Kwanini chadema hawapendi ukweli? na hapo ndo mm huwa siwaamini, kimsingi chadema wanampasuko mkubwa sana, sasa hawa viheleele wa JF muda wote wanachojua wao ni kusema hapana, huo mm huwa naufananisha na ugonjwa wa degedege, Lowasa kimsingi amefeli kuibomoa ccm kwa plani yake ya awali na angefanikiwa mambo yake yangemwendea vizuri, wengi hawaelewi hilo, kwani muda wote wao ni hapana2, Lowasa alitegemea mafuriko kutoka ccm, na ndo maana alisema kabla kwamba ushindi ni asubuhi.
Baada ya kushindwa kuibomoa ccm ile lugha yake ya kushinda asbuhi haisemi sasa, hicho nacho hamukisikii jamani? Lowasa kajikuta mafuriko ni mizigo wenzake ambao kimsingi hawana ushawishi kwa watu, mfano Masha, huyu masha alipigwa chini na wenje na juhudi kubwa alizofanya wakati huo ili atangazwe kuwa yy ndo mshindi, safari hii alikwenda Sengerema nako kapigwa na Ngereja-sasa kaibukia UKAWA.Mgeja pia hana ushawishi Shinyanga, Msindai ndo kabisaa, Dr.Makongoro Mahanga, hayo ndo mafuriko ya Lowasa kupata ushindi, wakaona hali imekuwa mbaya sana, imebidi abembelezwe Sumaye pamoja na tofauti zao za muda mrefu labda anaweza kusaidia ukiweka na kaukanda kao kakishikaji, bado Sumaye kaonekana alikuwa anaitwa Mr.0 maana yake katika mawaziri wakuu wa tz yy ndo alikuwa mzigo. kimsingi hali si shwari ndani ya umoja huo.