Tangu machi 2011, nchi ya Syria imekuwa katika machafuko na hatimaye vita ambapo zaidi ya watu 100,000 wameuawa wengi wakiwa askari wa vikosi vya usalama na maafisa wa kijeshi.
Kwa sasa Syria inakabiliwa na kitisho kutoka USA, Taifa kubwa kabisa lililopanga kuipiga Syria kwa madai kuwa ameruhusu vikosi vyake vitumie silaha za sumu.
Nini yanaweza kuwa madhara ya kushambuliwa Syria na kung'olewa Rais Assad?
(i) Iwapo makundi ya magaidi wa Free Syrian Army (FSA) au Jabhat Al-nusra watafanikiwa kuchukua madaraka, dunia itegemee mauaji makubwa ya jamii za wachache wakiwemo waislamu wa madhehebu ya Shia/Alawi wanaounda 14% ya watu wote na wakristo ambao ni 10%. Ikumbukwe kuwa Assad anaungwa mkono na washia na wakristo
(ii) Iwapo Syria itashambuliwa kuna uwezekano wa kuongezeka kwa makundi ya kigaidi na kuzidi kupata nguvu makundi kama vile Alfarouq Brigade na Islamic State of Iraq
(iii) Kushambuliwa kwa Syria kunaweza kukawa ni chanzo cha vita vikuu vya 3 vya dunia. Maana wakati USA na washirika wake wa Saudia, Qatar, Israel, Uturuki na Ufaransa wamepeleka majeshi na vifaa tayari kwa mashambulizi, Urusi nayo ambaye ni mshirika mkuu wa Assad imepeleka meli zake za kivita katika bahari ya Mediterranean na Rais Putin ameapa kumsaidia Assad. Pia Iran nayo imeapa kumsaidia Assad
(iv) Kushambuliwa na kung'olewa kwa Assad kutafuatiwa na kushambuliwa Hezbollah, Hammas na hatimaye Iran. Baada ya kushambuliwa Iran na kuuvunja ukanda wa kishia (Shiites Crescent) ambao ni washirika wakuu wa Urusi, USA itakuwa tayari imeizunguka Urusi. Ikumbukwe kuwa nchi karibu zote zilizokuwa zikiunda Warsaw Pact kwa sasa zinapiga magoti kuwa wanachama wa NATO
WITO WANGU: Hima hima watanzania na wapenda amani duniani kote, tuombe Mungu aepushe vita hii