Mpango wa mungu ni upi katika mapenzi na ndoa?

Dec 29, 2015
18
41
Hi guys

Hivi karibuni tulikua tunasuluhisha mgogoro wa ndoa wa family friend ambapo niliombwa na kikao kuongea na mwanamke aniambie shida ni nn hasa maana amekua akimsumbua mumewe kwa uzinzi

Sasa kwenye jamii kuna tatizo, wanawake tumeingia kwenye mashindano na wanaume ya mbio za uzinzi, pamoja na sababu zingine lakini lipo moja halizungumzwi sana ila ni tatizo kubwa

Tatizo hilo ni idadi kubwa ya wapenzi ya msichana tangu kuanza ngono hadi kuolewa kwake
Tumuite huyu binti doreen

Doreen, alibikiriwa form 2, form 3 akawa na mtu mwingine, form 4 hakua na mtu, form 5 akarudi kwenye mahusiano tena, wengi mnajua sekondari kumaliza mwaka na mpenzi ni kazi, hivyo form six akawa tena na mpenzi mwingine, na hawa wapenzi wa doreen wengi si wanafunzi wenzie ni mtaani, except yule wa kwanza, mzinduzi, in most cases anakua mwanafunzi mwenxie

Haya chuo
Ni mara chache mapenzi ya high school kwenda nayo chuo, so first year, 1st semester doreen ana mpenzi mpya, most likely a college mate, 2nd semester college mate atapigwa chini, ataona wanaume wa chuo ni watoto hawana pesa, maana hapa sasa anahitaji chumba kichafuke kwa vitu, tv, laptop, sub,-woofer, fashion, nguo za gharama, outings samaki samaki and other reputable high restaurants, since college mate cant afford this kind of life style, then doreen would prefer or would go for someone who is working ie a banker, a lawyer, an engineer, a business man etc

Kuanzia hapa ataanza kubadilisha hawa wafanyakazi, second year mwingine, baadae watashindwana, 3rd year anakuja mwingine tena, hapa sijazungumzia wapenzi watokanao na masomo, supplementally etc

Haya mtaani, kutafuta kazi
Naomba msomaji uendelee kuhesabu idadi ya wapenzi tangu form two
Doreen sasa amemaliza chuo anatafuta kazi, hapa pangeni wenyewe idadi
maana pana changamoto kwa girls
Doreen yupo kazini sasa amepata kazi, na hapo anatokea ""Peter"" hapo kazini, anachanganyikiwa na uzuri wa doreen, wanatokea vijana kadhaa pia wanaingia kwenye hiyo race ya kumpata Doreen
Kutokana na ushindani huo Peter anaona njia pekee ni kutangaza ndoa haraka, bila kuifahamu historia ya mapenzi ya Doreen maana alipomuuliza Doreen mm ni wa ngapi kwako akajibiwa ni wa 3

Sasa swali langu kwenu, mnadhani kwa orodha ya doreen tangu form 2 aanze mapenzi, na kwa pipes mbali mbali alizoziona unadhani peter anaweza kumridhisha Doreen katika maisha yao ya ndoa?
Ni wazi kwamba haiwezekani

Hoja yangu ni kuwa kama ulianza mapenzi secondary ni wazi kuwa utakua na msururu mrefu wa wapenzi hadi unafika kuolewa, na hapa sizungumzii binti malaya wala multiple relationships, nazungumzia unamaliza uhusiano mmoja then mkiachana ndipo unaanzisha mwingine, sasa kwa kuanzia O level hadi college hadi ndoa utakua umefikisha watu wangapi? Na mmeo atakuweza kweli?
Maana umeona wanaodandia kiuno kwa one hour hawashuki,umeona wa 40,30,20,10 minutes etc

Turudi kwenye mpango wa mungu, tendo baada ya ndoa, ikishindikana hiyo at least mtu aanze mapenzi after chuo, wahindi na waarabu ukiwaona couple wakiwa beach ni kushikana tu mikono na kubadilishana mawazo, no sex until marriage,

Kwa wanaume pia ni hivyo, umeshiriki ngono toka secondary school, hadi unafikia ndoa nguvu zote wameshazi proon, kusimamisha ni kwa timing halaf unakuja kuoana na Doreen, just imagine what will happen

Mercy
 
okey .. ila la kushikana shikana halafu useme unasubiria ndoa sijui kama kwa sasa linawezekana may be............ muhimu nikujitahidi kuridhika na uliyeolewa naye
 
Kila kitu kinabadilika, haijalishi uhindini au uarabuni, dunia imebadilika Na kwetu hapa imebadilika Mara kadhaa Zaidi, maana wazazi wa kisasa hawana wanachowafundisha watoto wao!!
 
utu ni kujiheshimu kujitunza ulicho ongea ni kweli kbisa tujaribu kujiheshimu kwa afya zetu
 
Umeongea jambo la maana sana ila mabadiliko ya dunia hii yenye social networks of all kinds na uhuru mkubwa unafanya hilo unaloshauri kuwa gumu kutekelezeka. Pia wazazi wengi kama alivyochangia mdau hapo juu ni kama wamekata tamaa na watoto wao,unakuta wazazi wengi wakisikia binti yao amepata mchumba au yuko na mwanaume basi wanachoomba Mungu ni Aolewe tu,wakiamini ndio solution katika maisha. Wazazi sio wakali na wenye msimamo kama zamani.
 
Tatizo kubwa linaanzia katika malezi hasa wakati wa utoto na kipindi cha balahe yanayofuatia ni matokeao tu.
 
Mtu wanasema haoi lakini kutwa ni kubadili wanawake, likewise kwa wanawake, kujitunza kuna thamani sana.
Ukiachia mwili ovyo, huenda hata ndoa isiwe na amani coz hata kama mumeo/mkeo yupo compatible kwa wakati ule, kuna maradhi ambayo huweza kupunguza uwezo wa mtu kushiriki unyumba. Muhimu sana kujitunza.
 
Turudi kwenye mpango wa mungu, tendo baada ya ndoa, ikishindikana hiyo at least mtu aanze mapenzi after chuo, wahindi na waarabu ukiwaona couple wakiwa beach ni kushikana tu mikono na kubadilishana mawazo, no sex until marriage,

Mercy
Well analysd...
OMG!! sasa ndiyo nikatafute goalkeeper??
 
asante sana agathe jean claudia umenena vyema..
sasa tufanyaje ili haya mambo yasiendelee kwa kizazi kijacho..?
 
Back
Top Bottom