Habari.. Mimi ni binti nilikuwa naishi na mwanaume kienyeji tu toka mwaka 2017 mwezi wa 8. Nilikuwa nasomea ualimu na nilimaliza mwaka Jana December..kifupi mwanaume wangu sio fighter ni wale mama's boy..hana shuguli yoyote anayofanya na tulikua tukiishi kwao na maisha yetu yalikua magumu na ya kubangaiza sana Mara nyingi pesa nilizokuwa napewa kama pocket money na ndugu zangu kwa ajili ya chuo ndio zilikua zikitusave .Nilipomaliza chuo niliamua kuingia mtaani kutafuta ajira yoyote ya kujishikiza maana ajira za ualimu ni za manati..nilibahatika kupata kazi ya receptionist hotel Fulani January, hapo ndio shida ilipoanzia mwenzangu hakitaka kabisa ile kazi akidai ni ya umalaya so nikae mpaka nipate shuleni..Mimi nilimsihi sana nijishikize tu wakati bado naendelea kutuma maombi mashuleni siku nikipata nitaacha hotelini. Niliikazania ile kazi coz maisha yalishakua magumu sana pale nyumbani mpaka wakati mwingine tunalala njaa, mwenzangu alikataa kabisa na alinipiga sana siku hiyo, nikaamua kuondoka kwenda kwa Dada yangu kuishi huku nikiendelea kufanya kazi hotelini..baada ya siku kadhaa tulielewana na mwenzangu na jioni moja nilipotoka kazini nilikwenda kumtembelea na aliniazima cm yangu ya smartphone kuwa ana kazi nayo baada ya siku mbili atanirudishia nikamuachia ile cm..ile cm nilinunuliwa na mdogo wangu wa kike baada ya kupata pesa Fulani..Jamani yule mwanaume baada ya siku kama 4 nikamkumbusha vp simu yangu, aligeuka mbogo akaniambia sahau kuhusu simu hii simu inafidia muda wote uliokaa kwangu..Je jamani nilikosea wapi niambieni na ni haki yeye kuninyang'anya simu? Naombeni mbinu za kuipata simu yangu tafadhali msinitukane

