Mpayukaji wa Msemahovyo - Kapayuka!


D

DoubleOSeven

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2008
Messages
661
Likes
12
Points
0
D

DoubleOSeven

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2008
661 12 0
WIKI jana ilikuwa tuandike barua kwa Jack Zumaa kumfahamisha kuwa hatupendi matendo yake.

Kipigo na mauaji ya jamaa yetu yalitufanya tusifanye hivyo. Hata hivyo nina rafiki yangu Sibusiso Sibulele wa Ngubane huko Bondeni. Alinipa mwaliko niende kushuhudia bila kujua nami yangu yanajulikana!

Kwanza naomba vijogoo mnisamehe. Silengi kumnanga mtu bali kueleza ukweli. Nitamnangaje wakati nami ni kijogoo tena kusiri? Ila jina la Jack lapaswa kuchunguzwa kuona ni kwanini kina Jack wanapenda urodi sana.

Ilibidi niende Sauzi kuona wasauzi wanalichukuliaje balaa la uzinzi tena wa mkubwa ili nijiandae kupambana na maswali ya wapiga kura kwenye uchaguzi wa uchafuzi ingawa nilishatabiriwa kushinda kwa kishindo cha radi.

Niliondoka Bongo na pipa la Air South Africa ile iliyoua Air Tanzia. Nilitua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo bila taabu. Huyo! Nilichukua mchuma hadi Kwazulu maeneo ya Mphumalanga.

Stori nilizokuta zinatia kinyaa na kufurahisha! Wasauzi wamegawanyika nusu kwa nusu. Wapo wanaounga mkono uchafu huu kwa vile Jamaa ni mzuluzi mwenzao wanasema; hakuna kosa kwa vile Jack ametoa inhlawulo. Kwa wasiojua lugha ya isizulu, inhlawulo ni faini ya ugoni.

Wapo wanaopinga na kutaka kunywa damu ya Zumaa kwa hasira.

Hakuna kilichonishangaza kama chama cha Zumaa kuunga mkono uzinzi huu unaopingana na sera za serikali kupambana na umeme! Kumbe utumwa mwingine watu huutafuta wenyewe!

Kweli sisi binadamu ni wapuuzi hakuna mfano. Nani angejua kuwa vijogoo wengi wanatucheka sisi vijogoo wenzao kwa vile hawajanaswa? Hata yule DJ aliyefia kifuani angekuwa hai huenda angecheka.

Si ajabu na jamaa yangu naye anachekelea asijue, yake kama yangu, yanajulikana kaya nzima kuwa ana ka-ugonjwa kanakoitwa Tigerwoodiosis karikogundulika huko kwa Joji Kichaka hivi karubuni?

Unajua kijiweni walipopata habari za uchafu na uchafuzi wa Zumaa kabla ya kujua wangu walisemaje? Eti wanataka kuanzia sasa mkuu wa kijiwe hata kaya lazima atangaze idadi ya hawara zake na watoto aliowazaa nje ya ndoa! Hivi wangapi watapona jinai hii?

Kwanza, wanafanya makosa. Hawajui wakuu huwa hatukosei. Hata ukizini, huitwi mzinzi bali dume la mbegu kama rafiki yangu Zumaa.

Hakuna jitu nalichukia kama Msomi. Eti linasema huu ni ufisadi wa ngono! Hivi bila hii kitu lingezaliwa? Linaenda mbele zaidi na kudai ni udhalilishaji wa akina mama utadhani hawapati urodu duniani! Eti linashauri vijogoo wengine wamendee vidosho wa Zumaa hata mimi ili tujue inauma kiasi gani kufanya upuuzi huu!

Bi Mkubwa wangu huwezi kumpata maana nimempa ulaji kwenye NGO. Na kwa vile ana ugonjwa wa gettingrichiosis, sitegemei agawe uroda wangu wala kujali kama ninakula urodi na visichana mitaani hata viwe vibinti vya marafiki zangu au wasaidizi wangu. Penye udhia penyeza rupia.

Halafu eti limsomi linashauri tuokoke! Napiga picha mzee mzima nikianza kujifunga na kusema: Jamani mwenzenu nimeokoka. Lazima nikiri na kutaja dhambi zangu. Kwanza nilizaa na Sofiiii Fyatu wanaharamu wawili ambao nawasomesha Ulaya. Hata huyu bibie napanga kumpa ulaji kijiweni kwa vile ni nyumba yangu ndogo.

Pia lazima niseme wazi na Bwana Yesu anisamehe. Mimi naugua ugonjwa wa ngono uitwao Kwetoisis dogodogozisis.

Pili, lazima nikiri. Huwa nawapeleka dogo dogo zangu nje na kula uroda nao hasa nisipoandamana na bi mkubwa ambaye wabaya wangu wanamwita Shosisto Shari Mpayukaji.


Lazima nizidi kutubu. Mmoja wa nyumba ndogo zangu aitwaye Fatema Allie nimempa ukuu wa kijiwe kwenye wilaya moja ya kijiweni.
Ila mjue. Huyu si mtoto wa rafiki yangu. Mie ni kijogoo hili sipingi. Nina tofauti na Zumaa. Mie siri mayai yangu wala marafiki zangu. Ila yakijileta nalamba. Maana fisi huwa hana mwiko.

Bwana God epushia mbali huyu mdudu wa kufunga kamba watu kuwa nimeokoka asiniingilie. Maana ni aibu! Muhimu lazima nikiri: Bwana hustahili kuja kwangu ila sema neno moja tu roho yangu itapona. Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndiyo maana namtamani hata Bikira Mari… we koma!

Kuna jamaa mmoja katoa mpya. Eti anasema Jack akimuona ndege jike anatamani ambake.

Hivyo, siku hizi hata njiwa wa Kijiweni wamehama kuhofia kufanyiwa mchezo mbaya! Sijui wamama wanaonyonyesha kama wanaweza kupita karibu naye na vichanga vyao! Eti anasema kwenye ikulu ya Jack kuwekwe ubao wenye maandiko: “Bosi ana ugonjwa wa kubaka baka, chunga sana na polisi hawana uwezo kumpa dawa.” Hayo tuyaache.

Turejee kwenye safari yangu ya Sauzi. Wengi wanalalamika kuwa kodi zao zinatumika kugharimia uzinzi wa Bwana Mkubwa. Hata mawaziri wake wanaanza kuogopa kuhusiana na vidosho vyao ukiachia mbali waume wa vidosho vilivyomo kwenye baraza lake la mawiziii.

Lakini wafanye nini iwapo nao wana ugonjwa uitwao Greedforpowersarcoma? Na Jack analijua hili. Anatumia urahisi kama ulimbo kuwanasa akijua hapendwi mtu bali cheo.

Nimempenda kitu kimoja Jack. Yeye ni kihiyo lakini hana vihiyo kwenye baraza lake la mawizi.

Nashukuru Mungu. Maana kama angesoma na kuwa profesa huenda naye angetoa shahada za chupi kama jamaa zangu waliotimuana hivi karibuni kule Kilimani.

Hivi inakuwaje mtu mzima, tena msomi au unayetegemewa kuitwa msomi ukadai au kutoa rushwa ya ngono? Hamuogopi kujidhalilisha ukiachia mbali miwaya jamani? Naona huyu anasoma na kusonya kwa vile naye alipata gamba lake kwa kuvua chup---sorry nonihino yake. Mtakwisha.

Acha uvivu na tamaa. Soma upate shahada yako. Nawe fanya kazi ulipwe mshahara wako. Kama kufundisha kumekushinda unataka kuwa cassanova, si uache uende ukawatafute vyangu pale Ohio. Nawe dada kama kusoma huwezi si uache uende zako Ohio ukauze hilo balaa lako.

Lo! Nimewananga wengine nikajisahau kuwa nami kwenye kijiwe changu nina mpango wa kumendea kagulo fulani kanakojileta leta. Hata hivyo mimi niko juu ya sheria za kijiwe na hata nikikosea sikosei. Mimi ni mtukufu kama Zumaa.

Sisi ni wakubwa bwana na mambo yetu ni makubwa na wengine tunayafanya siri kubwa ati. Uzuri wa Zumaa hafichi kama mimi ingawa naye anatumia pesa ya walipa kodi kufanya ufuska sorry ujogoo sorry, vituz vyake.

Uzuri yeye anatongoza wavaa gauni si wapiga kura kama mimi. Yeye hana uchaguzi wa uchafuzi mwakani kama mimi ambaye sasa mambo ya kutongoza tongoza wavaa gauni nimeacha.

Sasa najishughulisha na kutongoza wapiga kura ili wanipe ulaji tena. Lazima niseme. Kwenye ziara nitazoanza hivi karibuni kufufua ndoa na wapiga kura sitataka miswali ya kipumbavu ya “Umefanya nini kwa miaka yote mitano kwa kijiwe?”

Mimi ni maarufu kuliko chama changu cha UNM kinachoitwa Chama Cha Mafisadi (CCM) na wabaya wangu. Hata watabiri wameishanitabiria kushinda tena kwa kishindo cha mabomu ya Mbagala ati.

Anyway, acha nimalizie stori ya safari yangu bondeni. Una habari nilikaribishwa chakula cha usiku na mzee Zumaa mwenyewe? Huwezi kuamini. Tulikula na kunywa huku akiwa amezungukwa na vishosto vyake.

Alinishauri nami nitangaze hadharani vidosho vyangu badala ya kujinyima raha kukutana navyo kwa shida na gharama kubwa kwa kuogopa walevi. Nilimkubalia. Lakini we, nikitaja si walevi wengi watakufa kwa kihoro maana wengine ni wake za watu.

Baada ya kula chakula cha usiku na mzee Zumaa, siku ya pili nilikwenda Qunu kumsalimia mzee Madiba ambaye alinionya kuhusu mchezo huu mbaya wa kupenda uroda.

Du! Kumbe niko Bongo tena kijiweni Kwa Mfuga Mbwa! Ndoto nyingine bwana.

Acha nikitoe niende kununua pingu ili niwakamate wenye doshi
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,680
Likes
5,094
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,680 5,094 280
Mpayukaji is always the best in this style!!! duh
 
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
duuu...makubwa haya!
 

Forum statistics

Threads 1,251,743
Members 481,857
Posts 29,783,321