Mpendeni tu kwani kufanya vizuri ni makosa

Mpendeni tu kwani kufanya vizuri ni makosa

SOEN

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2023
Posts
407
Reaction score
184
IMG_5468.jpg
Hapa tulipo kwa nchi ilipopitia enzi za mwenda zake jamaa amepambana sana kuinua uchumi na kujenga mahusiano na mataifa ya nje na wadau mbalimbali wa maendeleo, uwekezaji umekua hakuna TRA kutumia mabavu.

Makusanyo ya kodi yameongezeka na yanazidi kupanda! Binafsi nasifu na kupongeza kwa jitihada hizi.
 
Ni jambo jema

Huyu ni Waziri pekee aliyewahi kuapishiwa Ikulu ndogo ya Chato sawia na Waziri mdogo Mollel

Ana Baraka zote za Kanda ya Ziwa 2030!
 
Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 umewezesha nchi kufikia mafanikio mbalimbali ikiwemo kuingia katika uchumi wa kati wa hadhi ya chini ambapo Taifa lilifanikiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa wastani wa asilimia 6 na kupungua kwa kiwango cha umaskini kwa zaidi ya asilimia tisa (9) kutoka asilimia 35.7 mwaka 2000/01 hadi asilimia 24.6 mwaka 2017/18. Aidha, vifo vya mama na watoto nchini vimepungua kutoka vifo 854 kwa vizazi 100,000 na vifo 99 kwa vizazi 1,000 mtawalia mwaka 2000 hadi vifo 524 kwa vizazi 100,000 na vifo 36 kwa vizazi 1,000 mtawalia mwaka 2020; kiwango cha udahili wa wanafunzi wa elimu ya msingi kimeongezeka kutoka asilimia 58.8 mwaka 2000 hadi 95.7 mwaka 2020; upatikanaji wa maji umeongezeka kutoka asilimia 50 mwaka 2000 hadi asilimia 86.7 mwaka 2020 kwa mijini na asilimia 55 mwaka 2000 hadi asilimia 72.3 mwaka 2020 kwa vijijini; na upatikanaji umeme vijijini umeongezeka na kufikia asilimia 69.8 mwaka 2020. Pamoja na mafanikio hayo, Taifa limepitia vipindi vigumu ikiwemo kudorora kwa uchumi wa dunia mwaka 2007 hadi 2008, mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO -19 mwaka 2020/21 pamoja na mabadiliko ya tabia nchi na vita vya Urusi na Ukraine vinavyoendelea. Serikali imeendelea kutekeleza Sera na Mikakati mbalimbali kuhakikisha inapambana na vihatarishi hivi vya maendeleo.
 
b1f1e16b-eaa3-4ada-9ef8-e3c95e77b7e0.jpg

Vijana haya mchakato upo wazi shirikini kwa wingi Dira ni ya wote vijana wenye mawazo pevu na bobevu
 
IMG_5472.jpg

Mmesahau enzi za barua ,RTD , magazeti mchana but now mimi nawewe tumeshika simu jana
 
View attachment 2575047
Hapa tulipo kwa nchi ilipopitia enzi za mwenda zake jamaa amepambana sana kuinua uchumi na kujenga mahusiano na mataifa ya nje na wadau mbalimbali wa maendeleo, uwekezaji umekua hakuna TRA kutumia mabavu.

Makusanyo ya kodi yameongezeka na yanazidi kupanda! Binafsi nasifu na kupongeza kwa jitihada hizi.
Yamepanda je yameleta tija gani kwa taifa la Tanzania?
 
Kuna faida gani kuongeza makusanyo ya mwezi huku pesa nyingi zikiibiwa?.
We need to be smart to speak of our money being stolen by those to whom we have entrusted power.
 
Tupe mfano wako,uchumi wako uliinukaje/kwa viwango vipi?Ili iwe rahisi kuwaelewesha wadau kwani inaonekana hawaelewi somo🤔
 
Back
Top Bottom