Mpenz wangu hanijali

Jamaa hana time na wewe, chapa lapa tu japo utaumia ila maisha yataendelea.....
pole
 
Kuna mtu amechukua nafasi ndio anamfanya awe busy wakati wote.
 
Pole dada siku zote ukiona mawasiliano yanasuasua jua there is something behind. Nakushauri nawe mchunie alafu tafuta siku muonane ana kwa ana ili mwongelee kuhusu mstakabali wa mahusiano yenu. Wala usije kutoa jozi mbele yake utaonekana dhaifu jitahidi uwe na confidence siku hiyo.Baada ya hapo utajua cha kufanya.
 
Kaachwa...
Mapenzi hayaeleweki wakati mwingine

Atakuwaje na uhakika kuwa kaachwa kwa mpenziwe kuwa kimya pekee?

Kosa huwa halitatuliwi kwa kufanya kosa jingine au lile lile...

Hawa watu ni wapenzi kwa mantiki hiyo wana nafasi ya kuongea na kurekebishana. Kama huyu dada anashindwa kufunga safari na kwenda kuongea na mpenziwe kulitatua hili basi ahesabu maumivu zaidi ya haya.

Mwisho wa mapenzi yao ni hadi pale watapokubaliana kuwa wameachana lakini si kwa mmojawao au wote kuchuniana.

Pia kuna wakati wapenzi huwa wanahitaji walau nafasi kidogo 'space'...it's a temporary thing.
 
Kaanza lini? Labda nakwepa jukumu la kuonyesha mapenzi ya kitamthilia kesho. Msikilizie mpaka jumapili, kama bado anang'ang'ania kukaa huko busy na hana mpango na wewe mtakie kila la kheri uendelee na maisha yako.

Mwambie unamuacha kabla hajakuwahi, ITAKUUMA SANA.
 

watu8 unadhani kila mtu anaweza kumuacha mwenzie kwa kumuambia na kukubaliana? Kwa wengine ukimya ndio kibuti chenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Mfuate mwambie ukweli kama ulivyotuambia sisi....ukiona hakuna mabadiliko....changanya ushauli uliopewa + akilizako= fanyamaamuzi
 
^^
Fanya ziara ya kushitukiza anapoishi, ujionee mwenyewe au uzungumze nae!
La msingi usijipe majibu mwenyewe au kuhisi na usiwe mwepesi wa hasira
Pole.. Mapenzi ndipo yalipotufikisha
^^
 
watu8 unadhani kila mtu anaweza kumuacha mwenzie kwa kumuambia na kukubaliana? Kwa wengine ukimya ndio kibuti chenyewe.

Inawezekana ukimya ukawa ni kibitu kama wengi wafanyavyo, lakini kuuchuna si namna nzuri ya kujiaminisha kuwa ukimya wa jamaa unamaanisha kibuti.

Bi mkubwa aondoe dukuduku lake kwa kuongea na mchumbaye, unless labda atuambie anaogopa kupigwa kibuti face to face.
 
Last edited by a moderator:
Isnt it crystal clear she isnt wanted any more??

Jirani huenda ikawa ndio au hapana...lakini azungumze na mchumba wake itakuwa ni vyema zaidi.

Kama ni kubuti basi na huyo mwanaume aseme ili kesho na keshokutwa asiwe na sababu za kujifaraghua tena.
 
Auchune tu na yeye, IF jamaa akija mtafuta baada ya muda she can decide kumpotezea au wakaongea new terms and conditions if she still wants him
 
Jirani huenda ikawa ndio au hapana...lakini azungumze na mchumba wake itakuwa ni vyema zaidi.

Kama ni kubuti basi na huyo mwanaume aseme ili kesho na keshokutwa asiwe na sababu za kujifaraghua tena.

Mie kwa kweli kwenye issue za mapenzi siumizagi kichwa. I have zero tolerance for games in the name of love.
 
Auchune tu na yeye, IF jamaa akija mtafuta baada ya muda she can decide kumpotezea au wakaongea new terms and conditions if she still wants him

But for how long?
 
Talk to him mweleze ukweli namna unavyojisikia kwa yeye kukuweka mbali nae,muulize sababu,
then kuwa na msimamo kama mwanamke kamili sio ukiambiwa ooh baby..unajua...unakua kimya kama kondoo aliyenyeshewa no!
You can stand with your own feet!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…