Mpenzi hataki niende Jeshini

Mpenzi hataki niende Jeshini

Anaogopa nn au anafikiri ukirudi dushe litakua la bakabaka.
 
Kwa lugha nyepesi ni kuwa huyo mpenzi wako hakupendi ninapo sema hivyo nina maanisha kuwa ametoka nje kabisa ya dhumuni la mapenzi ambapo ni kusaidiana kwenye shida na raha na kutiana moyo wakati wa kipindi kigumu huku mkipeana matumaini yenye mafanikio.

Mpenzi anayekupenda kutoka moyoni hawezi kuwa miongoni mwa wanaokurudisha nyuma bali miongoni mwa watu wanaokupa moyo ili usonge mbele mpenzi anayekupenda kwa dhati hawezi kuwa miongoni mwa watu wanaofurahia anguko lako au mateso yako bali anatakiwa awe ni mtu anayepambana na wewe bega kwa bega katika kuyakabili mahangaiko yako na kukufariji na kukupa moyo pale unapotaka kukata tamaa.

Kama mpenzi wako anaona upo kwenye kipindi kigumu alafu anapuuza au kukwamisha juhudi zako za kujikwamua kutoka hapo ulipo tambua kuwa huyo si mtu mzuri kwenye maisha yako na yakufaa kumuepuka mara moja kwa wakati huu usiupe moyo wako nafasi ya kuamua jambo zito kama hili kwani moyo unaongozwa na hisia za kimapenzi bali unatakiwa utumie uhalisia wa jambo na akili yako kufanya maamuzi.

Jaribu kuwatazama watu walionyuma yako wanahitaji msaada wako ,jaribu kuthamini juhudi za waliokufikisha hapo ulipo sahihi tathimini hasara na jitihada walizoonyesha wazazi wako hadi kukufikisha hapo je ungependa hayo yote yapotee kwa sababu mtu mmoja mpuuzi mliyekutana tu maishani.

Je upo ladhi kumwona mzazi wako akiteseka kwa kukosa msaada wako kwa ajili ya mtu asiye jua hata uchungu wa mahangaiko waliyopitia wazee wako hadi wewe kufika hapo kuachana nae haimaanishi kuwa hautopata mwingine mzuri kama yeye isipokuwa utapumzika huku ukimsubiri yule aliyeumbwa spesho kwa ajili yako wanawake warembo wamejaa kila kona na kila pembe ya dunia.

THINK BIG

Mkuu huwa unatumia kinywaji gani?
 
Habari wana Jamii forums.

Naingia kwenye jukwaa hili kwa mara ya kwanza nami kutafuta ushauri juu ya yanayonisibu. Najua Jamii forums ni elimu tosha kwa kuwepo watu wa aina tofauti tofauti.

Mimi ni kijana niliyemaliza chuo mwaka juzi mkoani mwanza katika chuo kimoja maarufu. Kwa sasa nafanya vibarua tu vya kuunga unga ili kusogeza siku, nina mpenzi ambaye naye kwa mwaka na nusu sasa na tunapendana sana.

Mwaka huu nahisi nitapata bahati ya kuingia katika jeshi la wananchi. Sasa tatizo ni kwamba mpenzi wangu huyu hataki mimi niende huko na kwamba nitakaponyanyua tu mguu kwenda huko na huku nyuma ndo basi tena sina changu.

Kiukweli nami nampenda sana na sijui nifanyeje kwa kweli. Wana Jamii forums najua kuna watu wana busara na hekima zao humu ambao wana uwezo wa kutoa kitu kitakachonisaidia mimi na wengine juu ya hili.

Nawasilisha.

kama yeye ndo alikulipia ada msikilize.utasubiri sensa upate dili
 
Unapangiwaje hatma ya maisha yako na mtu umuitaye "mpenzi" wako...!!!
 
Hasira sana kukutana na watoto kama nyinyi ambao hamuwezi kuamua hatima ya maisha yenu, pole najua umri wako ni mdogo. Usikubali hatima ya maisha yako akaamu mtu mwingine wakati una uwezo wa kufanya hivyo. Nenda jeshini dogo.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
#Wasukuma mnazidi nitia aibu aiseee....

Mwingine jana kagongwa nyoka anafanya mapenzi porini...wewe nae unamsikiliza mwanamke.

Mi nnavojua mwalimu wa hawa viumbe alishadanchi na alikuwaga na mtindio wa ubongo na alikuwa haoni vizuri mbaya sana kawarithisha kila kitu hadi kufikiri.

Maamuzi yao ndo ivo tena yametawaliwa na kiuno. Kazi kwako, hicho unachouliza mwenzio umewazia kwa kutumia kiuno sio kichwa.

Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Huyo Achana Naye Kuna Madada Wengi Sana Wako Single Humu Ukishapata Kazi Njoo Utangaze Nia Hapa Utawapata
 
Kwa lugha nyepesi ni kuwa huyo mpenzi wako hakupendi ninapo sema hivyo nina maanisha kuwa ametoka nje kabisa ya dhumuni la mapenzi ambapo ni kusaidiana kwenye shida na raha na kutiana moyo wakati wa kipindi kigumu huku mkipeana matumaini yenye mafanikio.

Mpenzi anayekupenda kutoka moyoni hawezi kuwa miongoni mwa wanaokurudisha nyuma bali miongoni mwa watu wanaokupa moyo ili usonge mbele mpenzi anayekupenda kwa dhati hawezi kuwa miongoni mwa watu wanaofurahia anguko lako au mateso yako bali anatakiwa awe ni mtu anayepambana na wewe bega kwa bega katika kuyakabili mahangaiko yako na kukufariji na kukupa moyo pale unapotaka kukata tamaa.

Kama mpenzi wako anaona upo kwenye kipindi kigumu alafu anapuuza au kukwamisha juhudi zako za kujikwamua kutoka hapo ulipo tambua kuwa huyo si mtu mzuri kwenye maisha yako na yakufaa kumuepuka mara moja kwa wakati huu usiupe moyo wako nafasi ya kuamua jambo zito kama hili kwani moyo unaongozwa na hisia za kimapenzi bali unatakiwa utumie uhalisia wa jambo na akili yako kufanya maamuzi.

Jaribu kuwatazama watu walionyuma yako wanahitaji msaada wako ,jaribu kuthamini juhudi za waliokufikisha hapo ulipo sahihi tathimini hasara na jitihada walizoonyesha wazazi wako hadi kukufikisha hapo je ungependa hayo yote yapotee kwa sababu mtu mmoja mpuuzi mliyekutana tu maishani.

Je upo ladhi kumwona mzazi wako akiteseka kwa kukosa msaada wako kwa ajili ya mtu asiye jua hata uchungu wa mahangaiko waliyopitia wazee wako hadi wewe kufika hapo kuachana nae haimaanishi kuwa hautopata mwingine mzuri kama yeye isipokuwa utapumzika huku ukimsubiri yule aliyeumbwa spesho kwa ajili yako wanawake warembo wamejaa kila kona na kila pembe ya dunia.

THINK BIG

Sioni kama msimamo wa msichana ni wa kukosa upendo. Asiye na upendo atakuruhusu hata kufanya ujambazi mradi ale na siku ukiuwawa au kutiwa mbaroni anahamia kwa mwingine siku hiyo hiyo. Anayekuchagulia kazi ya kufanya "anakupenda sana". Yeye si anaona shida unazopata? Na pengine hata mahitaji ya msingi humtimizii lakini anavumilia ili mradi upate kazi atayoridhika nayo.
Tukija kwenye kazi ya jeshi tambua kuwa kazi ya msingi ya mwanajeshi ni "kuua". Hizo lugha za "kulinda mipaka ya nchi" ni kuzunguka tu. Mtu mwingine lile wazo la kuajiriwa kazi ya "kuua" halikubaliki akilini mwake. Na mke anaweza kuhofu kuwa ukatili unaojifunza jeshini unaweza kuuhamishia nyumbani pale atakapokuudhi!
Pia huenda anahofia ujane wa mapema maana unaweza kutumwa Nigeria kupambana na boko haram likarudi jeneza!
Pia fikiria askari kutumwa nje ya nchi na kukaa miaka 3 huko bila kuonana na familia!
Kwa hiyo binti ni lazima asikilkilizwe na suala hili lisihusishwe na upendo maana tatizo si upendo ni aina ya kazi.
 
Ingekuwa vyema kama binti angekuwa anampa option zingine za life lakini kama yeye anataka tu usiende then baada ya hapo hakuna kinachoendelea...ili hali wewe kuna watu kibao wanakutegemea...na kuhusu ukatili basi kama watu wote wangekuwa na mawazo hayo basi wanajeshi wasingeoa...
Na kuhusu kufa au kubaki mjane basi watu wasingeoana kwa maana wangekuwa wanaogopa kufa wenzi wao na kubaki wajane....kinachotakiwa kama unapingana na mpenzi kwenye jambo linalogusa future yenu toa option zingine tena zenye mashiko..ili mtu ajipime mwenyewe...sio mtu anapata chansi alafu tu unamuambia mimi sipendi hivyo ngoja mungu atakupa nyingine...
 
hata mi nlikatazwa sahv ngekua zangu mjeda natembea kifua mbele...nenda tu mwayego
 
Njoo jeshn dogo achana Na uyo mwanamke kwanza ukifika uku hutamtaka tena uyo....wazur wengi njoo uwe kamanda
 
Nenda jeshini kwanza, ukishamaliza halafu ukarudi na kukuta ameolewa unaenda kufata platoon yote mliotoka mafunzoni kuja kuvamia wanapoishi na huyo mume wake mpya mnatembeza vipigo kwa wanaohucka na wasiohucka
 
ivi unajua kazi ya jeshi ni moja kati ya kazi zinazotakiwa uwe na uwamuzi mzuri na wa haraka sana.sasa ww unataka kwenda huko alafu eti GF kanizuiya naombeni ushauli khaaaa!!!ivi ww sikulaumu lkn jipime tena kwanza.kazi unayotaka kwenda alafu unapigwa mkwala na GF !!hhhahaha kweli tupo tofauti
 
Attachments

  • 1424523081993.jpg
    1424523081993.jpg
    10.4 KB · Views: 158
Mi nahisi mtu akikataa anatoa na sababu, mtoa mada hajafafanua hilo.
Mwanaume anaruhusiwa kuoa mwanamke ambaye si mwana jeshi lakini kuna kipindi nilisikia mwanamke mwanajeshi haruhusiwi kuolewa na raia...
Nisaidieni wadau hii ina ukweli wowote?
 
Hebu jaribu kuongea nae kwanza, kwani yeye anahofia nini?
 
Nenda jeshini kwanza, ukishamaliza halafu ukarudi na kukuta ameolewa unaenda kufata platoon yote mliotoka mafunzoni kuja kuvamia wanapoishi na huyo mume wake mpya mnatembeza vipigo kwa wanaohucka na wasiohucka

achukue kombania kabisa alafu wampige huyo jamaa funga fungua za kutosha, nyakuanyakua za kutosha....
 
Back
Top Bottom