Mpenzi hataki niende Jeshini

Mpenzi hataki niende Jeshini

Mwangaruka

Member
Joined
Nov 30, 2014
Posts
24
Reaction score
2
Habari wana Jamii forums.

Naingia kwenye jukwaa hili kwa mara ya kwanza nami kutafuta ushauri juu ya yanayonisibu. Najua Jamii forums ni elimu tosha kwa kuwepo watu wa aina tofauti tofauti.

Mimi ni kijana niliyemaliza chuo mwaka juzi mkoani mwanza katika chuo kimoja maarufu. Kwa sasa nafanya vibarua tu vya kuunga unga ili kusogeza siku, nina mpenzi ambaye naye kwa mwaka na nusu sasa na tunapendana sana.

Mwaka huu nahisi nitapata bahati ya kuingia katika jeshi la wananchi. Sasa tatizo ni kwamba mpenzi wangu huyu hataki mimi niende huko na kwamba nitakaponyanyua tu mguu kwenda huko na huku nyuma ndo basi tena sina changu.

Kiukweli nami nampenda sana na sijui nifanyeje kwa kweli. Wana Jamii forums najua kuna watu wana busara na hekima zao humu ambao wana uwezo wa kutoa kitu kitakachonisaidia mimi na wengine juu ya hili.

Nawasilisha.
 
Nenda jeshini,akiolewa na mtu mwingine, juwa hakuwa riziki yako! Dunia ya sasa pesa mbele mapenzi yanafuata.
 
How do you people live? Demuuuu anakupangia maishaaaa? Bora hata angekuwa mke.

Usiende jeshini tuliza kitako tuliii kama una nyolewaaa, ungoje umuone atavoolewa na kamanda wa jeshi. Baadae utakuja kujilaumu kwanini hukwenda, bora ungeenda na kumuona bibie kakuhariabia maisha kumbe UMEJIHARIBIA MNYEWE MAISHA. Alichofanya bibie ni kukupa kamba tu na wewe ulivo boya ukaenda kujinyonga mwenyeweeeeeeeeee.
 
kaa nae chini muulize, anapenda wewe uwe nani na nafasi gani katika kazini? akijibu, mwambie unampa mwezi 1 wa yeye kuhakikisha unakuwa kazini. na kama akisema anataka uwe mjasiriamali, mwambie akupe mtaji wa kutosha wewe kufanya kile unachotaka, au akutafutie kazi kabla ya june 2015, uwe kazini na mshahara mnono unapata.

akijikanyaga mwambie mimi naenda jeshi, nikimaliza nakuoa na maisha yanaendelea, ukimtukuza sana unaweza ukashangaa cku ya cku anakuacha ktk mataa anaenda na Dangote.

ila mtie moyo, mwambie ni muda mfupi tu mama nitakuwa nimemaliza kozi usijali.
 
lara 1
Dah hili lina ukweli sana. Ndo maana nimekuja humu kwa kujua nitafungua mind. Asante sana mkuu lara
 
Last edited by a moderator:
Kwa hakika hizo kazi za kuungaunga na mapenzi uliyonayo kwa huyo binti ipo siku utajinyonga kama sio kurudi humu kuomba ushauri tena baada ya wenye fedha (tena wengine wanajeshi haohao) kumbeba kwa kuwa wanatimiza mahitaji yake.

Juhudi ni mtego wa noti mkuu, na mapenzi bila pesa ni sawa na mboga bila chumvi!Ushauri wangu ni kuwa hakuna haja ya kulumbana nae kwa sasa (msije gombana hata jeshini kwenyewe hujaenda)

Wewe kaa kimya chance ikija mpe taarifa tu ya kumuaga, then atachagua kukusubiri au kukupiga chini!Ukipata hiyo kazi kuna wanawake wengi wazuri ambao bila fedha ungewasikia ndotoni tu. Mfano ni huyu hapa miss chagga kwanza aje kukushauri sasa hivi.
 
Nna wasiwasi na swala la ukomavu wa akili (umri) kwenu wote wawili, na sina uhakika kama kweli maisha mnayafahamu vyema...

Any way..

Mpelekee comments hizi azisome zote, atajua tu kua unampenda na yeye atakua ameshaurika pia kupitia hapa, na atakungoja ukitoka mafunzo kwakua atakua ameelewa...
 
ungesema pia na sababu alizokupa kwanini hataki ujiunge na jeshi, labda anakuona unaweza kufanya vyema Zaidi ya 'kutalii kwenye mapango ya Amboni' (No pun), Muulize vizuri. Ila hiyo condition kwamba ukienda ndio basi tena noma sana bro, who's the man in that relationship?
 
Bro, me nadhan hakujua jinsi gan umesumbukia elim yako hadi hapo ulipo, kama na ww hukuona Hilo, bac usiende jeshin, ila kama ulitesekea hiyo shahada, Bro ni bora ukaenda 2,
 
Kama ndo Mara ya kwanza kutolewa bikra na Huyo mwanamke,au ww ndiye uliyemtoa bikra,ukienda huko utakutana na misumari zaidi yake. Pili ww ndiye mwanamme lazima uchakalike mwishoni utakuwa bushoke. Jitathmini na ondoa kauli take eti bila yeye huwezi ishi.
 
Je aliwahi kukuambia anapenda ufanye kazi gani? na je amewahi kukuelekeza mamna ya kuipata hiyo kazi?
Kisha angalia mtazamo na uchungu wake kwako juu ya kuishi bila kazi. Kama haonyeshi kuguswa na maisha yako ya kuunga unga basi hana upendo wa kweli kwako.

Hapa picha ninayoipata kwake ni kua anakutafutia sababu ya kuachana na wewe. Kipimo kizuri cha kujua hilo ni wewe kwenda jeshini kama atakusubiri basi ni wako na kama atakuacha basi alikua hana malengo ya kuishi na wewe.
 
Kwa lugha nyepesi ni kuwa huyo mpenzi wako hakupendi ninapo sema hivyo nina maanisha kuwa ametoka nje kabisa ya dhumuni la mapenzi ambapo ni kusaidiana kwenye shida na raha na kutiana moyo wakati wa kipindi kigumu huku mkipeana matumaini yenye mafanikio.

Mpenzi anayekupenda kutoka moyoni hawezi kuwa miongoni mwa wanaokurudisha nyuma bali miongoni mwa watu wanaokupa moyo ili usonge mbele mpenzi anayekupenda kwa dhati hawezi kuwa miongoni mwa watu wanaofurahia anguko lako au mateso yako bali anatakiwa awe ni mtu anayepambana na wewe bega kwa bega katika kuyakabili mahangaiko yako na kukufariji na kukupa moyo pale unapotaka kukata tamaa.

Kama mpenzi wako anaona upo kwenye kipindi kigumu alafu anapuuza au kukwamisha juhudi zako za kujikwamua kutoka hapo ulipo tambua kuwa huyo si mtu mzuri kwenye maisha yako na yakufaa kumuepuka mara moja kwa wakati huu usiupe moyo wako nafasi ya kuamua jambo zito kama hili kwani moyo unaongozwa na hisia za kimapenzi bali unatakiwa utumie uhalisia wa jambo na akili yako kufanya maamuzi.

Jaribu kuwatazama watu walionyuma yako wanahitaji msaada wako ,jaribu kuthamini juhudi za waliokufikisha hapo ulipo sahihi tathimini hasara na jitihada walizoonyesha wazazi wako hadi kukufikisha hapo je ungependa hayo yote yapotee kwa sababu mtu mmoja mpuuzi mliyekutana tu maishani.

Je upo ladhi kumwona mzazi wako akiteseka kwa kukosa msaada wako kwa ajili ya mtu asiye jua hata uchungu wa mahangaiko waliyopitia wazee wako hadi wewe kufika hapo kuachana nae haimaanishi kuwa hautopata mwingine mzuri kama yeye isipokuwa utapumzika huku ukimsubiri yule aliyeumbwa spesho kwa ajili yako wanawake warembo wamejaa kila kona na kila pembe ya dunia.

THINK BIG
 
Back
Top Bottom