Mpende mke wako ila usimweke wazi madili yako yote, ona wangu alivyotaka kunipeleka polisi kunifungisha maisha

Samweli Mathayo

JF-Expert Member
Aug 1, 2017
1,577
1,700
Ni kitambo sana tokea nineweka komenti au siredi hapa

Kwa kifupi
Mwezi wa kwanza nilifanya jaribio dogo kumpima mke wangu juu ya uvumilivu wake na uwezo wa kifua chake kubeba mazito,

Mchana tulienda shambani mi na mke wangu, akalima mi nikaenda karibu na mti nikaanza kuchimba shimo kama kabuli lefu kidogo, muda wa kwenda nyumbani ukafika, akatangulia nikabaki namalizia kuchimba, saa nne usiku nilichelewa makusudi
Nilitoka shamba nikiwa na pick up limejaa damu maana nilimchinja kuku makusudi,

Nikafika nyumbani usiku saa sita nimamuita mke wangu chumbani kwamba naomba unisindikize ,nikamwambia unakumbuka lile shimo, sasa nililichimba kwa ajili ya shughuli muhimu ,akasema mbona usiku sasa?, nikasema njoo, akatoka nje kuangalia gari limejaa damu, na kuangalia nyuma akaona kama mzigo umefungwa kama mtu umekunjwa kunjwa kumbe ni gogo, ila nikamwambia nimeua mtu nataka nimzike, akashtuka sana akataka kupiga kelele nikamziba mdomo,

Baadae nikamueleza akanielewa, anakaa kwenye kiti pembeni yangu nikaendesha pikapu mpaka kwenye shamba letu nje ya mji kidogo ambako niliandaa shimo mapema wakati wa kuandaa shamba,

Nikamwacha ndani ya gari nikabeba mzigo (gogo) ambalo nililifunika shuka jeupe lililopakwa damu damu, akawa anaogopa hata kuangalia,

Nikaliweka gogo kwenye shimo nikafukia nikaanza kufukia, nikamaliza nkamwambia twende,

Nikamsihi atunze siri, tukakubaliana, ila cha kushangaza hakumaliza miezi tabia akabadili akaanza kubuli , akawa anarudi nyumbani usiku, mara anibwatukie mbele ya watu na watoto, nikavumilia wee wapi, nikanyanyasika si anajua naogopa kumgusa,akawa analeta rafiki zake ndani wanapiga kelele wanalewa, mara apigiwe simu na wanaume, nikawa bwege kwa muda,nikimuuliza saa nyingine analeta jeuri anajua na nikimgusa atasema, siku moja nikawa na wageni nyumbani hakupika wala kufanya kitu, nikajiuliza hivi kwanini hasa,

Sasa akajichanganya akachukua hela ya kazini ninetengewa niende field akatumia kwa mambo yake nilichofanya nikamtandika kofi la maana nikamuongezea,

Akaenda kwao akatahamaki, akawaeleza wazazi wake kwamba hanitaki tena nimebadilika mno, baba mkwe akawa ana msihi arudi, akakataa, nikaamua kumfuata, alipoona tu akakataa akasema niliua mtu hayuko tayari kurudiana nami, akasema kwamba anajua hata tulipomzika, na si mara ya kwanza mimi kuua, na akasema wakitaka atawaonesha nilipozika mtu huyo,

Mama mkwe akasema lazima walipot polisi haiwezekani, maana walidhani ni kufungwa na mali watachukua, ukioa kabila la kupenda hela uko kaskazini hatari sana,

Wakanipeleka kwa mjumbe walitaka kunikapeleka haraka polisi, nikajieleza nikasema kwamba mi si kuuawa ilikuwa experiment zangu tu,

Nikaita mashahid nilokuwa ninepamga nao dili ,ikabidi twende mwana mke awaoneshe mtu alipozikwa,

Tukaanza kufukua kufikia wanaona ni gogo limeshaanza kuliwa.mchwa na nguo zile,


Nilipomaliza nkasema wewe mwanamke basi ntaoa mwingine,


Wanaume kuwa makini aisee hawa wanawake hatari unaweza fungwa kuwahusisha dili
 
Mmh hili jaribio lako ni hatarishi, huyo mwanamke sio kwamba hakupendi ila wewe pia umemuweka kwenye wakati mgumu, lazima mtu awaze hatima ya maisha yake pia, kama umeweza kumua binadamu mwingine kwake itakuaje? We sema story kama za kutunga fulani.

All in all mwanamke sio wa kumwamini kabisa, sio wa Kaskazini tu, ngoma droo wote
 
Kwa kifupi unachosema ni kuwa hakuna siri ya watu wawili. Kanuni hii haijawahi kubadilika. Ukitaka jambo (hasa kama ni zito) liwe siri, basi usimwambie mtu yoyote hata mkeo. Kuna mambo unaweza kushare nae....kuna mengine just keep it to yourself. Mtadumu.
 
Back
Top Bottom