswahilini.
Ndani chumbani, kila kitu ndani kwa ndani, ni kama vile Lilly alijua kuwa nakaribia kusafiri na kwamba nitam-miss, alinipa ile wajuzi wa mambo wanasema mseto wa hardcore seksi na crazy seksi! Lilikuwa ni tukio la kipekee sana, huwa inatokea mara chache sana!
Ilipigwa game ambayo hata yeye mwenyewe alihoji kuwa amepatwa na nini ile siku? Zile style ambazo Lilly huwa mbishi nazo, leo alikuwa anazianzisha mwenyewe! Kuna style ambazo alikuwa hazitaki, si tu kuzifanya bali hata kuziskia, lakini kwa siku hii niliruhusiwa!
Ni katika game hii hii, ndio kwa mara ya kwanza lilly aliniomba tushushe godoro chini, na nilipotaka kujua kulikoni, alitoa hoja kuwa linampunguzia ufanisi wake na kwamba pia kuna kitu special anataka kunionyesha!
Nikakubali.
Nikajikakamua mtoto wa kiume, nikalishusha godoro chini! Nipo tayari kuonyeshwa kitu special kwa ufanisi sahihi.
Waione:
chiko18 NYANYADO Aristidi selestin Milugwi Heaven Sent icca peterchoka Gobe loveissweet miss nuru Ngosha ze Dong Lee Cho in whitedoug3 pius manasse vesta bertha micheal HARUFU HALELUYA MOSHI Pritty wa joseph