Mpango wa kukuza mfuko wa taasisi za kijamii (NGO,CBO, SC) fundraising program

mrico

Senior Member
Mar 29, 2013
143
225
Tuanzia hapa… Kumekuwa na wimbi kubwa la taasisi za kijamii kuanzishwa, kuyumba hata kupelekea kufa kutokana na ukosefu wa mbinu za kutafuta fedha za kuendeshea shughuli zao au miradi yao.

Nathubutu kusema ni kukosa mbinu za kutafuta fedha kwa sababu fedhaa zipo ila tambua ili uzipate lazima uwe na mbinu pamoja na ubunifu.

Tuanzie hapa… nitaeleza baadhi ya njia ambazo taasisi inaweza kufanya na kujihakikishia uhai wake.

  • Kutafuta ufadhiri kutoka kwa mashirika ya kimataifa: Mashirika ya kimataifa yanayojihusisha na maswala ya kijamii hua yanatafuta mashirika ya ndani ya nchi kadhaa ili kufikisha huduma zao kwa kundi waliolilenga, hivyo hutoa ufadhiri kwa mashirika ya nchi kadhaa yanayojihusisha na huduma au miradi sawa na yao. Kwa kua NGO zipo nyingi inawabidi wapate NGO mahususi kwa kuweka dirisha la maombi.NGO za nchi husika zitatakiwa kutuma maombi ya ufadhili (GRANT PROPOSAL). Unaweza kuona hizi fursa kwa kufanya regular visiting kwenye websites zao.
  • Kutafuta ufadhiri kutoka kwenye makampuni ya ndani ya nchi: Makampuni mengi ya ndani ya nchi huwa yana utaratibu wa kurudisha fadhira kwa jamii kutokana na kutumia huduma zao au bidhaa zao, hivyo inakupasa kujua kampuni husika inapendelea kufadhiri miradi ya aina gani kisha kama NGO yako inafanya miradi sawa na matakwa ya kampuni hiyo basi unapoomba huu ufadhili ni rahisi kupata. Mfano Millicom Tanzania wamekua wakifadhili miradi ya uchimbaji wa visima karibia kila mwaka.. mifano ni mingi sana.. Chakutambua kuwa huku pia wanahitaji proposal yako ya kishindani.
  • Michango kutoka kwa taasisi za ndani: Ikiwa NGO yako imedhamilia kutekeleza mradi au huduma ya kijamii ndani ya jamii ya eneo furani, si jambo mbaya kuhusisha taasisi mbalimbali za eneo hilo ili kupata msaada Zaidi juu ya changamoto mlizonazo taasisi hizo inaweza kuwa kanisa, msikiti, vikundi vya kijamii, n.k.
  • Mfadhiri binafsi: Inaweza kuwa shirika, kampuni au mtu binafsi ambapo mtamwona anaharakati za kijamii basi kama NGO mkithibitisha hilo sasa manapanga mbinu za kumshawishi kufadhili taasisi yako/yenu hili linachukua muda sana ila linapofanikiwa huwa linamanufaa sana kwa sababu taasisi inakuwa na uwakika wa fedha kila mwaka kutoka kwa huyu mfadhili. Moja ya mbinu ya kushawishi ni kumtaka kuwa mlezi au rafiki wa taasisi kwa kumtumia barua ya mwaliko na kuomba meetings za mara kwa mara.
  • Kutumia kampeni: Njia hii ya kutafuta fedha kwa ajiri ya miradi, kuendesha taasisi au kununua asset inahusisha kampeni maalumu ambayo ndani yake kunakuwa na mkusanyiko wa matukio, ,matukio hayo ndio haswa yanayochangisha fedha mfano michezo ya riadha,mpira wa miguu, muziki, bonanza, n.k. Kampeni hizi zinaweza kufanyika kila mwaka (annual appeal campaign) au mara moja baada ya kipindi cha miaka kadhaa (capital campaign). fedha itatoka kwa sponsors, participants na attendees.
Tuanzia hapo kwa sasa.....nitaupdate ikimpendeza mwenyezi mungu..
Nakaribisha mwenye nyama zaidi.

whatsapp /call 0759600809
private fundraising consulting
 

mrico

Senior Member
Mar 29, 2013
143
225
UPDATED

  • Matukio maalumu NGO inaweza kuandaa special event kwa ajili ya kuchangisha fedha na kuonyesha changamoto wanazozipitia. Hapa wanatakiwa kualikwa watu mbalimbali ikiwemo wenye connections Nyingi. Wajumbe wa taasisi lazima waje na list ya watu potentials kuwaalika kwenye tukio hilo. Tukio hili linaweza kuwa chakula cha hisani , mashindano ya michezo, mnada, harambee, n.k.
  • Michango ya mtu kwa mtu Huu ni utaratibu umekua ukionekana sana kwenye kuchangisha fedha kwa kufwata uhusiano binafsi na watu mbalimbali. Kwa hapa Tanzania wanatumia kwa kila mjumbe wa taasisi kupewa fomu maalumu ambayo ataenda kuwachangisha watu anaofahamiana nao au kuwapa fomu watu wengine anaofahamiana nao nao wakawachangishe wanaofahamiana nao. Tunaona kwenye harusi , nyumba za ibada, n.k. Ila kwa wenzetu nchi zilizoendelea wanatumia mifumo ya teknologia ambapo wametengeneza platforms kwa ajili ya kuchangisha fedha ambapo platforms hizi zinaruhusu kuwaalika marafiki zako kutoka kwenye mitandao ya kijamii na kwenda kukuchangia moja kwa moja na fedha inaingia kwenye account yako/ya NGO. Hili linaweza kufanyika hata hapa kwetu ikiwa taasisi na wajumbe wake wataamua kwenda extra miles. Mfano www.givelively.org, www.qgiv.com
final update click here

👉Grant opportunity 28/10/2020
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,887
2,000
Very nice 👍 mimi naomba tu mnimegee hao sponsors wekeni hapa details zao tuingie ndani ☺️☺️☺️☺️🤣😊
 

mrico

Senior Member
Mar 29, 2013
143
225
Very nice 👍 mimi naomba tu mnimegee hao sponsors wekeni hapa details zao tuingie ndani ☺☺☺☺🤣😊
Nitaweka kadri ninavyokutana nazo fursa za sponsors..ila baada ya kumalizia hiyo mada ya fundraising resources bado 2 tips hapo nikipata wakati mzuri nitaanalyz soon...
 

mrico

Senior Member
Mar 29, 2013
143
225
FINAL UPDATE

  • Michango ya hadhara kimtandao: Hii ni mifumo ya kitechnologia inayotumia software ambayo inafanya uchangishaji wa fedha kwa njia ya mtandao, ambapo unatakiwa kujisajili na kuweka mpango wa mradi wako kwenye uwazi na ukweli na dunia nzima itaweza kuona mradi wako ambao wataguswa watachangia. Mfano www.crowdfunding.com (worldwide)www.gogetfunding.com (worldwide)www.wezeshasasa.com (Tanzania)www.changa.co.ke (Kenya) ,zipo nyingi sana……………..
  • Michango ya mauzo: Pia taasisi inaweza kufanya fundraising kwa kuuza huduma au bidhaa. Taasisi inaweza kubuni bidhaa au huduma na kuuza kwa jamii kisha kurejesha asilimia kadhaa kwenye mradi, Member wanaweza kuwa na kipaji au taaluma fulani wakatumia hizo kwa kubuni na kuuza huduma au bidhaa na kuchangia asilimia ya mapato kwenye miradi ya taasisi. Njia nyingine ni taasisi kuomba au kuwa na ubalozi mdogo wa bidhaa au huduma kisha kuitangaza (kuifanyia sales & marketing) na asilimia kadhaa ya mauzo itarudi kuchangia mradi wenu. Mfano hai unaweza kumwangalia mwanamziki Shetta ikitumia kipaji chake cha music kutekeleza miradi ya taasisi yake ya sawa initiative. Pia unaweza kuona kwa taasisi ya Flaviana Matata katikati ya mwaka 2020 ilitambulisha sokoni Lavy Sanitary Pads. Lavy Pads will donate 10 percent of profit from the products which will go directly to help girls in schools. flavianamatata kuzindua PADS
declare an interest
Wadau/wamiliki/ wanaotarajia kuanzisha NGO, CBO nawakaribisha tufanye kazi pamoja kwenye maswala yote ya fundraising kwa ushirikiano mkubwa.

call/whatsapp 0759600809

Naweza saidia kufanya Haya:
General Fundraising consulting
Fundraising Management
Grants Channelings
Grant proposal writing
Fundraising Skills Training
 

mrico

Senior Member
Mar 29, 2013
143
225
Abilis Foundation
Type of projects:
supporting people with disabilities to implement their own projects in developing countries
Location: developing countries
Eligibility: Disabled People's Organisations from developing countries.
Apply here
 

mrico

Senior Member
Mar 29, 2013
143
225
Very nice 👍 mimi naomba tu mnimegee hao sponsors wekeni hapa details zao tuingie ndani ☺☺☺☺🤣😊
Rafto Prize 2021
Type of project:
Recognition to those who fight against oppression. A candidate should be active in the struggle for the ideals and principles underlying the United Nations Universal Declaration of Human Rights and should represent a non-violent perspective.
Location: Worldwide
Eligibility: Individuals or organisations can be nominated
Grant size: $20,000
Deadline: February 1 2021
Apply
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,887
2,000
Rafto Prize 2021
Type of project:
Recognition to those who fight against oppression. A candidate should be active in the struggle for the ideals and principles underlying the United Nations Universal Declaration of Human Rights and should represent a non-violent perspective.
Location: Worldwide
Eligibility: Individuals or organisations can be nominated
Grant size: $20,000
Deadline: February 1 2021
Apply

Cc; Farolito
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom