Habari wana Jamii forums.
Naingia kwenye jukwaa hili kwa mara ya kwanza nami kutafuta ushauri juu ya yanayonisibu. Najua Jamii forums ni elimu tosha kwa kuwepo watu wa aina tofauti tofauti.
Mimi ni kijana niliyemaliza chuo mwaka juzi mkoani mwanza katika chuo kimoja maarufu. Kwa sasa nafanya vibarua tu vya kuunga unga ili kusogeza siku, nina mpenzi ambaye naye kwa mwaka na nusu sasa na tunapendana sana.
Mwaka huu nahisi nitapata bahati ya kuingia katika jeshi la wananchi. Sasa tatizo ni kwamba mpenzi wangu huyu hataki mimi niende huko na kwamba nitakaponyanyua tu mguu kwenda huko na huku nyuma ndo basi tena sina changu.
Kiukweli nami nampenda sana na sijui nifanyeje kwa kweli. Wana Jamii forums najua kuna watu wana busara na hekima zao humu ambao wana uwezo wa kutoa kitu kitakachonisaidia mimi na wengine juu ya hili.
Nawasilisha.
Kwani wewe akili yako na moyo wako unakutumaje? tena huyo mwanamke wako ningekua mie ningekushawishi uende ili ukirudi unakua ngangari zaidi na ntajigamba kua mpenzi wangu namtegemea kwa mengi...