Mpendazoe aibukia Kinondoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpendazoe aibukia Kinondoni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Aug 3, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sekretarieti ya CHADEMA jimbo na Wilaya ya Kinondoni imemwomba mwanachama wake aliyehamia chama hicho hivi karibuni, Fred Mpendazoe (CHADEMA) kuwania ubunge katika Jimbo la Kinondoni. Tayari Mpendazoe amekubali kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwenye jimbo hilo.
   
 2. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu nae bora aende jimboni alikozaliwa.
   
 3. Vica

  Vica Member

  #3
  Aug 3, 2010
  Joined: May 27, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naombeni matoke ya kinondoni na mtera
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Jimbo la Kinondoni aliyeongoza ni Bw. Iddi Azan) akifuatiwa na Bi. Shy-Rose Bhanji
  Jimbo la Mtera aliyeongoza ni Bw. Livingstone Lusinde (5,810) akifuatiwa na Bw. John Malecela (5,379),
   
 5. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  akikosa huko aje achukue jimbo la JF ..
   
 6. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,182
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  mi namshauri apoe kwanza, apime alikotoka na anaenda wapi!
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  ni kiranja mzuri bungeni, anastahilim kuwepo lakindi ndio kazi inabidi ifanyike
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mtera Mzeee wetu kaangukia pua kwa kijana Lusinde.................
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Dah jamaa anabadilisha majimbo kama mashati!
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  jamani jimbo la ubungo vipi?
   
 11. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani mwacheni abaki huku huku Segerea apambane na Mahanga mwakilishi wa RA. chonde chonde CHADEMA mpeni nafasi ya kugombea huku, mimi nina usongo na huyu mwakilishi wa mafisadi. Mpendazoe atakuwa mhanga na mmoja wa wapiganaji dhidi ya ufisadi huku Makongoro akiwakilisha mafisadi! patakuwa patamu nami nimeamua kuondokana na siasa za kujificha nitatoka hadharani na kumsaidia Mpendazoe, shujaa wangu aliyeacha ubunge na marupurupu yote kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu.
   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,378
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  mtoto akililia wembe mpe...
   
 13. n

  nyamate Member

  #13
  Aug 3, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siyo mashati tu na soksi pia.Kwani kishapu alitoka kua huko?
   
 14. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  3rd August 10
  Mpendazoe aibukia ubunge Kinondoni

  Mwandishi Wetu

  Baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni za kuwania ubunge jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliyekuwa Mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe, ameombwa na chama hicho kuwania ubunge wa jimbo la Kinondoni .
  Ni baada ya Mpendazoe kuangushwa kwenye kura za maoni wa jimbo la Segerea hivi karibuni na Rachel Mashishanga katika uchaguzi ndani ya chama hicho uliofanyika hivi karibuni.
  Katika uchaguzi huo, Rachel alipata kura 41 na kumbwaga Mpendazoe aliyeambulia kura 28.
  Kwa mujibu wa Katibu wa Chadema, Wilaya ya Kinondoni, Fred Kimath, sekretarieti ya chama hicho jimbo na Wilaya ya Kinondoni ilikaa jana na kutoa uamuzi wa kumshauri Mpendazoea kuwania ubunge katika jimbo hilo.
  " Kwa kutambua umuhimu wa kuwa na watu mashuhuri kama Mpendazoe na Mashishanga, sekretarieti ilituma ujumbe kumwomba agombee jimbo la Kinondoni na amekubali kufanya hivyo, “ alisema Kimath.
  Alisema ujumbe ulioonana na Mpendazoe ni pamoja na Mwenyekiti wa jimbo hilo, Michael Sebugabo, Katibu Fred Kimath, Mweka Hazina, Edgar Njwaba, Katibu Mwenezi Moses Raymond, Katibu wa Mkoa wa Kinondoni, Henry Kilewo.
  Kimath, alisema sekretarieti imeitisha kikao cha kamati ya utendaji kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo yake kabla ya mkutano wa kura za maoni na uteuzi kwa kuzingatia Katiba na kanuni za chama.
  “Sekretarieti inamshukuru Mpendazoe kwa kukubali wito huu wa kuwatumikia Watanzania ikiamini Mpendazoe ni Mbunge wa Taifa ambaye m chango wake unahitajika kuing’oa CCM,” alisema Kimath.
  Mpendazoe alikihama Chama cha Mapinduzi CCM mapema mwaka huu, akidai kuwa kimepoteza mwelekeo na kuhamia Chama cha Jamii (CCJ).
  Baada ya chama hicho kukosa usajili wa kudumu hivyo kukosa sifa ya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Mpendazoe aliamua kuhamia Chadema.

  NIPASHE
  Mpendazoe aibukia ubunge Kinondoni
   
 15. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ITS A GUD MOVE I GUESS...! tunahitaji wabunge wa chadema wazidi 50. tumuunge mkono plzz..!
   
 16. D

  Dick JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mfa maji huyo....., la kuvunda.......!
   
 17. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  na mrema ntasemaje?mwacheni ajaribu bahati yake
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Anajuta na atajuta kuhama ccm, kuhama jimbo lake, angebadilisha kimoja, either chama au jimbo, amekurupuka, amebadilsha vyote, sasa anahaha, wale akina chiligati walisema wanamtakia maisha mema, hata mimi naungana nao. segerea amechemsha, sasa kinondoni, bila shaka alikuwa hajapima kina cha maji, sasa ndo anajua kuwa nikirefu, na uwezekano wa kisurvive ni mdogo. aje tuungani tu huku mtaani kuuza magazeti, si ajabu story yake imeishia hapo. Aliondoka kwa mbwembwe nyingi mara ccm si mama yangu, sasa atajua kuwa ccm ni zaidi ya mama yake kwenye siasa. siajabu hata angeshindwa wangemsaidia kuiba, japokuwa uchaguzi wa mwaka huu mzee wakaya kasema kila mmoja kashabaleghe, akajitafutie, asije kulia hapa kila siku baba baba. Pole sana mpendazoe, ndiyo na maanisha pole sana. Hiyo ndo siasa.
   
 19. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Chadema hawakupitisha mtu kinondoni wakati wa kura za maoni?
   
 20. v

  valour Senior Member

  #20
  Aug 3, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ubunge sio kukurupuka ni kupanga mikakati na kuangalia ni jinsi gani unaweza kusaidia sehemu yenye matatizo. Sasa kwenda tu kwenye jimbo mradi liko wazi wananchi tunakuwa na wasiwasi kwa kweli.
   
Loading...